ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - فهرس التراجم


ترجمة معاني آية: (157) سورة: الأعراف
ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلرَّسُولَ ٱلنَّبِيَّ ٱلۡأُمِّيَّ ٱلَّذِي يَجِدُونَهُۥ مَكۡتُوبًا عِندَهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ يَأۡمُرُهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَىٰهُمۡ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡخَبَٰٓئِثَ وَيَضَعُ عَنۡهُمۡ إِصۡرَهُمۡ وَٱلۡأَغۡلَٰلَ ٱلَّتِي كَانَتۡ عَلَيۡهِمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِهِۦ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَٱتَّبَعُواْ ٱلنُّورَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ مَعَهُۥٓ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Rehema hii nitawaandikia wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mambo ya kumuasi, na wanaomfuata Mtume aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yaandikwa huko kwao katika Taurati na Injili; anawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni lema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishla vichafu vya hivyo kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo aliviharamisha Mwenyezi Mungu, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, na wakaukubali unabii wake, wakamheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur’ani aliyoteremshiwa, wakaufuata mwendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi waja wake Waumini.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (157) سورة: الأعراف
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

إغلاق