Check out the new design

Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo e ɗemngal Swahili - Ñiiɓirde Ruwwad ngam eggo. * - Tippudi firooji ɗii


Firo maanaaji Simoore: Simoo tuubabuya   Aaya:

At-Tawbah

بَرَآءَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
[Huku ni] kujiweka mbali kutokako kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kunawaendea wale mlioagana nao miongoni mwa washirikina.
Faccirooji aarabeeji:
فَسِيحُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَرۡبَعَةَ أَشۡهُرٖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُخۡزِي ٱلۡكَٰفِرِينَ
Basi tembeeni katika ardhi miezi minne, na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu atawahizi makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
وَأَذَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوۡمَ ٱلۡحَجِّ ٱلۡأَكۡبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِيٓءٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ وَرَسُولُهُۥۚ فَإِن تُبۡتُمۡ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Na ni tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwaendea watu wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu yuko mbali na washirikina, na Mtume wake wake pia yuko mbali. Kwa hivyo, mkitubu, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkigeuka, basi jueni kuwa nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu. Na wabashirie wale waliokufuru adhabu chungu.
Faccirooji aarabeeji:
إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ثُمَّ لَمۡ يَنقُصُوكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَمۡ يُظَٰهِرُواْ عَلَيۡكُمۡ أَحَدٗا فَأَتِمُّوٓاْ إِلَيۡهِمۡ عَهۡدَهُمۡ إِلَىٰ مُدَّتِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ
Isipokuwa wale mlioahidiana nao katika washirikina, kisha hawakuwapunguza chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu. Basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wachamungu.
Faccirooji aarabeeji:
فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلۡأَشۡهُرُ ٱلۡحُرُمُ فَٱقۡتُلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡ وَخُذُوهُمۡ وَٱحۡصُرُوهُمۡ وَٱقۡعُدُواْ لَهُمۡ كُلَّ مَرۡصَدٖۚ فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّواْ سَبِيلَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na ikiisha miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni na wazingireni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni njia yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
وَإِنۡ أَحَدٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ٱسۡتَجَارَكَ فَأَجِرۡهُ حَتَّىٰ يَسۡمَعَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبۡلِغۡهُ مَأۡمَنَهُۥۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡلَمُونَ
Na ikiwa yeyote miongoni mwa washirikina atakuomba ulinzi, basi mpe ulinzi ili apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahali pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni kaumu wasiojua kitu.
Faccirooji aarabeeji:
كَيۡفَ يَكُونُ لِلۡمُشۡرِكِينَ عَهۡدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ فَمَا ٱسۡتَقَٰمُواْ لَكُمۡ فَٱسۡتَقِيمُواْ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ
Vipi washirikina watakuwa na agano kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake, isipokuwa wale mliofanya agano nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu watawawia wanyoofu, basi nanyi pia wawieni wanyoofu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamungu.
Faccirooji aarabeeji:
كَيۡفَ وَإِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ لَا يَرۡقُبُواْ فِيكُمۡ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ يُرۡضُونَكُم بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَتَأۡبَىٰ قُلُوبُهُمۡ وَأَكۡثَرُهُمۡ فَٰسِقُونَ
Vipi, na wakiwa na ushindi dhidi yenu, hawachungi kwenu udugu wala ahadi. Wanawafurahisha kwa midomo yao tu, lakini nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
ٱشۡتَرَوۡاْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلٗا فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Walinunua Ishara za Mwenyezi Mungu kwa thamani chache, kwa hivyo wakaizuilia njia yake. Hakika hao ni maovu waliyokuwa wakiyatenda.
Faccirooji aarabeeji:
لَا يَرۡقُبُونَ فِي مُؤۡمِنٍ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُعۡتَدُونَ
Hawachungi kwa Muumini udugu wala ahadi. Basi hao ndio wapindukiao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِۗ وَنُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ
Kwa hivyo wakitubu, na wakasimamisha Sala, na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazipambanua Aya kwa kaumu wanaojua.
Faccirooji aarabeeji:
وَإِن نَّكَثُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُم مِّنۢ بَعۡدِ عَهۡدِهِمۡ وَطَعَنُواْ فِي دِينِكُمۡ فَقَٰتِلُوٓاْ أَئِمَّةَ ٱلۡكُفۡرِ إِنَّهُمۡ لَآ أَيۡمَٰنَ لَهُمۡ لَعَلَّهُمۡ يَنتَهُونَ
Na wakivunja viapo vyao baada ya agano lao, na wakaitia dosari Dini yenu, basi piganeni na viongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha.
Faccirooji aarabeeji:
أَلَا تُقَٰتِلُونَ قَوۡمٗا نَّكَثُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ وَهَمُّواْ بِإِخۡرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٍۚ أَتَخۡشَوۡنَهُمۡۚ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخۡشَوۡهُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
Je, hampigani na kaumu waliovunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumtoa Mtume, nao ndio waliowaanza mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mmwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.
Faccirooji aarabeeji:
قَٰتِلُوهُمۡ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ بِأَيۡدِيكُمۡ وَيُخۡزِهِمۡ وَيَنصُرۡكُمۡ عَلَيۡهِمۡ وَيَشۡفِ صُدُورَ قَوۡمٖ مُّؤۡمِنِينَ
Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na awanusuru dhidi yao, na aviponye vifua vya kaumu ya Waumini.
Faccirooji aarabeeji:
وَيُذۡهِبۡ غَيۡظَ قُلُوبِهِمۡۗ وَيَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima kubwa.
Faccirooji aarabeeji:
أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تُتۡرَكُواْ وَلَمَّا يَعۡلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ مِنكُمۡ وَلَمۡ يَتَّخِذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَلِيجَةٗۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ
Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, na Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu, na wala hawakumfanya yeyote mwendani wao isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
Faccirooji aarabeeji:
مَا كَانَ لِلۡمُشۡرِكِينَ أَن يَعۡمُرُواْ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ شَٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلۡكُفۡرِۚ أُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ وَفِي ٱلنَّارِ هُمۡ خَٰلِدُونَ
Haikuwa kwa washirikina kwamba waiimarishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa wanazishuhudia nafsi zao wenyewe ukafiri. Hao matendo yao yaliharibika, na katika Moto wao watadumu.
Faccirooji aarabeeji:
إِنَّمَا يَعۡمُرُ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمۡ يَخۡشَ إِلَّا ٱللَّهَۖ فَعَسَىٰٓ أُوْلَٰٓئِكَ أَن يَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ
Hakika anayeimarisha tu misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akasimamisha Sala, na akatoa Zaka, na wala hakumnyenyekea isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.
Faccirooji aarabeeji:
۞ أَجَعَلۡتُمۡ سِقَايَةَ ٱلۡحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ كَمَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَجَٰهَدَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ لَا يَسۡتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuimarisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu dhalimu.
Faccirooji aarabeeji:
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ أَعۡظَمُ دَرَجَةً عِندَ ٱللَّهِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ
Wale walioamini, na wakahama, na wakafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao wana daraja kubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofuzu.
Faccirooji aarabeeji:
يُبَشِّرُهُمۡ رَبُّهُم بِرَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَرِضۡوَٰنٖ وَجَنَّٰتٖ لَّهُمۡ فِيهَا نَعِيمٞ مُّقِيمٌ
Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo wana neema za kudumu.
Faccirooji aarabeeji:
خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ
Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَابَآءَكُمۡ وَإِخۡوَٰنَكُمۡ أَوۡلِيَآءَ إِنِ ٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡكُفۡرَ عَلَى ٱلۡإِيمَٰنِۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa marafiki walinzi wenu ikiwa wanaupendelea ukafiri kuliko Imani. Na mwenye kuwafanya marafiki walinzi miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu.
Faccirooji aarabeeji:
قُلۡ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ وَإِخۡوَٰنُكُمۡ وَأَزۡوَٰجُكُمۡ وَعَشِيرَتُكُمۡ وَأَمۡوَٰلٌ ٱقۡتَرَفۡتُمُوهَا وَتِجَٰرَةٞ تَخۡشَوۡنَ كَسَادَهَا وَمَسَٰكِنُ تَرۡضَوۡنَهَآ أَحَبَّ إِلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٖ فِي سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Sema: Ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibika kwake, na makazi mnayoyaridhia, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu aje na amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
لَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٖ وَيَوۡمَ حُنَيۡنٍ إِذۡ أَعۡجَبَتۡكُمۡ كَثۡرَتُكُمۡ فَلَمۡ تُغۡنِ عَنكُمۡ شَيۡـٔٗا وَضَاقَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ ثُمَّ وَلَّيۡتُم مُّدۡبِرِينَ
Hakika Mwenyezi Mungu aliwanusuru katika maeneo mengi, na siku ya Hunayni wakati wingi wenu uliwapa majivuno, lakini haukuwafaa kitu, na ardhi ikawa finyu kwenu pamoja na upana wake. Kisha mkageuka mkapeana migongo.
Faccirooji aarabeeji:
ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini. Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
ثُمَّ يَتُوبُ ٱللَّهُ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atamkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡمُشۡرِكُونَ نَجَسٞ فَلَا يَقۡرَبُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ بَعۡدَ عَامِهِمۡ هَٰذَاۚ وَإِنۡ خِفۡتُمۡ عَيۡلَةٗ فَسَوۡفَ يُغۡنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦٓ إِن شَآءَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na ikiwa mnahofia umasikini, basi Mwenyezi Mungu atawatajirisha kutoka katika fadhila zake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima kubwa.
Faccirooji aarabeeji:
قَٰتِلُواْ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ ٱلۡحَقِّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ حَتَّىٰ يُعۡطُواْ ٱلۡجِزۡيَةَ عَن يَدٖ وَهُمۡ صَٰغِرُونَ
Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharamishi yale aliyoharimisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawashiki Dini ya haki, miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa hiari yao, hali wametii.
Faccirooji aarabeeji:
وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ عُزَيۡرٌ ٱبۡنُ ٱللَّهِ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَى ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ ٱللَّهِۖ ذَٰلِكَ قَوۡلُهُم بِأَفۡوَٰهِهِمۡۖ يُضَٰهِـُٔونَ قَوۡلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُۚ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۖ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ
Na Mayahudi walisema: Uzeir ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Na Wakristo walisema: Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kauli yao tu kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Faccirooji aarabeeji:
ٱتَّخَذُوٓاْ أَحۡبَارَهُمۡ وَرُهۡبَٰنَهُمۡ أَرۡبَابٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُوٓاْ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗاۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ سُبۡحَٰنَهُۥ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Waliwafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni mabwana badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu Mmoja, hapana mungu isipokuwa Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayoyashirikisha.
Faccirooji aarabeeji:
يُرِيدُونَ أَن يُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَيَأۡبَى ٱللَّهُ إِلَّآ أَن يُتِمَّ نُورَهُۥ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa aitimize Nuru yake hata makafiri wakichukia.
Faccirooji aarabeeji:
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ
Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili aipe ushindi juu ya dini zote, hata washirikina wakichukia.
Faccirooji aarabeeji:
۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡأَحۡبَارِ وَٱلرُّهۡبَانِ لَيَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۗ وَٱلَّذِينَ يَكۡنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلۡفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٖ
Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wanaolimbika dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu chungu.
Faccirooji aarabeeji:
يَوۡمَ يُحۡمَىٰ عَلَيۡهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكۡوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمۡ وَجُنُوبُهُمۡ وَظُهُورُهُمۡۖ هَٰذَا مَا كَنَزۡتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡ فَذُوقُواْ مَا كُنتُمۡ تَكۡنِزُونَ
Siku zitakapotiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mliyozilimbikia nafsi zenu. Basi onjeni mliyokuwa mkilimbika.
Faccirooji aarabeeji:
إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَهۡرٗا فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ مِنۡهَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُمٞۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُۚ فَلَا تَظۡلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمۡۚ وَقَٰتِلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ كَآفَّةٗ كَمَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ كَآفَّةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ
Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili katika andiko la Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu.
Faccirooji aarabeeji:
إِنَّمَا ٱلنَّسِيٓءُ زِيَادَةٞ فِي ٱلۡكُفۡرِۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُحِلُّونَهُۥ عَامٗا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامٗا لِّيُوَاطِـُٔواْ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّواْ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُۚ زُيِّنَ لَهُمۡ سُوٓءُ أَعۡمَٰلِهِمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hakika kuahirisha (miezi) ni kuzidi tu katika kukufuru; wanapotezwa kwa hilo wale waliokufuru. Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharimisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Mwenyezi Mungu, ndiyo wahalalishe yale aliyoyaharimisha Mwenyezi Mungu. Wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَا لَكُمۡ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلۡتُمۡ إِلَى ٱلۡأَرۡضِۚ أَرَضِيتُم بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ فَمَا مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ
Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera siyo isipokuwa chache.
Faccirooji aarabeeji:
إِلَّا تَنفِرُواْ يُعَذِّبۡكُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَيَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيۡـٔٗاۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Kama hamuendi, atawaadhibu adhabu chungu, na atawabadilisha na kaumu wasiokuwa nyinyi, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Faccirooji aarabeeji:
إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدۡ نَصَرَهُ ٱللَّهُ إِذۡ أَخۡرَجَهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ثَانِيَ ٱثۡنَيۡنِ إِذۡ هُمَا فِي ٱلۡغَارِ إِذۡ يَقُولُ لِصَٰحِبِهِۦ لَا تَحۡزَنۡ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَنَاۖ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَيۡهِ وَأَيَّدَهُۥ بِجُنُودٖ لَّمۡ تَرَوۡهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلسُّفۡلَىٰۗ وَكَلِمَةُ ٱللَّهِ هِيَ ٱلۡعُلۡيَاۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipomtoa wale waliokufuru, akiwa ni wa pili wa wawili walipokuwa katika pango, alipomwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Basi Mwenyezi Mungu akauteremsha utulivu wake juu yake, na akamuunga mkono kwa majeshi ambayo hamkuyaona, na akalifanya neno la wale waliokufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
ٱنفِرُواْ خِفَافٗا وَثِقَالٗا وَجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Tokeni muende mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hayo ni heri kwenu ikiwa mnajua.
Faccirooji aarabeeji:
لَوۡ كَانَ عَرَضٗا قَرِيبٗا وَسَفَرٗا قَاصِدٗا لَّٱتَّبَعُوكَ وَلَٰكِنۢ بَعُدَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلشُّقَّةُۚ وَسَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَوِ ٱسۡتَطَعۡنَا لَخَرَجۡنَا مَعَكُمۡ يُهۡلِكُونَ أَنفُسَهُمۡ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Lau ingelikuwa ipo faida ya papo kwa hapo, na safari fupi, basi hakika wangelikufuata. Lakini wameona ni mbali na kuna mashaka. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: Tungeliweza, basi bila ya shaka tungelitoka pamoja nanyi. Wanaziangamiza nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo.
Faccirooji aarabeeji:
عَفَا ٱللَّهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمۡ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَتَعۡلَمَ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Mwenyezi Mungu amekusamehe! Kwa nini ukawapa ruhusa kabla ya kukubainikia wale wanaosema ukweli, na ukawajua waongo?
Faccirooji aarabeeji:
لَا يَسۡتَـٔۡذِنُكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أَن يُجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلۡمُتَّقِينَ
Hawakuombi ruhusa wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho ili wafanye Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema wachamungu.
Faccirooji aarabeeji:
إِنَّمَا يَسۡتَـٔۡذِنُكَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَٱرۡتَابَتۡ قُلُوبُهُمۡ فَهُمۡ فِي رَيۡبِهِمۡ يَتَرَدَّدُونَ
Hakika wanakuomba ruhusa tu wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zikatia shaka. Basi hao wanasitasita katika shaka yao.
Faccirooji aarabeeji:
۞ وَلَوۡ أَرَادُواْ ٱلۡخُرُوجَ لَأَعَدُّواْ لَهُۥ عُدَّةٗ وَلَٰكِن كَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمۡ فَثَبَّطَهُمۡ وَقِيلَ ٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ
Na wangelitaka kweli kutoka, basi bila ya shaka wangelikuandalia maandalizi. Lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao, kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa!
Faccirooji aarabeeji:
لَوۡ خَرَجُواْ فِيكُم مَّا زَادُوكُمۡ إِلَّا خَبَالٗا وَلَأَوۡضَعُواْ خِلَٰلَكُمۡ يَبۡغُونَكُمُ ٱلۡفِتۡنَةَ وَفِيكُمۡ سَمَّٰعُونَ لَهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ
Lau wangelitoka kati yenu, wasingeliwazidisha isipokuwa mchafuko, na wangetangatanga kati yenu wakiwatakia fitina. Na miongoni mwenu wapo wanaowasikiliza sana. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.
Faccirooji aarabeeji:
لَقَدِ ٱبۡتَغَوُاْ ٱلۡفِتۡنَةَ مِن قَبۡلُ وَقَلَّبُواْ لَكَ ٱلۡأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَظَهَرَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَهُمۡ كَٰرِهُونَ
Hakika, walikwisha taka fitina tangu zamani, na wakakugeuzia mambo, mpaka ikaja haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu hali kuwa wao wamechukia.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ ٱئۡذَن لِّي وَلَا تَفۡتِنِّيٓۚ أَلَا فِي ٱلۡفِتۡنَةِ سَقَطُواْۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ
Na miongoni mwao wapo wanaosema: Niruhusu wala usinifitini. Kwa yakini wao hivyo wamekwishatumbukia katika fitina. Na hakika Jahannam imewazunguka makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
إِن تُصِبۡكَ حَسَنَةٞ تَسُؤۡهُمۡۖ وَإِن تُصِبۡكَ مُصِيبَةٞ يَقُولُواْ قَدۡ أَخَذۡنَآ أَمۡرَنَا مِن قَبۡلُ وَيَتَوَلَّواْ وَّهُمۡ فَرِحُونَ
Likikupata zuri, linawawia baya. Na ukikusibu msiba, wanasema: Sisi hakika tuliangalia mambo yetu vizuri tangu zamani. Na wanageuka kwenda zao hali ya kuwa wamefurahi.
Faccirooji aarabeeji:
قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Sema: Halitusibu isipokuwa yale aliyotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini!
Faccirooji aarabeeji:
قُلۡ هَلۡ تَرَبَّصُونَ بِنَآ إِلَّآ إِحۡدَى ٱلۡحُسۡنَيَيۡنِۖ وَنَحۡنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمۡ أَن يُصِيبَكُمُ ٱللَّهُ بِعَذَابٖ مِّنۡ عِندِهِۦٓ أَوۡ بِأَيۡدِينَاۖ فَتَرَبَّصُوٓاْ إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ
Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipokuwa moja katika mazuri mawili? Na sisi tunawatazamia kuwa Mwenyezi Mungu atawasibu kwa adhabu kutoka kwake, au kwa mikono yetu. Basi tazamieni, nasi hakika tunatazamia pamoja nanyi.
Faccirooji aarabeeji:
قُلۡ أَنفِقُواْ طَوۡعًا أَوۡ كَرۡهٗا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمۡ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ
Sema: Toeni kwa kupenda au kwa kuchukia. Kamwe hakitakubaliwa kutoka kwenu. Kwani hakika nyinyi mmekuwa kaumu wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
وَمَا مَنَعَهُمۡ أَن تُقۡبَلَ مِنۡهُمۡ نَفَقَٰتُهُمۡ إِلَّآ أَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأۡتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمۡ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمۡ كَٰرِهُونَ
Na hawakuzuiliwa kukubaliwa kutoa kwao isipokuwa kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala isipokuwa huku ni wavivu, wala hawatoi isipokuwa nao wamechukia.
Faccirooji aarabeeji:
فَلَا تُعۡجِبۡكَ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُمۡۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَتَزۡهَقَ أَنفُسُهُمۡ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ
Basi zisikufurahishe mali zao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwazo katika maisha ya dunia hii, na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
وَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنَّهُمۡ لَمِنكُمۡ وَمَا هُم مِّنكُمۡ وَلَٰكِنَّهُمۡ قَوۡمٞ يَفۡرَقُونَ
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao si katika nyinyi. Lakini wao ni kaumu wanaoogopa.
Faccirooji aarabeeji:
لَوۡ يَجِدُونَ مَلۡجَـًٔا أَوۡ مَغَٰرَٰتٍ أَوۡ مُدَّخَلٗا لَّوَلَّوۡاْ إِلَيۡهِ وَهُمۡ يَجۡمَحُونَ
Lau kama watapata pa kukimbilia au mapango au pahala pa kuingia, basi hakika wangeligeuka kwenda huko huku wanakimbia mbio zisizozuilika.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِنۡهُم مَّن يَلۡمِزُكَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ فَإِنۡ أُعۡطُواْ مِنۡهَا رَضُواْ وَإِن لَّمۡ يُعۡطَوۡاْ مِنۡهَآ إِذَا هُمۡ يَسۡخَطُونَ
Na miongoni mwao kuna yule anayekusengenya katika kuhusiana na sadaka. Kwa hivyo wakipewa kwayo, wanaridhika. Na wasipopewa kwayo, tazama, wanakasirika.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَوۡ أَنَّهُمۡ رَضُواْ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَقَالُواْ حَسۡبُنَا ٱللَّهُ سَيُؤۡتِينَا ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ وَرَسُولُهُۥٓ إِنَّآ إِلَى ٱللَّهِ رَٰغِبُونَ
Na lau kuwa waliridhia kile alichowapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila yake, na pia Mtume wake; hakika sisi ni wenye kumtaka Mwenyezi Mungu!
Faccirooji aarabeeji:
۞ إِنَّمَا ٱلصَّدَقَٰتُ لِلۡفُقَرَآءِ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡعَٰمِلِينَ عَلَيۡهَا وَٱلۡمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمۡ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَٱلۡغَٰرِمِينَ وَفِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۖ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Hakika sadaka ni za mafakiri tu, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na waliogharamika, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu uliofaridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِنۡهُمُ ٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱلنَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٞۚ قُلۡ أُذُنُ خَيۡرٖ لَّكُمۡ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَيُؤۡمِنُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ رَسُولَ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na miongoni mwao kuna wale wanaomuudhi Nabii na wanasema: Yeye ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la heri kwenu. Anamwamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanaoamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wana adhabu chungu.
Faccirooji aarabeeji:
يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ لِيُرۡضُوكُمۡ وَٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَحَقُّ أَن يُرۡضُوهُ إِن كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ
Wanawaapia kwa Mwenyezi Mungu ili wawaridhishe nyinyi, ilhali Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaostahiki zaidi kwamba wao wawaridhishe ikiwa wao ni Waumini.
Faccirooji aarabeeji:
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدٗا فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡخِزۡيُ ٱلۡعَظِيمُ
Je, hawajui ya kwamba anayempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo hakika ana Moto wa Jahannam adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa.
Faccirooji aarabeeji:
يَحۡذَرُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيۡهِمۡ سُورَةٞ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمۡۚ قُلِ ٱسۡتَهۡزِءُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ مُخۡرِجٞ مَّا تَحۡذَرُونَ
Wanafiki wanaogopa kwamba iteremshwe Sura juu yao itakayowaambia yale yaliyo katika nyoyo zao. Sema: Fanyeni stihizai! Hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayoyaogopa.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَئِن سَأَلۡتَهُمۡ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلۡعَبُۚ قُلۡ أَبِٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ وَرَسُولِهِۦ كُنتُمۡ تَسۡتَهۡزِءُونَ
Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Kwani mlikuwa mkimfanyia masikhara Mwenyezi Mungu, na ishara zake, na Mtume wake?
Faccirooji aarabeeji:
لَا تَعۡتَذِرُواْ قَدۡ كَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡۚ إِن نَّعۡفُ عَن طَآئِفَةٖ مِّنكُمۡ نُعَذِّبۡ طَآئِفَةَۢ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Msitoe udhuru. Hakika mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja miongoni mwenu, tunaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao wamekuwa wahalifu.
Faccirooji aarabeeji:
ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ بَعۡضُهُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمُنكَرِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَقۡبِضُونَ أَيۡدِيَهُمۡۚ نَسُواْ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمۡۚ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ
Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na hukataza mema, na huifumba mikono yao. Walimsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia akawasahau. Hakika wanafiki ndio wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ هِيَ حَسۡبُهُمۡۚ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ
Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu watadumu humo. Hiyo ndiyo inawatosha, na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu ya kudumu.
Faccirooji aarabeeji:
كَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ كَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنكُمۡ قُوَّةٗ وَأَكۡثَرَ أَمۡوَٰلٗا وَأَوۡلَٰدٗا فَٱسۡتَمۡتَعُواْ بِخَلَٰقِهِمۡ فَٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِخَلَٰقِكُمۡ كَمَا ٱسۡتَمۡتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُم بِخَلَٰقِهِمۡ وَخُضۡتُمۡ كَٱلَّذِي خَاضُوٓاْۚ أُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Ni kama wale waliokuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuwaliko nyinyi. Basi walistareheka na fungu lao, na nyinyi mnastareheka na fungu lenu, kama walivyostareheka kwa fungu lao wale waliokuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyozama. Hao, matendo yao yaliharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliohasiri.
Faccirooji aarabeeji:
أَلَمۡ يَأۡتِهِمۡ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَقَوۡمِ إِبۡرَٰهِيمَ وَأَصۡحَٰبِ مَدۡيَنَ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتِۚ أَتَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Je, hazikuwajia habari za wale waliokuwa kabla yao, kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyopinduliwa chini juu? Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Faccirooji aarabeeji:
وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ سَيَرۡحَمُهُمُ ٱللَّهُۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na husimamisha Sala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّٰتِ عَدۡنٖۚ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani zipitiazo mito chini yake, watadumu humo. Na makazi mema katika Bustani za kudumu, na Radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndizo kubwa zaidi kuliko yote. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na wawiye mgumu. Na makazi yao ni Jahannamu, na hapo ndipo pabaya zaidi pa kuishia.
Faccirooji aarabeeji:
يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُواْ وَلَقَدۡ قَالُواْ كَلِمَةَ ٱلۡكُفۡرِ وَكَفَرُواْ بَعۡدَ إِسۡلَٰمِهِمۡ وَهَمُّواْ بِمَا لَمۡ يَنَالُواْۚ وَمَا نَقَمُوٓاْ إِلَّآ أَنۡ أَغۡنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضۡلِهِۦۚ فَإِن يَتُوبُواْ يَكُ خَيۡرٗا لَّهُمۡۖ وَإِن يَتَوَلَّوۡاْ يُعَذِّبۡهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَا لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ
Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; nao hakika wamekwisha sema neno la ukafiri, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakawa na utashi mkubwa juu ya yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia ila kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwatajirisha, na Mtume wake pia kutokana na fadhila zake. Basi wakitubu, itakuwa heri kwao. Na wakigeuka, Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na wala hawana katika ardhi mlinzi yeyote wala wa kuwanusuru.
Faccirooji aarabeeji:
۞ وَمِنۡهُم مَّنۡ عَٰهَدَ ٱللَّهَ لَئِنۡ ءَاتَىٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na miongoni mwao kuwa wale waliomuahidi Mwenyezi Mungu kwamba: Akitupa katika fadhila yake, hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika waliotengenea.
Faccirooji aarabeeji:
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُم مِّن فَضۡلِهِۦ بَخِلُواْ بِهِۦ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ
Basi alipowapa katika fadhila yake, wakaifanyia ubahili na wakageuka hali ya kuwa wamepeana mgongo.
Faccirooji aarabeeji:
فَأَعۡقَبَهُمۡ نِفَاقٗا فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ يَلۡقَوۡنَهُۥ بِمَآ أَخۡلَفُواْ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُواْ يَكۡذِبُونَ
Basi akawafuatisha unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakapokutana naye, kwa sababu ya kuwa walimvunjia Mwenyezi Mungu yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uongo.
Faccirooji aarabeeji:
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ سِرَّهُمۡ وَنَجۡوَىٰهُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu?
Faccirooji aarabeeji:
ٱلَّذِينَ يَلۡمِزُونَ ٱلۡمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهۡدَهُمۡ فَيَسۡخَرُونَ مِنۡهُمۡ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنۡهُمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Wale wanaowabeua Waumini wanaotoa sadaka nyingi na wasio nacho cha kutoa ila kiasi cha juhudi yao, hivyo wanawafanyia masikhara. Mwenyezi Mungu atawakejeli wao! Nao wana adhabu chungu!
Faccirooji aarabeeji:
ٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ أَوۡ لَا تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ إِن تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ سَبۡعِينَ مَرَّةٗ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Waombee kusitiriwa dhambi, au usiwaombee kusitiriwa dhambi. Hata ukiwaombea kusitiriwa dhambi mara sabini, Mwenyezi Mungu hatawasitiria dhambi. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
فَرِحَ ٱلۡمُخَلَّفُونَ بِمَقۡعَدِهِمۡ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓاْ أَن يُجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُواْ لَا تَنفِرُواْ فِي ٱلۡحَرِّۗ قُلۡ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرّٗاۚ لَّوۡ كَانُواْ يَفۡقَهُونَ
Walifurahi walioachwa nyuma kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wakachukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakasema: Msitoke kwenda katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto kubwa zaidi, laiti wangelikuwa wanafahamu!
Faccirooji aarabeeji:
فَلۡيَضۡحَكُواْ قَلِيلٗا وَلۡيَبۡكُواْ كَثِيرٗا جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Basi na wacheke kidogo, na walie sana. Hayo ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Faccirooji aarabeeji:
فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٖ مِّنۡهُمۡ فَٱسۡتَـٔۡذَنُوكَ لِلۡخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخۡرُجُواْ مَعِيَ أَبَدٗا وَلَن تُقَٰتِلُواْ مَعِيَ عَدُوًّاۖ إِنَّكُمۡ رَضِيتُم بِٱلۡقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٖ فَٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡخَٰلِفِينَ
Basi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na wakakutaka idhini ya kutoka - basi sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami. Hakika nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao waliobakia nyuma.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰٓ أَحَدٖ مِّنۡهُم مَّاتَ أَبَدٗا وَلَا تَقُمۡ عَلَىٰ قَبۡرِهِۦٓۖ إِنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَمَاتُواْ وَهُمۡ فَٰسِقُونَ
Wala usimsalie kabisa yeyote katika wao akifa, wala usisimame kaburini kwake. Hakika hao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakafa na hali ni wamevuka mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَا تُعۡجِبۡكَ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَأَوۡلَٰدُهُمۡۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَتَزۡهَقَ أَنفُسُهُمۡ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ
Wala zisikupendeze mali zao na watoto wao. Mwenyezi Mungu anataka tu kuwaadhibu kwa hayo katika dunia; na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
وَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٌ أَنۡ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَجَٰهِدُواْ مَعَ رَسُولِهِ ٱسۡتَـٔۡذَنَكَ أُوْلُواْ ٱلطَّوۡلِ مِنۡهُمۡ وَقَالُواْ ذَرۡنَا نَكُن مَّعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ
Na inapoteremshwa Sura kwamba muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye nguvu miongoni mwao hukutaka ruhusa na wanasema: Tuache tuwe pamoja na wanaokaa nyuma!
Faccirooji aarabeeji:
رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ
Waliridhia kwamba wawe pamoja na wabakiao nyuma, na nyoyo zao zikafunikwa, kwa hivyo hawafahamu.
Faccirooji aarabeeji:
لَٰكِنِ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ جَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡخَيۡرَٰتُۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Lakini Mtume na wale walioamini pamoja naye, walifanya Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na hao ndio wana heri nyingi. Na hao ndio waliofaulu.
Faccirooji aarabeeji:
أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Mwenyezi Mungu amewaandalia Bustani zipitazo mito kwa chini yake, watadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Faccirooji aarabeeji:
وَجَآءَ ٱلۡمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ لِيُؤۡذَنَ لَهُمۡ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na walikuja wenye kutoa udhuru miongoni mwa Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale waliomdanganya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Itawafika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu.
Faccirooji aarabeeji:
لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakuna lawama juu ya wanyonge, wala juu ya wagonjwa, wala juu ya wale wasiopata cha kutoa, maadamu wanamsafia nia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوۡكَ لِتَحۡمِلَهُمۡ قُلۡتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحۡمِلُكُمۡ عَلَيۡهِ تَوَلَّواْ وَّأَعۡيُنُهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُواْ مَا يُنفِقُونَ
Wala wale wanaokujia ili uwape kipando, ukasema: Sina kipando cha kuwakubebea juu yake, kwa hivyo wanageuka kwenda huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kwamba hawatapata cha kutoa.
Faccirooji aarabeeji:
۞ إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Hakika njia ya lawama iko tu juu ya wale wanaokuomba ruhusa wasiende vitani ilhali wao ni matajiri. Waliridhia kwamba wawe pamoja na wanaosalia nyuma. Na Mwenyezi Mungu akaiziba mioyo yao. Kwa hivyo hawajui.
Faccirooji aarabeeji:
يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Watawatolea udhuru mtakapowarudia. Sema: Msitoe udhuru; hatutawaamini. Mwenyezi Mungu amekwisha tujulisha habari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri; naye atawaambia mliyokuwa mkiyatenda.
Faccirooji aarabeeji:
سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Watawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najisi, na makaazi yao ni Jahannam, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
Faccirooji aarabeeji:
يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ لِتَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡۖ فَإِن تَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرۡضَىٰ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Wanawaapia ili muwe radhi nao. Lakini hata mkiwa radhi nao nyiye, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka.
Faccirooji aarabeeji:
ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Mabedui ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ
Na katika Mabedui hao kuna yule anayefikiri kuwa kile wanachotoa ni gharama ya bure, na anawatazamia nyinyi mambo yawageukie. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na katika Mabedui kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kuwasogeza karibu kwa Mwenyezi Mungu na ya kupatia dua za Mtume. Ndiyo! Hizo hakika ni mambo ya kuwasogeza wao karibu. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلۡأَوَّلُونَ مِنَ ٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحۡسَٰنٖ رَّضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي تَحۡتَهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Na wale waliotangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na wale waliowafuata kwa uzuri, Mwenyezi Mungu aliwaridhia, na wao walimridhia, na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Faccirooji aarabeeji:
وَمِمَّنۡ حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مُنَٰفِقُونَۖ وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ مَرَدُواْ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعۡلَمُهُمۡۖ نَحۡنُ نَعۡلَمُهُمۡۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيۡنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٖ
Na katika mabedui walio jirani zenu kuna wanafiki; na katika wakazi wa Madina pia wapo wale waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.
Faccirooji aarabeeji:
وَءَاخَرُونَ ٱعۡتَرَفُواْ بِذُنُوبِهِمۡ خَلَطُواْ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Na wengine walikiri dhambi zao, walichanganya matendo mema na mengine mabaya. Huenda Mwenyezi Mungu akakubali toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
خُذۡ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡ صَدَقَةٗ تُطَهِّرُهُمۡ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٞ لَّهُمۡۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwayo, na waombee dua. Hakika kuomba dua kwako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote
Faccirooji aarabeeji:
أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقۡبَلُ ٱلتَّوۡبَةَ عَنۡ عِبَادِهِۦ وَيَأۡخُذُ ٱلصَّدَقَٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anakubali toba ya waja wake, na anazichukua sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana?
Faccirooji aarabeeji:
وَقُلِ ٱعۡمَلُواْ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na sema: Tendeni matendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini watayaona matendo yenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; basi naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Faccirooji aarabeeji:
وَءَاخَرُونَ مُرۡجَوۡنَ لِأَمۡرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمۡ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيۡهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Na wapo wengine wanaongojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ima atawaadhibu au atawakubalia toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مَسۡجِدٗا ضِرَارٗا وَكُفۡرٗا وَتَفۡرِيقَۢا بَيۡنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَإِرۡصَادٗا لِّمَنۡ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبۡلُۚ وَلَيَحۡلِفُنَّ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّا ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya madhara, na ukafiri, na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa ajili ya wale waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: Hatukukusudia isipokuwa uzuri tu. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao hakika ni waongo.
Faccirooji aarabeeji:
لَا تَقُمۡ فِيهِ أَبَدٗاۚ لَّمَسۡجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقۡوَىٰ مِنۡ أَوَّلِ يَوۡمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِۚ فِيهِ رِجَالٞ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُطَّهِّرِينَ
Usisimame ndani yake kabisa. Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa uchamungu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo wanaume wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.
Faccirooji aarabeeji:
أَفَمَنۡ أَسَّسَ بُنۡيَٰنَهُۥ عَلَىٰ تَقۡوَىٰ مِنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٍ خَيۡرٌ أَم مَّنۡ أَسَّسَ بُنۡيَٰنَهُۥ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٖ فَٱنۡهَارَ بِهِۦ فِي نَارِ جَهَنَّمَۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Je, mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka? Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
Faccirooji aarabeeji:
لَا يَزَالُ بُنۡيَٰنُهُمُ ٱلَّذِي بَنَوۡاْ رِيبَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Na jengo lao hilo walilolijenga halitaacha kuwa shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
Faccirooji aarabeeji:
۞ إِنَّ ٱللَّهَ ٱشۡتَرَىٰ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَنفُسَهُمۡ وَأَمۡوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلۡجَنَّةَۚ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقۡتُلُونَ وَيُقۡتَلُونَۖ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ وَٱلۡقُرۡءَانِۚ وَمَنۡ أَوۡفَىٰ بِعَهۡدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِۚ فَٱسۡتَبۡشِرُواْ بِبَيۡعِكُمُ ٱلَّذِي بَايَعۡتُم بِهِۦۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Hakika Mwenyezi Mungu alinunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao wana Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki katika Taurati, na Injili, na Qur-ani. Na nani atimizaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Faccirooji aarabeeji:
ٱلتَّٰٓئِبُونَ ٱلۡعَٰبِدُونَ ٱلۡحَٰمِدُونَ ٱلسَّٰٓئِحُونَ ٱلرَّٰكِعُونَ ٱلسَّٰجِدُونَ ٱلۡأٓمِرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَٱلۡحَٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Wale wanaotubia, wanaoabudu, wanaohimidi, wanaokimbilia heri, wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu, na wanaolinda mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na wabashirie Waumini.
Faccirooji aarabeeji:
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن يَسۡتَغۡفِرُواْ لِلۡمُشۡرِكِينَ وَلَوۡ كَانُوٓاْ أُوْلِي قُرۡبَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina, hata wakiwa ni jamaa zao, baada ya kwisha wabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni.
Faccirooji aarabeeji:
وَمَا كَانَ ٱسۡتِغۡفَارُ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوۡعِدَةٖ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوّٞ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنۡهُۚ إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٞ
Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake isipokuwa kwa sababu wa ahadi aliyomuahidi. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiweka mbali naye. Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu.
Faccirooji aarabeeji:
وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوۡمَۢا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰهُمۡ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ
Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapotosha kaumu baada ya kwisha waongoa mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.
Faccirooji aarabeeji:
إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ
Hakika Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu zote na ardhi; huhuisha na hufisha. Nanyi hamna mlinzi yeyote wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu.
Faccirooji aarabeeji:
لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِيِّ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ ٱلۡعُسۡرَةِ مِنۢ بَعۡدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٖ مِّنۡهُمۡ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّهُۥ بِهِمۡ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Mwenyezi Mungu alikwisha kubali toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari waliomfuata katika saa ya ugumu, baada ya kwamba nyoyo za kundi miongoni mwa zilikuwa zimekaribia kukengeuka. Basi akakubali toba yao. Hakika Yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Na pia wale watatu walioachwa nyuma hata ardhi wakaiona kuwa ni finyu juu yao pamoja na ukunjufu wake, na nafsi zao zikawabana, na wakayakinika kuwa hakuna kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake Yeye. Kisha akawakubalia toba ili nao watubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukubali toba sana, Mwenye kurehemu.
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَكُونُواْ مَعَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.
Faccirooji aarabeeji:
مَا كَانَ لِأَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ وَمَنۡ حَوۡلَهُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ أَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرۡغَبُواْ بِأَنفُسِهِمۡ عَن نَّفۡسِهِۦۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ لَا يُصِيبُهُمۡ ظَمَأٞ وَلَا نَصَبٞ وَلَا مَخۡمَصَةٞ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوۡطِئٗا يَغِيظُ ٱلۡكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنۡ عَدُوّٖ نَّيۡلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٞ صَٰلِحٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Haiwafailii watu wa Madina na Mabedui walio kando kando yao kusalia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayo ni kwa sababu wao hakiwapati kiu, wala machovu, wala njaa, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, isipokuwa huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya uzuri.
Faccirooji aarabeeji:
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةٗ صَغِيرَةٗ وَلَا كَبِيرَةٗ وَلَا يَقۡطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمۡ لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Wala hawatoi masurufu madogo wala makubwa, wala hawalivuki bonde, isipokuwa huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Faccirooji aarabeeji:
۞ وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ
Na haiwapasi Waumini kutoka wote pamoja. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapowarudia, ili wajihadharishe?
Faccirooji aarabeeji:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَٰتِلُواْ ٱلَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ ٱلۡكُفَّارِ وَلۡيَجِدُواْ فِيكُمۡ غِلۡظَةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ
Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu miongoni mwa makafiri, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu.
Faccirooji aarabeeji:
وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Na inapokwisha teremshwa Sura, basi wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walioamini iliwazidishia Imani, nao wanafurahi.
Faccirooji aarabeeji:
وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَتۡهُمۡ رِجۡسًا إِلَىٰ رِجۡسِهِمۡ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ
Na ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi iliwazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ya kuwa wao ni makafiri.
Faccirooji aarabeeji:
أَوَلَا يَرَوۡنَ أَنَّهُمۡ يُفۡتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٖ مَّرَّةً أَوۡ مَرَّتَيۡنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Je, hawaoni ya kwamba wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.
Faccirooji aarabeeji:
وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ
Na ikishateremka Sura, hutazamana wao kwa wao, (kama kwamba wanasema:) Je, yuko yeyote anayewaona nyinyi? Kisha huondoka wakaenda. Mwenyezi akaziondoa nyoyo zao kwa kuwa hao ni kaumu wasiofahamu.
Faccirooji aarabeeji:
لَقَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولٞ مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ عَزِيزٌ عَلَيۡهِ مَا عَنِتُّمۡ حَرِيصٌ عَلَيۡكُم بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Hakika amekwisha wajia Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yale yanayowataabisha, anawajali sana, kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.
Faccirooji aarabeeji:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ
Kwa hivyo, wakigeuka, basi wewe sema, ”Mwenyezi Mungu ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi ninamtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.
Faccirooji aarabeeji:
 
Firo maanaaji Simoore: Simoo tuubabuya
Tippudi cimooje Tonngoode hello ngoo
 
Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo e ɗemngal Swahili - Ñiiɓirde Ruwwad ngam eggo. - Tippudi firooji ɗii

Firi ɗum ko fedde hentorde kanngameeji firo e ballondiral e Ceeɗɗi Da'wa e Rabwa e Ceeɗɗi Ballondiral Ndeernde Islaam e ɗemngal.

Uddude