Check out the new design

Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani. * - Übersetzungen

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Übersetzung der Bedeutungen Surah / Kapitel: Ṣād   Vers:
وَقَالُواْ مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالٗا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ ٱلۡأَشۡرَارِ
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu? [62]
[62] Na watu wa Motoni watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tulikuwa duniani tukiwahisabu kuwa ndio katika waovu, na wa duni, wasio kuwa na jema lolote? Na watu hao ni wale mafakiri wa Kiislamu.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
أَتَّخَذۡنَٰهُمۡ سِخۡرِيًّا أَمۡ زَاغَتۡ عَنۡهُمُ ٱلۡأَبۡصَٰرُ
Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ? [63]
[63] Imekuwaje kuwa sisi tukiwakejeli na wala hawakuingia Motoni pamoja nasi? Au wamekwisha ingia na macho yetu yakazibwa tusiwaone tu?
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقّٞ تَخَاصُمُ أَهۡلِ ٱلنَّارِ
Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni. [64]
[64] Hakika hayo tuliyo yataja ya hadithi ya watu wa Motoni ni kweli ambayo haina budi kutokea, nayo ni ya kugombana kwa watu wa Motoni wao kwa wao.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٞۖ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu, [65]
[65] Ewe Muhammad! Waambie washirikina: Hakika mimi ni mwenye kukuonyeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wake, Mtenda nguvu, Mwenye kumshinda kila mwenye madaraka.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفَّٰرُ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. [66]
[66] Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yao, Mwenye nguvu asiye shindika, Mwenye kusamehe, akazifuta dhambi za mwenye kumuamini.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قُلۡ هُوَ نَبَؤٌاْ عَظِيمٌ
Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa. [67]
[67] Ewe Muhammad! Waambie: Haya ninayo kuambieni ni khabari kubwa, ambazo nyinyi mnazipuuza. Msizikanye!
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
أَنتُمۡ عَنۡهُ مُعۡرِضُونَ
Ambayo nyinyi mnaipuuza. [68]
[68] Ewe Muhammad! Waambie: Haya ninayo kuambieni ni khabari kubwa, ambazo nyinyi mnazipuuza. Msizikanye!
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
مَا كَانَ لِيَ مِنۡ عِلۡمِۭ بِٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰٓ إِذۡ يَخۡتَصِمُونَ
Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana. [69]
[69] Mimi sikuwa nikijua khabari za watukufu walio juu walipo kuwa wakizozana juu ya shauri ya Adam, kwa sababu mimi sikupitia njia za kupata ilimu zilizo zowewa na watu za kusoma vitabu au kupokea masomo kwa wataalamu. Njia yangu mimi ya kujua ni kwa kufunuliwa kwa Wahyi.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِن يُوحَىٰٓ إِلَيَّ إِلَّآ أَنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri. [70]
[70] Na mimi sikufunuliwa kwa Wahyi ila kwamba hakika mimi ni Mtume wa kukufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi kwa njia iliyo wazi kabisa.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن طِينٖ
Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. [71]
[71] Watajie pale alipo sema Mola wako Mlezi kuwaambia Malaika: Mimi nataka umba mtu, naye ni Adam a.s., kutokana na udongo.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ
Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii. [72]
[72] Nikisha timiza kumuumba na nikampulizia siri ya uhai, nayo ni roho, muangukieni kwa kusujudu sijida ya kumtukuza na kumuamkia.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
فَسَجَدَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ
Basi Malaika wakat'ii wote pamoja. [73]
[73] Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِلَّآ إِبۡلِيسَ ٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri. [74]
[74] Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسۡجُدَ لِمَا خَلَقۡتُ بِيَدَيَّۖ أَسۡتَكۡبَرۡتَ أَمۡ كُنتَ مِنَ ٱلۡعَالِينَ
Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? [75]
[75] Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ewe Iblisi! Nini kilicho kuzuilia kumsujudia niliye muumba Mimi mwenyewe bila ya kuingiliwa na yeyote kati yake! Umejiona mkubwa hali nawe si mkubwa, au hakika wewe nafsi yako ni katika walio shinda ukubwa?
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. [76]
[76] Iblisi akasema: Mimi ni bora kuliko Adam; kwani Wewe umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo. Basi vipi mimi nimsujudie yeye?
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. [77]
[77] Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kumlipa Iblisi kwa kiburi chake cha kukataa amri ya Mola wake Mlezi, alimwambia: Basi toka kwenye kundi la watukufu walio juu, kwani wewe umekwisha fukuzwa kutokana na rehema yangu!
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
وَإِنَّ عَلَيۡكَ لَعۡنَتِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo. [78]
[78] Na hakika wewe umetengwa mbali na kila kheri mpaka Siku ya Malipo. Hapo utalipwa kwa sababu ya kunikufuru Mimi na kunifanyia kiburi.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe. [79]
[79] Iblisi akasema: Mola Mlezi! Nipe muhula, wala usinifishe mpaka Siku ya kufufuliwa viumbe.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula, [80]
[80] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi wewe utaakhirishwa, utapewa muhula, mpaka siku ya wakati tunao ujua Sisi, nao ni kumalizika dunia.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ
Mpaka siku ya wakati maalumu. [81]
[81] Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Basi wewe utaakhirishwa, utapewa muhula, mpaka siku ya wakati tunao ujua Sisi, nao ni kumalizika dunia.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote, [82]
[82] Iblisi akasema: Basi naapa kwa Ukubwa wako na Utukufu wako, kwa yakini nitawapoteza watu wote, isipo kuwa waja wako ulio wateuwa kwa ajili ya kukut'ii Wewe. Hao sina madaraka nao.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa. [83]
[83] Isipo kuwa waja wako ulio wateuwa kwa ajili ya kukut'ii Wewe. Hao sina madaraka nao.
Arabische Interpretationen von dem heiligen Quran:
 
Übersetzung der Bedeutungen Surah / Kapitel: Ṣād
Suren/ Kapiteln Liste Nummer der Seite
 
Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani. - Übersetzungen

Übersetzung von Ali Muhsin Al-Barwani.

Schließen