Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni. Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka.
Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa ya kuyahifadhi na kuyakuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo yatima afike umri wa uwongofu, atapo weza mwenyewe kuendesha mambo yake baraabara. Hapo tena ndio mpeni mali yake. Wala msipunje vipimo na mizani kwa kupunguza mnapo toa, au kuongeza mnapo chukua. Bali pimeni kwa uadilifu kama muwezavyo. Na Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi ila kwa kadiri iwezavyo bila ya karaha. Na mkisema neno katika kuhukumu, au ushahidi, au khabari, au mfano wa hayo, basi msikengeuke mkaacha uadilifu na ukweli. Bali hakikisheni kusema sawa, bila ya kuzingatia makhusiano ya jinsi, yaani uke na ume, au rangi, au ujamaa au ushemeji. Wala msitengue ahadi za Mwenyezi Mungu alizo chukua kwenu kwa taklifu, wala ahadi zilio baina yenu wenyewe kwa wenyewe, katika mambo yaliyo fungamana na maslaha yaliyo ruhusiwa kisharia. Bali timizeni ahadi hizi zote. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa kutilia mkazo mjitenge na yaliyo katazwa, na mkumbuke kuwa Sharia ni kwa ajili ya maslaha yenu.
Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.
Wala msiiache Njia niliyo kuwekeeni, kwani hiyo ndiyo Njia Iliyo Nyooka itayo kufikisheni kwenye mafanikio ya duniani na Akhera. Bali ifuateni Njia hii, wala msifuate njia nyingine za upotovu alizo kukatazeni Mwenyezi Mungu, ili msije kufarikiana mkawa makundi makundi na mapande mapande, ya madhehebu na vyama, na mkawa mbali na Njia ya Mwenyezi Mungu iliyo kaa sawa. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa amri ya nguvu ili msije mkamkhalifu Yeye.
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi.
Na tulimteremshia Musa Taurati kwa kumtimizia neema mtu aliye simama msimamo mwema katika mambo ya Dini. Na tuliiteremsha kwa kueleza wazi kila jambo katika mafunzo yalio nasibiana na watu wake, na ni uwongofu kwendea Njia iliyo sawa, na rehema kwao kwa kuifuata. Na hayo ni hivyo ili Wana wa Israili waiamini Siku ya kukutana na Mola wao Mlezi, Siku ya Kiyama na kuhisabiwa kwa mambo walio amrishwa kuyafanya.
Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili mrehemewe.
Na hii Qur'ani ni Kitabu, kilicho barikiwa, tulicho kiteremsha, chenye kukusanya kheri za Mwenyezi Mungu, na manufaa ya Dini na dunia. Basi kifuateni, na ogopeni msende kinyume chake, ili Mola wenu Mlezi apate kukurehemuni.
Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma.
Tumeiteremsha hii Qur'ani ili msipate kutoa udhuru kwa uasi wenu mkasema: Wahyi haukuteremka ila kwa mataifa mawili tu ya kabla yetu, nao ni watu wa Taurati na watu wa Injili. Na sisi hatuna ilimu kabisa ya kusoma vitabu vyao na kufahamu uwongozi uliomo humo.
Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Na Sisi tumeiteremsha Qur'ani ili wasiseme pia: Lau kuwa sisi tumeteremshiwa ufunuo kama walivyo teremshiwa wao, tungeli washinda kwa uwongofu, na hali yetu ingeli kuwa bora zaidi, kwa sababu ya akili zetu ni pana zaidi na sisi tumetengenea vizuri! Baada ya hii leo hamna hoja ya kuasi kwenu. Wala hapana udhuru wa kauli yenu hii. Kwani Qur'ani imekujieni kutoka kwa Mola Mlezi wenu, nayo ni alama iliyo wazi ya ukweli wa Muhammad. Inabainisha yote mnayo yahitajia katika Dini yenu na dunia yenu. Inakuongoeni kwenye Njia iliyo sawa, na rehema kwenu kuifuata. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko huyo anaye zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu alizo ziteremsha katika Vitabu vyake, na Ishara zake alizo ziumba katika ulimwengu, naye akazipuuza na asiziamini, na wala asizitende! Na Sisi tutawaadhibu hao wanao zikataa Ishara zetu, wala hawazingatii adhabu yenye mwisho wa uchungu, kwa sababu ya kukataa kwao na kuacha kuzingatia kwao.
4. إبقاء معلومات نسخة الترجمة الموجودة داخل المستند.
5. إفادة المصدر (QuranEnc.com) بأي ملاحظة على الترجمة.
6. تطوير الترجمات وفق النسخ الجديدة الصادرة من المصدر (QuranEnc.com).
7. عدم تضمين إعلانات لا تليق بترجمات معاني القرآن الكريم عند العرض.
نتائج البحث:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".