ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: الصف   آية:

سورة الصف - Surat As-Saff

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Kila kiliomo katika mbingu na kiliomo katika ardhi kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa ni laiki yake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kuvishinda vitu vyote, Mwenye hikima iliyo fika ukomo.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفۡعَلُونَ
Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema msiyo yatenda?
Enyi mlio amini! Kwa ajili ya nini mnasema kwa ndimi zenu yasiyo hakikishwa na vitendo vyenu?
التفاسير العربية:
كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُواْ مَا لَا تَفۡعَلُونَ
Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.
Mwenyezi Mungu anachukia mno kuwa nyinyi mnasema msiyo yatenda.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِهِۦ صَفّٗا كَأَنَّهُم بُنۡيَٰنٞ مَّرۡصُوصٞ
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana.
Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigania kutaka kulinyanyua Neno lake nao wameshikamana kitu kimoja, kama kwamba wao ni jengo lilio simama imara.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ لِمَ تُؤۡذُونَنِي وَقَد تَّعۡلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡۖ فَلَمَّا زَاغُوٓاْ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliye tumwa kwenu? Walipo potoka, Mwenyezi Mungu aliziachia nyoyo zao zipotoke. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.
Ewe Muhammad! Kumbuka pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi mimi, na hali nyinyi mnajua kwamba hakika mimi ni Mjumbe niliye tumwa na Mwenyezi Mungu nije kwenu? Walipo endelea na kuiacha Haki, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao zisipokee uwongofu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio toka kwenye ut'iifu wake.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!
Na kumbuka pale Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume nimetumwa kwenu, mwenye kusadikisha yaliyo nitangulia yaliomo katika Taurati, na kukupeni bishara ya Mtume atakaye kuja baada yangu. Jina lake ni Ahmad. Alipo kuja huyo Mtume aliye bashiriwa kwa Ishara zilizo wazi wakasema: Haya uliyo tujia nayo ni uchawi dhaahiri! (Kwa ushahidi wa kubashiriwa Nabii Muhammad s.a.w. katika vitabu vya Kikristo na Kiyahudi, tazama: Kumbukumbu la Torati 18.19-22, na Injili ya Yohana 16.5-14.)
التفاسير العربية:
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Na nani aliye zidi kwa udhaalimu kuliko huyo aliye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, naye anaitwa aingie katika Dini ya Kiislamu, Dini ya haki na kheri? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio shikilia dhulma.
التفاسير العربية:
يُرِيدُونَ لِيُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.
Wana wa Israili wanamzulia Mwenyezi Mungu uwongo, ili ati wapate kuizima nuru ya Dini yake kwa vinywa vyao, kama anaye taka kuizima nuru ya jua kwa kuipulizia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuikamilisha nuru yake kwa kuitimiza Dini yake hata hao makafiri wakiudhika.
التفاسير العربية:
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ
Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.
Mwenyezi Mungu ndiye aliye mtuma Mtume wake, Muhammad, pamoja na Qur'ani ambayo ni uwongofu kwa watu wote, na Uislamu ambao ndio Dini ya haki, ili autukuze juu ya dini zote, ijapo kuwa washirikina wataudhika.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَٰرَةٖ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ
Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu?
Enyi mlio amini! Nikuongozeni kwenye biashara kubwa ambayo itakuokoeni na adhabu yenye machungu makali?
التفاسير العربية:
تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Biashara hii ni kuwa mumuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na mpigane Jihadi katika Njia ya MwenyeziMungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Hayo aliyo kuonyesheni ndiyo kheri yenu ikiwa nyinyi mnajua.
التفاسير العربية:
يَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ وَيُدۡخِلۡكُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّٰتِ عَدۡنٖۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.
Muamini na mpigane Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ili akusameheni madhambi yenu, na akutieni katika Bustani zinazo pita kati yake mito, na maskani nzuri katika Bustani za milele. Hayo ndiyo malipo makubwa.
التفاسير العربية:
وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!
Na neema nyengine ambazo Waumini Mujahidina wanazo zipenda, ni msaada utokao kwa Mwenyezi Mungu na ushindi wa karibu utakao kuleteeni kheri zake. Na ewe Muhammad! Wabashirie Waumini kuwa watapata malipo haya.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُوٓاْ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوَارِيِّـۧنَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٞ مِّنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٞۖ فَأَيَّدۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَىٰ عَدُوِّهِمۡ فَأَصۡبَحُواْ ظَٰهِرِينَ
Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru. Basi tukawaunga mkono walio amini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.
Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu anapo kutakeni Mtume wa Mwenyezi Mungu muwe wasaidizi wake. Kama walivyo kuwa masahaba wa Isa wasaidizi wa Mwenyezi Mungu alipo sema: Nani wa kunisaidia mimi kwa Mwenyezi Mungu? Basi kundi moja katika Wana wa Israili lilimuamini Isa, na kundi jengine likamkataa. Sisi tukawapa nguvu walio amini juu ya maadui zao walio kufuru. Basi kwa kuwapa nguvu kwetu wakawa ni wenye kushinda.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: الصف
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق