Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - Mealler fihristi


Anlam tercümesi Ayet: (155) Sure: Sûratu'l-A'râf
وَٱخۡتَارَ مُوسَىٰ قَوۡمَهُۥ سَبۡعِينَ رَجُلٗا لِّمِيقَٰتِنَاۖ فَلَمَّآ أَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ قَالَ رَبِّ لَوۡ شِئۡتَ أَهۡلَكۡتَهُم مِّن قَبۡلُ وَإِيَّٰيَۖ أَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآۖ إِنۡ هِيَ إِلَّا فِتۡنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهۡدِي مَن تَشَآءُۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَاۖ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡغَٰفِرِينَ
Na Mūsā alichagua miongoni mwa watu wake wanaume sabiini walio bora kati yao, akatoka na wao akaenda hadi Tū,r Sīnā’ kwa wakati na muda ambao Mwenyezi Mungu Alimuagizia akutane na Yeye pamoja nao ili watubie kwa yale yaliyokuwa kwa wahuni wa Wana wa Isrāīl ya kuabudu kigombe. Walipokuja mahala hapo walisema, «Hatutakuamini, ewe Mūsā mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi, basi utakaposema na Yeye tuoneshe.» Papo hapo walishikwa na mtetemeko mkali wakafa. Akasimama Mūsā akimnyenyekea Mwenyezi Mungu na akasema, «Ewe Mola wangu, niwaambie nini Wana wa Isrāīl nikiwajia na hali wewe umewaangamiza wabora wao? Lau unataka ungaliwaangamiza wote kabla ya hali hii ya kuwa mimi niko na wao. Hilo lingalikuwa sahali zaidi kwangu. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wachache wa akili miongoni mwetu? Kitendo hiki ambacho watu wangu wamekifanya cha kuabudu kigombe, hakikuwa isipokuwa ni majaribu na mtihani, unampoteza kwayo unayemtaka miongoni mwa viumbe wako na unamuongoza kwayo unayemtaka kumuongoza. Ni wewe mtegemewa wetu na mwenye kutunusuru, tughufirie dhambi zetu na uturehemu kwa rehema zako; na wewe ndiye bora wa wenye kusamehe makosa na kusitiri dhambi.
Arapça tefsirler:
 
Anlam tercümesi Ayet: (155) Sure: Sûratu'l-A'râf
Surelerin fihristi Sayfa numarası
 
Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - Mealler fihristi

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

Kapat