next

سورة الذاريات - Adh-Dhariyat

prev

1 : 51

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaapa kwa upepo wenye kurusha mchanga. info
التفاسير: |

2 : 51

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا

Na mawingu yenye kubeba uzito mkubwa wa maji. info
التفاسير: |

3 : 51

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا

Na jahazi zinazopita baharini na kutembea kwa wepesi na usahali. info
التفاسير: |

4 : 51

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا

Na Malaika wenye kugawanya vitu kwa viumbe kutoka kwa Allah Mtukufu kama mvua na rizki na kadhalika. info
التفاسير: |

5 : 51

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ

Kwamba mnayoahidiwa, (enyi watu), ya kufufuliwa na kuhesabiwa ni ya kweli na uhakika. info
التفاسير: |

6 : 51

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ

Na kwamba kuhesabiwa na kulipwa mema kwa amali njema ni jambo lenye kutokea. info
التفاسير: |
next

سورة الذاريات - Adh-Dhariyat

prev
:
0:00 0:00