ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (93) سورة: الأنعام
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمۡ يُوحَ إِلَيۡهِ شَيۡءٞ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثۡلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ فِي غَمَرَٰتِ ٱلۡمَوۡتِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓاْ أَيۡدِيهِمۡ أَخۡرِجُوٓاْ أَنفُسَكُمُۖ ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَوۡنَ عَذَابَ ٱلۡهُونِ بِمَا كُنتُمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَكُنتُمۡ عَنۡ ءَايَٰتِهِۦ تَسۡتَكۡبِرُونَ
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
Nabii huyu hakusema uwongo alipo tangaza kuwa Qur'ani imetoka kwaMwenyezi Mungu. Na hapana mwenye kumshinda kwa udhaalimu huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au akasema: Nimepata wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuwa kapata wahyi wowote ule. Vile vile hapana dhaalimu mkubwa zaidi kuliko anaye sema: Mimi nitaleta maneno sawa na hayo aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa unaijua hali ya hao madhaalimu nao wamo katika shida za mauti, na Malaika wanazing'oa roho zao kutokana na miili yao, kwa ukali na nguvu, ungeli ona vitisho vya kushitua vinawashukia! Wakati huo hao huambiwa: Sasa malipo yenu ya adhabu ya kudhalilisha na kufedhehesha yanaanza. Malipo haya ni kwa vile mlivyo kuwa mkimzulia Mwenyezi Mungu bila ya haki, na ni malipo kwa kuwa kiburi chenu kilikuzuieni msiangalie na kuzipima Aya, Ishara, za uumbaji za Mwenyezi Mungu ziliomo katika Qur'ani.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (93) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق