Check out the new design

Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani * - Mealler fihristi

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Anlam tercümesi Sure: Sûratu'ş-Şuarâ'   Ayet:
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Watu wa Luut'i waliwakanusha Mitume.
Alipo waita Luut'i watu wake wamuabudu Mwenyezi Mungu pekee, na waache ushirikina, waliwakanusha Mitume wote.
Arapça tefsirler:
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao, Luut'i: Je! Hamumchimngu?.
Ewe Mtume! Watajie watu wako pale Lut'i alipo waambia watu wake, naye ni ndugu yao na shemeji yao:
Arapça tefsirler:
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
Hakika mimi nimetumwa kwenu na Mwenyezi Mungu nikuleteeni Dini ya Haki. Nami ni muaminifu wa kuifikisha Dini hii.
Arapça tefsirler:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.
Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na ifuateni amri yangu kwa ninayo kuitieni.
Arapça tefsirler:
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Wala mimi sitaki kwenu ujira kwa uwongofu na uwongozi ninao kuitieni. Sina ujira ila kwa Mwenye kumiliki viumbe vyote na Mlezi wao.
Arapça tefsirler:
أَتَأۡتُونَ ٱلذُّكۡرَانَ مِنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?.
Lut'i alisema: Nyinyi mnastarehea kuwaingilia wanaume mkaacha wanawake? Kwa hayo anakusudia kuyakanya yale waliyo yazoea ya vitendo vichafu. "Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?" Yaani kazi ya liwat'i, ambayo tangu asli yake ni ukosefu muovu, unao chusha hata kuusikia, kinyume na maumbile, unao mteremsha mwanaadamu chini kabisa. Na lau kuwa unaenea basi huharibu sunna ya kuoa, nayo ni sunna ya maumbile, hata uzazi ukatike na ulimwengu usite kuendelea. Na kwa liwat'i huenea maradhi kama yanavyo enea kwa uzinzi kama tego, kisonono, donda ndugu, maradhi ya ngozi kama ukurutu, na hutokea ishara za kudhoofika nyama za nyuma hata ikawa mtu hawezi kujizuia kutokwa na choo ovyo. Na nyuma kwake mtu huchanua kukawa kama mdomo wa tarumbeta. Na huko nyuma hujaa vijidudu vya maradhi na hivyo humuambukiza mwenye kumuingilia na yeye hivyo vijidudu vikenda mletea maradhi mengine ya njia za mkojo. Na huenda huyo mwenye kufanywa mambo hayo akawa mpumbavu hafai kitu, ikiwa kaanza tangu utotoni. Na huenda akajidai kuonesha ujanadume mwingi kuliko kiasi kwa kutaka kuficha upungufu wake wa uume. (Karibuni imedhihiri kuwa maradhi ya khatari kabisa ya AIDS [Ukimwi] yameenea zaidi sana kwa watendao kitendo hichi na watumiao madawa ya ulevi, ijapo kuwa na wazinzi nao hupata!). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameukemea ukosefu huu katika Aya kadhaa wa kadhaa, na akabainisha hikima ya Mwenye kuhukumu kwa kuharimisha huku, kwa kusema: " Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!"
Arapça tefsirler:
وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٌ عَادُونَ
Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!.
Na mnaacha aliyo kuumbieni Mwenyezi Mungu ya kustarehe na wake zenu walio halali yenu? Ama hakika nyinyi ni watu mlio pindukia mipaka ya udhalimu katika kufanya maasi.
Arapça tefsirler:
قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُخۡرَجِينَ
Wakasema: Ewe Luut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!.
Walikasirika kwa kule kuwakataza na kuwakemea kwa sababu ya jambo ovu na wakasema: Kama hukuacha kutukebehi tutakutoa mji kwa izara kubwa.
Arapça tefsirler:
قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلۡقَالِينَ
Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu.
Lut'i akasema: Hakika mimi nakichukia mno hichi kitendo chenu, wala sitoacha kabisa kukipinga na kukikebehi.
Arapça tefsirler:
رَبِّ نَجِّنِي وَأَهۡلِي مِمَّا يَعۡمَلُونَ
Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.
Na akamwomba Mola wake Mlezi amwokoe yeye na ahali zake na wayatendayo wale wajinga, baada ya kwisha kata tamaa kuwa hawamsikilizi.
Arapça tefsirler:
فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,.
Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake, akamwokoa yeye na wale walio fuata wito wake, kwa kuwatoa wote majumbani mwao wakati wa kuteremka adhabu kuwashukia wenye kukanusha.
Arapça tefsirler:
إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ
Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
Ila mkewe kizee aliye baki, na hakutoka nao. Yeye akaangamia kwa kufuru zake na ukhaini wake, kwa kuwaunga mkono wakosefu.
Arapça tefsirler:
ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawaangamiza wale wengine.
Kisha Mwenyezi Mungu akawahiliki makafiri watendao uovu kwa hilaki kali na mbaya.
Arapça tefsirler:
وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلۡمُنذَرِينَ
Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
Na Mwenyezi Mungu aliwateremshia wale watu wapotovu mawe kutoka mbinguni, yakawateketeza. Na ilikuwa mvua ya kutisha kwa wingi wake na namna yake. Basi mvua ovu ya walio kwisha onywa ni mvua hiyo, kwani iliteremka kwa uangamizi mkubwa mno!
Arapça tefsirler:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
Hakika adhabu ile iliyo wateremkia watu wale hapana shaka ni hoja yenye kuonyesha utimilivu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Wala si wengi katika watu wako wenye kusadiki hayo.
Arapça tefsirler:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kusifika kwa rehema iliyo kamilika. Huwapa adhabu watendao dhambi, na huwalipa wema Waumini.
Arapça tefsirler:
كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume.
Hichi kisa cha Shuaibu pamoja na Watu wa Al Aykat, Machakani, nao ni msitu wenye miti mizuri, karibu na Madian. Kikundi cha watu waliteremkia hapo na wakakaa. Mwenyezi Mungu akawapelekea Shuaibu kama alivyo wapelekea watu wa Madian. Wakamkadhibisha katika wito wake. Na kwa hivi wakawa wamekanusha risala za Mitume wote.
Arapça tefsirler:
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ شُعَيۡبٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?.
Ewe Muhammad! Watajie watu wako pale Shuaibu alipo waambia watu wa Machakani: Je! Hamumkhofu Mwenyezi Mungu mkamuamini? Wakaingia kumkadhibisha.
Arapça tefsirler:
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
Hakika mimi nimetumwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote nikuongoeni na nikuongozeni. Nami ni muaminifu wa kuufikisha ujumbe wake kwenu.
Arapça tefsirler:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
Basi tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na nit'iini kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na kuziokoa nafsi zenu na madhambi.
Arapça tefsirler:
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Na mimi kwa hivi kukuongozeni na kukufunzeni sikutakini ujira wowote. Mimi sina malipo kaamili kwa sababu ya kazi yangu ila kutokana na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Arapça tefsirler:
۞ أَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُخۡسِرِينَ
Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
Shuaibu akawaamrisha kutimiza vipimo kwa ukamilifu wanapo pima, kwani ilikuwa ada yao kupunguza kwa pishi na mizani, kupunguza haki za watu kwa kuwapunja na kuwapimia kasoro.
Arapça tefsirler:
وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِ
Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;.
Na wapimieni watu kwa mizani ya sawa sawa, ili wachukue haki yao kwa uadilifu ulio nyooka.
Arapça tefsirler:
وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi.
Wala msiwapunguzie watu haki zao, wala msipite katika nchi mkifisidi kwa kuuwa, na uharamia, na kufanya madhambi, na kufuata pumbao.
Arapça tefsirler:
 
Anlam tercümesi Sure: Sûratu'ş-Şuarâ'
Surelerin fihristi Sayfa numarası
 
Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani - Mealler fihristi

Ali Muhsin Al-Barvani Tercüme Etti.

Kapat