ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (38) سورة: الأنعام
وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَٰٓئِرٖ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِي ٱلۡكِتَٰبِ مِن شَيۡءٖۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يُحۡشَرُونَ
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.
Na dalili yenye nguvu kabisa ya uwezo wa Mwenyezi Mungu na hikima yake, na rehema yake, ni kuwa Yeye kaumba kila kitu, na wala hapana juu ya ardhi mnyama anaye tambaa juu yake au chini yake, wala ndege arukaye kwa mbawa zake katika anga, ila Mwenyezi Mungu amewaumba kuwa ni jamii za umati kama mlivyo nyinyi. Na amewajaalia wawe na sifa zao, na vitambulisho vyao, na mipango yao ya maisha yao. Hatukukiacha kitu katika Kitabu kilicho andikwa kilioko kwetu ila tumekithibitisha. Na ikiwa wanakanusha, basi watafufuliwa pamoja na kaumu zote kwa ajili ya hisabu Siku ya Kiyama.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (38) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق