Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Fassarar Ma'anoni Aya: (44) Sura: Suratu Fadir
أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَكَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعۡجِزَهُۥ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمٗا قَدِيرٗا
Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza.
Je! hao hukaa na wakakanya tu ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina, bila ya wao kusafiri katika ulimwengu wakaangalia kwa macho yao athari za maangamizo yaliyo wateremkia walio kuwa kabla yao kwa sababu ya kuwakadhibisha kwao Mitume? Na kabla ya wao yalikuwako mataifa yaliyo kuwa na nguvu kushinda wao. Nguvu zao hazikuweza kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye hashindwi na chochote kilioko mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye ilimu kubwa kabisa, Mwenye uweza mkubwa kabisa.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Aya: (44) Sura: Suratu Fadir
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Rufewa