Alif Lam Mim, ni harufi zilizo undiwa Qur'ani, kama yalivyo undiwa maneno yenu. Ikiwa mmeshindwa kuleta mfano wake hii, basi ni ushahidi kuwa hii inatokana na Mwenyezi Mungu, wala hakuisema mwanaadamu.
Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinacho toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Huu ni uteremsho wa Qur'ani umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yao. Hapana shaka yoyote kuwa hii imeteremka kutoka kwake.
Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyo toka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasio fikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.
Ati wanasema: Kaizua Muhammad, naye akamsingizia Mwenyezi Mungu! Haiwafalii wao kusema hayo. Kwani hii ni Haki, Kweli, iliyo teremka kutokana na Mola wako Mlezi, ili upate kuwakhofisha kwayo watu ambao hawajapata kujiwa na Mtume kabla yako, utaraji kwa onyo hili wapate kuongoka na waifuate Haki.
Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?
Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi, A'rshi, kwa utawala ulio laiki naye. Nyinyi hamna badala yake Yeye yeyote msaidizi wa kukunusuruni, wala mwombezi wa kukuombeeni. Basi je, mtaendelea kushikilia kuwa katika ukafiri na inda, wala msiwaidhike kwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu?
Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi.
Yeye huyaendesha mambo ya uumbaji katika mbingu na ardhi, kisha amri yake hupanda kwenda kwake kwa siku ambayo kadiri yake ni kama miaka elfu kwa mujibu wa miaka ya duniani mnayo ihisabu nyinyi.
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
Huyo ndiye aliye sifika kwa kuumba na kutawala na kupanga, Mwenye kuyajua ya ghaibu ya viumbe vyote na wanayo yaona, ambaye amri yake ni yenye kushinda, Mkunjufu wa rehema,
Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.
Kisha akawafanya dhuriya zake wa namna mbali mbali kutokana na maji machache, dhaifu, yasiyo tamanika kwa kawaida. Katika Aya hii tukufu "utokane na kizazi cha maji dhaifu". Neno la Kiarabu lilio tumiwa ni "Mahiin". Neno hili likitumiwa kwa mtu lina maana ya "dhaif", mnyonge, na pia lina maana ya "chache". Basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Min maain mahiin" maana yake ni "kutokana na maji machache dhaifu" , ndiyo ya kudharauliwa. Mfano wa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Au mimi si bora kuliko huyu aliye (mahiin) mnyonge wala hawezi kusema waziwazi?" (Azzukhruf: 43.52). Na neno "Mahana al-ibila" maana yake "Kamkama maziwa ngamia". Kwa hivyo basi hapana ubaya kulifasiri neno hili Mahiin katika Aya hii kwa maana ya maji yanayo toka kwa kuchupa, au kumiminika, (kama yanavyo toka maziwa kwenye chuchu) au machache.
Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
Kisha akamsimamisha na kumkuza, na akamtia ndani yake siri yake aliyo mkhusisha nayo, na akakupeni masikio, na macho, na akili, mpate kusikia na kuona na kufahamu. Nanyi hamshukuru ila kwa uchache.
Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.
Na wanao kanya kufufuliwa wakasema: Ati sisi tukisha kuwa mchanga, ulio changanyika na mchanga wa ardhi, usibagulike, ndio kweli tutarejea kwa umbo jipya? Hao hakika si kama wanakanya kufufuliwa tu, bali wanakadhibisha yote yatayo kuwako Akhera.
Na ungeli waona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi, (wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumesha ona, na tumesha sikia. Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa.
Lau kuwa umejaaliwa kuwaona wakosefu kwenye msimamo wa hisabu ungeli ona ajabu. Pale wale wakosefu wenye kujivuna watavyo inamisha vichwa vyao kwa hizaya inayo tokana na Mola wao Mlezi, nao watasema kwa unyonge: Ewe Mola wetu Mlezi! Tumekwisha yaona tuliyo kuwa na upofu nayo, na tumekwisha yasikia tuliyo kuwa na uziwi nayo, basi turejeshe duniani tupate tenda mema ambayo tuliyo kuwa hatuyatendi. Hakika sasa hivi sisi tumeyakinika na walio kuja nayo Mitume wako.
Na lau tungeli taka tunge mpa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyo toka kwangu : Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu.
Na lau kuwa tunataka tungeli mpa kila mtu uwongofu wake, lakini kauli yangu ilikwisha tangulia, nayo ni: Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa majini na watu. Kwa kuwa tulijua kuwa wengi wao watakhiari upotovu.
Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Basi ionjeni adhabu kwa vile mlivyo ghafilika na kukutana nami hii leo. Hakika Sisi tunakuacheni katika adhabu kama watu walio sahauliwa. Na onjeni adhabu ya milele isiyo katika, kwa sababu ya ukafiri wenu na uasi wenu.
Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni.
Hakika wanazisadiki Ishara zetu wale ambao wanapo waidhiwa kwazo huanguka chini kwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, na wakamtakasa Mola wao Mlezi na kila upungufu, na wakamsifu kwa kila ukamilifu. Na wala wao hawatakabari wakakataa kuzifuata Ishara hizi.
Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku.
Mbavu zao zinabambatuka na vitanda vyao, yaani wanaacha usingizi wao, kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa kuikhofu ghadhabu yake, na kutumai rehema yake; na ambao kutokana na mali tuliyo wapa wanatoa kwa ajili ya mambo ya kheri.
Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda.
Na hapana mtu yeyote anaye jua kiasi cha Mwenyezi Mungu alicho muandalia na akawafichia katika neema kubwa kubwa, na ambazo ni za kupoza macho yao, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wanayachuma ya ut'iifu na vitendo.
Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa.
Kwani watu watakuwa sawa katika malipo yao, na hali wamekhitalifiana katika vitendo vyao? Je! Aliye kuwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni kama mwenye kumkataa na akamuasi? Hasha! Hawawi sawa!
Na ama wale walio tenda uovu, basi makaazi yao ni Motoni. Kila wakitaka kutoka humo watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mliyo kuwa mkiikanusha.
Ama wale walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu kwa kufuru zao, makaazi yao aliyo watayarishia ni Motoni. Kila wakijaribu kutoka watarudishwa huko huko. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlipo kuwa duniani mkishikilia kuikadhibisha.
Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.
Na tunaapa: Hapana shaka tutawaonjesha duniani adhabu duni kabla hawajaifikia hiyo adhabu kubwa kabisa, nayo ni kudumu milele katika Moto. Huenda pengine watakao adhibiwa kwa hiyo adhabu duni watatubia, waache ukafiri wao.
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.
Na hapana mtu yeyote aliye zidi udhaalimu kuidhulumu Haki na kuidhulumu nafsi yake, kuliko mtu anaye kumbushwa kwa Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zilizo wazi, kisha akaacha kuziamini juu ya kuwa ni wazi dhaahiri. Hakika Sisi tutajilipizia juu ya kila mkosefu!
Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
Na Sisi tulikwisha mpa Musa Taurati. Basi usiwe na shaka na kupokea kwa Musa Kitabu hicho. Na tumekijaalia Kitabu alicho teremshiwa Musa kiwe ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.
Na kutokana na Wana wa Israili tumejaalia wawepo Maimamu, waongozi, wa Dini, wasimame kuwaongoa watu, kwa kuitikia amri yetu kwa vile walivyo vumilia kuyatenda yaliomo katika Taurati, na wakawa wanazisadiki Ishara zetu ukomo wa kusadiki.
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii?
Je! Kwani Mwenyezi Mungu aliwaacha walio wakadhibisha Mitume wao, na hakuwabainishia kwamba Yeye aliwahilikisha wengi katika kaumu zilizo watangulia, na wao wanapita kwenye majumba yao, na wanatembea kwenye maskani zao? Hakika katika hayo pana mawaidha ya kuwaonyesha Haki. Wao wameingiwa na uziwi, hawasikii mawaidha haya.
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni?
Wameingia upofu, na wala hawaoni ya kwamba hakika Sisi tunapeleka mvua na mito kwenye ardhi za ukame ambazo hazimei mimea, na tukaziotesha mazao yake, wakala wanyama wao, na wao wenyewe wakala nafaka zake na matunda yake? Wamepofuka, na kwa hivyo hawazioni dalili za Mwenyezi Mungu za kuwafufua wafu.
Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli?
Na washirikina wanakwambia wewe na Waumini: Wakati gani Mwenyezi Mungu atakufungulieni mpate ushindi? Twambieni wakati wake ikiwa nyinyi ni wasema kweli.
Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.
Waambie: Siku ya hukumu na kufafanua ikikufikilieni, walio kufuru haitowafaa kitu imani yao, wala hawatapewa muhula hata chembe ya hiyo adhabu wanayo istahiki.
Na ikiwa kufanya maskhara kama hivi ndio mtindo wao, basi wapuuzilie mbali. Na wewe ngojea ukweli aliyo kuahidi Mola wako Mlezi juu yao, kwani wao wanakungojea ushindwe.
4. إبقاء معلومات نسخة الترجمة الموجودة داخل المستند.
5. إفادة المصدر (QuranEnc.com) بأي ملاحظة على الترجمة.
6. تطوير الترجمات وفق النسخ الجديدة الصادرة من المصدر (QuranEnc.com).
7. عدم تضمين إعلانات لا تليق بترجمات معاني القرآن الكريم عند العرض.
نتائج البحث:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".