Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni?
Na wengine wapo wanao kutazama na wanalifikiria jambo lako, na wanaona dalili zilizo wazi za Unabii wako. Lakini bado hawaongoki wakafuata. Mfano wa hayo ni mfano wa kipofu, nawe huwezi kuwaongoa hao vipofu. Upofu wa macho ni kama upofu wa moyo. Wote hawana uwongofu! Kipofu haioni njia kwa kuhisi, na mpotovu haongoki kwa maana.
Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao.
Hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu atawalipa watu kwa vitendo vyao kwa uadilifu na haki, wala hatamdhulumu hata mmoja wapo kwa kitu chochote. Lakini watu wanajidhulumu nafsi zao kwa kukhiari kwao ukafiri kuliko Imani.
Na Siku atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya mchana! Watatambuana. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Ewe Mtume! Wahadharishe na Siku tutayo wakusanya kwa ajili ya Hisabu, wawe na hakika kuwa Siku ya Akhera itakuja, baada ya kuwa walikuwa wakiikanusha na wakikumbuka maisha yao ya duniani tu. Waone ni kama saa moja tu ya mchana, hapana wasaa wa kufanya kitendo chochote cha kheri, na wajuane wao kwa wao wakilaumiana kwa kufuru na upotovu walio kuwa nao! Wamekhasiri wakanushao Siku ya Akhera na wasitangulize vitendo vyema katika dunia yao, na wakakosa neema za Akhera kwa kufuru zao.
Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, au tukakufisha kabla yake, marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayo yafanya.
Ewe Mtume! Tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, nayo kuwa utawashinda na wao watapata adhabu, au tukakufisha kabla ya kuyaona yote hayo, vyovyote vile hawawezi kuepuka kurejea kwetu tuwahisabie na kuwalipa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kuwachungua na Mwenye kujua kila walitendalo, naye atawalipa.
Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Na kila umma ulijiwa na Mtume akafikisha wito wa Mwenyezi Mungu, akaamini aliye amini, na akakanusha aliye kanusha. Ikifika Siku ya kufufuliwa, Mtume wao atakuja na kuwatolea ushahidi wale walio mkadhibisha kuwa hao ni makafiri, na walio amini kuwa ni Waumini. Basi Mwenyezi Mungu atawahukumu kwa uadilifu ulio timia. Hatomdhulumu yeyote katika malipo anayo stahiki.
. Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
Na makafiri wanakusudia kuikanusha Siku ya Akhera, basi wanaihimiza kwa kejeli na kusema: Itakuwa lini hiyo adhabu unayo tuahidi, kama wewe, ewe Mtume, na hao walio pamoja nawe, ni wakweli katika hayo mnayo yaamini na mnatuitia sisi tuyakubali?
Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii.
Ewe Mtume! Waambie: Mimi sina uwezo wa kujitendea mwenyewe kheri wala shari, ila kwa aliyo niwezesha Mwenyezi Mungu. Basi vipi niweze kuihimiza ije upesi hiyo adhabu? Hakika kila umma una ukomo wake aliyo uwekea Mwenyezi Mungu tangu na tangu. Ukiwadia ukomo huo basi hawatoweza kuuchelewesha hata kidogo, kama wasivyo weza kuutanguliza!
Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wakosefu?
Waambie wanao himiza ifike adhabu: Hebu niambieni, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu usiku au mchana, pana faida gani watayo ipata wakosefu wenye madhambi kutaka ije kwa haraka? Na hali adhabu yote ni mbaya!
Tena je! Ikisha tokea mtaiamini? Je! Ndio sasa tena? Na nyinyi mlikuwa mkiihimiza.
Sasa mnaikanusha adhabu? Tena itapo kufikieni mtaambiwa kwa kubeuliwa: Je! Sasa mnaamini kwa kuwa mnaiona, na nyinyi huko duniani mlikuwa mkiihimiza kwa dharau na kukanusha!
Kisha walio dhulumu wataambiwa: Onjeni adhabu ya kudumu. Kwani mtalipwa isipo kuwa yale mliyo kuwa mkiyachuma?
Tena Siku ya Kiama wataambiwa walio jidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na kukanusha: Onjeni adhabu ya milele..sasa hamlipwi ila kwa a'mali zenu mlizo zitenda duniani.
Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi!
Na makafiri, kwa njia ya kejeli na kukataa, wanakutaka wewe, Mtume, uwaambie hivyo ni kweli hayo uliyo yaleta katika Qur'ani na khabari za kufufuliwa, na adhabu? Waambie: Naam! Kwa haki ya Muumba wangu aliye niumba, hakika hayo yatakuwa bila ya shaka yoyote. Wala nyinyi hamtoshinda wala hamwezi kuzuia adhabu aitakayo Mwenyezi Mungu kukuleteeni.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
ߢߌߣߌ߲ߠߌ߲ ߞߐߝߟߌ:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".