ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - فهرس التراجم


ترجمة معاني آية: (160) سورة: الأعراف
وَقَطَّعۡنَٰهُمُ ٱثۡنَتَيۡ عَشۡرَةَ أَسۡبَاطًا أُمَمٗاۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ إِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰهُ قَوۡمُهُۥٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنۢبَجَسَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۚ وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡغَمَٰمَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Na tuliwagawa watu wa Mūsā miongoni mwa Wana wa Isrāīl makabila kumi na mbili, kwa idadi ya Asbāṭ- wana wa Ya’qūb-, kila kabila ikajulikana kupitia kiongozi wake. Na tulimpelekea wahyi Mūsā, walipotaka watu wake kwake maji ya kunywa waliposhikwa na kiu katika kuzunguka kwao, tukamwambia, «Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.» Akalipiga na pakabubujika chemchemi za maji sehemu kumi na mbili, na watu wa kila kabila, miongoni mwa yale makabila kumi na mbili, walijua mahali pao pa kunywa, hakuna kabila litakaloingia sehemu ya kunywa ya kabila lingine. Na tukawafinika kiwingu juu yenu, na tukawateremshia mann- kitu kinachofanana na gundi chenye ladha kama ya asali- na salwā- ndege wanaofanana na wale wanaoitwa sumānā (tomboro), na tukawaambia, «Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku.» Walivichukia na kuvichoka hivyo kwa muda mrefu wa kuvitumia na wakasema, «Hatutavumilia juu ya chakula kimoja.» Na wakataka kubadilishiwa kizuri walichonacho kwa ambacho ni kiovu. Na wao hawakutudhulumu sisi walipoacha kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuacha kusimama na yale Aliyoyalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao, kwa kuwa walizikosesha kila jema na kuzipeleka kwenye shari na mateso.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (160) سورة: الأعراف
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

إغلاق