Alif Laam Raa.[1] Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimefanywa kuwa sawasawa, kisha zikapambanuliwa kwa kina, kilichotoka kwa Mwenye Hekima, Mwenye habari zote.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawastarehesha starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na atampa kila mwenye fadhila, fadhila yake. Na wakikengeuka, basi mimi hakika ninawahofia adhabu ya hiyo Siku Kubwa.
Hebu angalia! Ati wanafunika vilivyomo vifuani mwao ili wamfiche Mwenyezi Mungu! Jueni kuwa wanapojigubika nguo zao, Yeye anajua yale wanayoyaficha na yale wanayoyaweka hadharani. Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi yaliyomo vifuani.
Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote hayo yako katika Kitabu chenye kubainisha.
Na Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili awajaribu ni nani kati yenu ndiye mzuri zaidi wa matendo. Na wewe ukisema, "Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa" hakika wale waliokufuru watasema, "Haya si isipokuwa uchawi ulio wazi."
Na hata tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwishahisabiwa, wao hakika watasema, "Ni nini kinachoizuia?" Jueni! Siku itakapowajia, basi haitaondolewa kwao. Na yatawazingira yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyomgusa, hakika yeye husema, "Mabaya yamekwishaniondokea." Hakika yeye ni mwenye kufurahi, mwenye kujifahiri mno.
Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kikaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema, "Mbona hakuteremshiwa hazina, au Malaika akaja pamoja naye?" Hakika, wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa kila kitu.
Na wasipokuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur-ani) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye. Basi je, nyinyi ni Waislamu?
Basi je, yule ambaye ana ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wake Mlezi, na unaofuatwa na shahidi anayetoka kwake, na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa kilichokuwa mwongozi na rehema. Hao wanaiamini. Naye anayeikufuru katika makundi, basi Moto ndipo pahali pa miadi yake. Kwa hivyo, usiwe katika shaka juu yake. Hakika, hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, lakini wengi wa watu hawaamini.
Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo? Hao wataletwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema, "Hawa ndio waliomdanganyishia Mola wao Mlezi. Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu."
Hao hawakuwa ni wa kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu. Watazidishiwa adhabu; kwa kuwa, hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona.
Mfano wa makundi mawili haya ni kama kipofu na kiziwi, na mwenye kuona na anayesikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamkumbuki?
Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu, wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni, watu wasiokuwa na maoni. Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo."
Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walioamini. Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi, lakini mimi nawaona mnafanya ujinga.
Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu, wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao. Hapo bila ya shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu."
Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa."
Na akawa anaunda jahazi, na kila walipopita karibu nayo wakuu kutoka kwa kaumu yake, wanamkejeli. Yeye akasema, "Ikiwa nyinyi mnatukejeli, basi sisi pia tunawakejeli kama mnavyotukejeli.
Mpaka ilipokuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema, "Pakia humo katika kila kitu, jozi mbili ya dume na jike, na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwishawapitia hukumu, na watu walioamini." Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache tu.
Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe, naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri.
Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde kutokana na maji. (Nuhu) akasema: "Leo hakuna wa kulindwa kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule aliyemrehemu mwenyewe." Na wimbi likawatenganisha, basi akawa katika waliozama majini.
Na ikasemwa: "Ewe ardhi! Meza maji yako. Na Ewe mbingu! Jizuie." Basi maji yakadidimia chini, na amri hiyo ikapitishwa, na (jahazi) likasimama juu ya (mlima) wa Al-Juudiy. Na ikasemwa: Wapotelee mbali kaumu madhalimu!
Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki. Na Wewe ndiye hakimu bora zaidi ya wote wanaohukumu.
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Hakika yeye ni (wa) matendo yasiyo mema. Basi usiniombe jambo usilo na elimu nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa wajinga.
Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako kutokana na kukuomba nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehi na ukanirehemu, nitakuwa katika waliohasiri.
Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya umma miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na zitakuwapo umma tutakazozistarehesha, na kisha zitaguswa na adhabu chungu itokayo kwetu.
Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala kaumu yako, kabla ya haya. Basi subiri! Hakika Mwisho mwema ni wa wacha Mungu.
Na kwa kina 'Aadi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu isipokuwa Yeye tu. Nyinyi si chochote isipokuwa ni wazushi tu.
Na enyi kaumu yangu! Mwombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawatumia mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika kwa wingi, na atawazidishia nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wahalifu."
Sisi tunasema: 'Baadhi ya miungu yetu imekusibu kwa baa.' Akasema, "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika.
Na wakikengeuka, "Basi hakika mimi nimekwishawafikishia yale niliyotumwa nayo kwenu. Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu."
Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika waliangamizwa kina 'Aadi, kaumu ya Hud.
Na kina Thamud tuliwatumia ndugu yao Saleh. Akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika ardhi, na akawaweka humo imara. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.
Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa heri kwetu. Je, unatukataza kuwaabudu wale ambao baba zetu walikuwa wakiwaabudu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayotuitia.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mnaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, naye akawa amenipa rehema kutoka kwake, je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu.
Na enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu awe Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimguse kwa ubaya, ikaja kuwaangamiza adhabu iliyo karibu.
Basi ilipokuja amri yetu, tulimwokoa sawasawa Saleh na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu.
Na hakika wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Kisha hakukaa isipokuwa mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma.
Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa, Mtukufu.
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda mabaya. Yeye akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo je, hakuna hata mwanamume mmoja miongoni mwenu aliyeongoka?
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Basi wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma, isipokuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakaowafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu sana?
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shu'aib. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yoyote isipokuwa Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi ninawaona mko katika hali njema, nami ninawahofia adhabu ya siku kubwa hiyo itakayowazingira.
Wakasema: Ewe Shu'aibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno!
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mnaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sitaki kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza. Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye ninarudi.
Na enyi kaumu yangu! Kuhalifiana nami kusiwapelekee hata mkasibiwa na mfano wa yale waliyosibiwa kaumu ya Nuhu, au kaumu ya Hud, au kaumu ya Saleh. Na kaumu ya Lut si mbali nanyi.
Wakasema: Ewe Shu'aibu! Mengi katika hayo unayoyasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona dhaifu miongoni mwetu. Na lau kuwa si jamaa zako, tungekupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu.
Akasema: Enyi kaumu yangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazingira yote mnayoyatenda.
Na enyi kaumu yangu! Fanyieni katika mahali penu, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na ni nani mwongo. Na ngojeni, hakika mimi pia ninangoja pamoja nanyi.
Na amri yetu ilipokuja, tulimwokoa sawasawa Shu'aibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na ukelele uliwanyakua wale waliodhulumu, na wakaishia wamekufa kifudifudi katika majumba yao!
Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu.
Na ama wale waliofurahishwa, wao watakuwa katika Bustani wadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na kikomo.
Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyoabudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimizia fungu lao bila ya kulipunguza.
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini kukazuka kuhitilafiana ndani yake. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayowahangaisha.
Na dumisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mazuri huondoa mabaya. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.
Basi mbona hawakuwepo katika vizazi vya kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanaokataza uharibifu katika nchi, isipokuwa wachache tu, miongoni mwa wale tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu walifuata yale waliyostareheshwa kwayo, na walikuwa wahalifu.
Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu. Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba. Na lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja.
Na yote tunayokusimulia katika habari za Mitume yale tunayoimarisha kwayo moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.
Na ni ya Mwenyezi Mungu tu ghaibu ya mbinguni na ardhi, na mambo yote yatarejeshwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee. Na Mola wako Mlezi haghafiliki mbali na yale mnayoyatenda.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
የፍለጋ ዉጤቶች:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".