Check out the new design

Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani. * - Übersetzungen

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Übersetzung der Bedeutungen Surah / Kapitel: Yūnus   Vers:
فَلَوۡلَا كَانَتۡ قَرۡيَةٌ ءَامَنَتۡ فَنَفَعَهَآ إِيمَٰنُهَآ إِلَّا قَوۡمَ يُونُسَ لَمَّآ ءَامَنُواْ كَشَفۡنَا عَنۡهُمۡ عَذَابَ ٱلۡخِزۡيِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٖ
Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda.
Lau kila mji ungeli amini ingeli wafaa Imani yao. Lakini hawaamini, na kwa hivyo hayapatikani manufaa. Ila kaumu ya Yunus. Kwani wao waliamini, na wakapata manufaa yao. Tuliwaondolea hizaya na machungu, na tukawapa starehe ya dunia inayo pita, mpaka ifike Siku ya Kiyama.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَأٓمَنَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ كُلُّهُمۡ جَمِيعًاۚ أَفَأَنتَ تُكۡرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ
Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka watu wote katika ardhi waamini, wangeli amini. Basi wewe usihuzunike kwa ukafiri wa washirikina. Wala haiwi Imani ila kwa khiari. Basi wewe huwezi kuwalazimisha watu kwa nguvu ili wafuate Haki na waitikie. Haikupasii kutaka kuwalazimisha waamini, wala hutoweza, hata ukijitahidi vipi.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تُؤۡمِنَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَجۡعَلُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ
Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao.
Hawezi mtu kuamini ila akiielekeza nafsi yake kwa hayo, na Mwenyezi Mungu akamsahilishia sababu na njia za hayo. Ama yule asiye ielekea Imani huyo basi amestahiki kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu, na kupata adhabu yake. Na mwendo wa Mwenyezi Mungu ni kuwapa adhabu na ghadhabu wale wanao zipuuza na kuzikataa hoja zilio wazi, na wala hawazizingatii.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قُلِ ٱنظُرُواْ مَاذَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَا تُغۡنِي ٱلۡأٓيَٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ
Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini.
Ewe Nabii! Waambie hawa wenye inda: Tazameni Ishara zilizo wazi zinazo onyesha Ungu na Upweke wa Mwenyezi Mungu zilio enea katika mbingu na ardhi. Lakini Ishara, juu ya wingi wake, na maonyo na yangawa na nguvu, hayawafai kitu watu wanao kataa na wala hawatumii akili zao. Hawa wanao kanya kama hawaamini, basi hawatoangalia. Aya hii na Aya nyingi nyenginezo zinaita watu wajifunze kwa kuangalia na kuzingatia (Observation). Na inaita watu wajifunze ilimu ya ulimwengu na viliomo ndani yake, kwani huo ulimwengu umedhalilishwa kwa ajili ya mwanaadamu. Kisha hizo Aya zinataka watu waingie katika ilimu za kujaribu (Experimental Science). Kwani hiyo ni njia ya kujua kwa kuona vinavyo onekana.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
فَهَلۡ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثۡلَ أَيَّامِ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِهِمۡۚ قُلۡ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ
Basi, je! Wanangojea jingine ila kama yaliyo tokea siku za watu walio pita kabla yao? Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanao ngoja.
Basi hao wakanyao wanangojea lolote ila kufikiwa na siku za shida kama zilizo wapata kaumu ya Nuhu, na kaumu ya Musa, na wengineo? Ewe Nabii! Waambie: Ikiwa mnangojea mfano wa hayo, basi ngojeni! Nami pia nangojea pamoja nanyi. Na karibu hivi mtasibiwa na kushindwa, na Siku ya Kiyama mtapata adhabu.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيۡنَا نُنجِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na walio amini. Ndio kama hivyo,inatustahiki kuwaokoa Waumini.
Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na Waumini kutokana na adhabu hiyo. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwaokoa, na ahadi yake ni ya kweli, wala hayendi kinyume.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.
Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa mna shaka na ukweli wa Dini niliyo tumwa kuileta kwenu, basi jueni kuwa kama mtavyo tia shaka mimi kabisa sitoabudu hayo masanamu mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu ambaye mambo yenu yote yapo mikononi mwake. Yeye ndiye anaye kutoeni roho. Na Yeye ameniamrisha niwe katika wanao muamini Yeye.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
وَأَنۡ أَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Na uelekeze uso wako kwenye Dini ya Kweli, wala usiwe katika washirikina.
Ewe Nabii! Simama sawasawa, umuelekee Mwenyezi Mungu vilivyo. Wala usijitie katika miongoni mwa walio mshirikisha Mwenyezi Mungu. Epukana nao, na uwe mbali nao, wewe na Waumini wanao kufuata.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.
Wala usimkimbilie kwa kumwomba na kumuabudu yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Hao hawakuletei manufaa wala madhara. Ukifanya hayo inakuwa umekwisha ingia miongoni mwa washirikina walio dhulumu. Na anayo katazwa Nabii, ndio wanakatazwa umma wake wote. Na hivyo ndio ukomo wa kukanya. Kwani kumkanya ambaye hayumkiniki kutenda anacho kanywa, ndio hadi ya kukanya.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
 
Übersetzung der Bedeutungen Surah / Kapitel: Yūnus
Suren/ Kapiteln Liste Nummer der Seite
 
Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani. - Übersetzungen

Übersetzung von Ali Muhsin Al-Barwani.

Schließen