ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (95) سورة: الأنعام
۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰۖ يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَمُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتِ مِنَ ٱلۡحَيِّۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa?
Hakika dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu kufufua, na kuwa ni Yeye pekee anaye stahiki kuabudiwa, na kufufua kwake watu kutoka makaburini, zimeenea na zimo za namna mbali mbali. Kwani ni Yeye peke yake ndiye anaye ipasua mbegu ukachipua mmea, na ni Yeye ndiye anaye ipasua kokwa ukatokeza mti. Na hivyo humfufua aliye hai kutokana na kisicho kuwa hai, kama mtu kutokana na udongo. Na akatoa kisicho kuwa hai kutokana na kilicho hai, kama maziwa kutokana na mnyama. Huyo Muweza Mtukufu ndiye Mungu wa Haki. Basi kisiwepo kitu cha kukugeuzeni mkaacha kumuabudu Yeye mkaviabudu vyenginevyo. Imeunganishwa Aya hii ya kupasua mbegu na kokwa, na Aya ya kupambazua asubuhi ambayo inaashiria kuwepo mwangaza, na kiza, na ya kwamba mwangaza umeshikamana kwa nguvu na kukua kwa mimea na miti. Hayo ni kwa kuwa mbegu na kokwa baada ya kuchipua zinahitajia chakula. Na chakula hichi kinatokana na mbolea maalumu kutokana na ardhi, na pia kutokana na mwangaza wa jua. Kwa hivyo mizizi yao inakwenda chini kutafuta chakula cha ardhi, na vigogo vyake na matawi inapata chakula kutokana na mwako wa jua ambalo ndilo linachomoza asubuhi.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (95) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق