Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo itaraji, basi sema nao maneno laini.
Ukilazimika kujikurupusha na hao walio tajwa wenye haja, kwa sababu ya shida uliyo nayo, na ukawa hukuwapa kwa kuto kuwa nacho cha kuwapa sasa, na ilhali unataraji Mwenyezi Mungu atakufungulia baadae, basi nena nao kwa maneno mema ya kuwapa imani nawe.
Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi.
Wala usiuzuilie mkono wako kutoa katika mambo ya kheri, ukaufanya kama ulio fungwa pingu za chuma shingoni mwako ukawa huwezi kuukunjua. Wala usiukunjue wote kabisa kwa kutumia ovyo. Utakuja tukanika kwa ubakhili na majuto, au utabaki huna kitu umefilisika kwa sababu ya ubadhirifu na israfu.
Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.
Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha katika wao amtakaye. Kwani Yeye anawajua vyema tabia zao, na anaziona hali zao. Basi Yeye humpa kila mmoja wao, pindi akishika njia zake, kwa inavyo wafikiana na hikima yake Mwenyezi Mungu.
Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa.
Ikiwa yaliyo khusiana na riziki yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, basi haikufaliini kuwauwa watoto wenu kwa kukhofu ufakiri utao weza kutokea. Kwani Sisi ni Wenye kudhamini riziki zao na riziki zenu. Hakika kuwauwa hao ni dhambi kubwa.
Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.
Wala msiukaribie uzinzi, kwa kuziingilia sababu zinazo pelekea uzinzi. Jambo hilo ni jambo la aibu na uovu usio fichikana, na hapana njia mbovu kama hiyo.
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.
Wala msiuwe nafsi yoyote ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa ila kuuwa huko kukiwa kwa haki, kwa kuwa nafsi hiyo inastahiki kuuwawa kwa ajili ya kisasi au kuwa ni adhabu ya sharia. Na mwenye kuuliwa kwa kudhulumiwa Sisi tumempa jamaa yake wa karibu haki juu ya yule muuwaji, kwa kutaka kwa Qadhi auliwe kwa kisasi. Lakini naye asipite mpaka katika kuuwa, akataka kumuuwa mtu mwengine asiye kuwa muuwaji, au kwa kuwauwa wawili badala ya mmoja. Kwani Mwenyezi Mungu amemsaidia huyo kwa kumpa haki ya kisasi au kulipwa fidiya. Basi haimfalii kukiuka mipaka iliyo wekwa.
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.
Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa, ya kuiamirisha na kuikuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo mtoto afike umri wa utambuzi kuweza kuendesha mambo yake. Na akisha fika hivyo basi mkabidhini mali yake, na timizeni ahadi zote mlizo chukua. Kwani Mwenyezi Mungu atamsaili (atamuliza) aliye vunja ahadi kwa kuvunja kwake, na atamhisabia kwa hayo.
Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na khatimaye ndio bora.
Na mnapo mpimia mushtiri mpimieni vilivyo, na pimeni mizani kwa uadilifu. Kwani kuweka sawa vipimo na mizani ni bora kwenu kwa hapa duniani, kwa sababu huwaraghibisha watu kufanya nanyi biashara. Na malipo mazuri zaidi ni ya Akhera.
Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa.
Ewe mtu! Usifuate maneno wala vitendo usivyo vijua. Basi usiseme: Nimesikia...na hali hukusikia. Au: Najua...na hali hujui. Kwani masikio, macho na moyo, vyote hivyo Siku ya Kiyama vitamuuliza mtu kwa alivyo tenda kwavyo.
Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima.
Wala usitembee katika ardhi kwa kiburi na majivuno. Kwani vyovyote utavyo fanya huwezi kuipasua ardhi kwa nguvu za mkanyago wako, na kama utavyo kuwa mrefu huwezi kuipita urefu milima.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
ئىزدەش نەتىجىسى:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".