ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: التغابن   آية:

سورة التغابن - Surat At-Taghabun

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
Vitu vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa laiki na utukufu wake. Yeye ndiye peke yake Mwenye ufalme ulio timia, na Mwenye sifa njema, na ndiye Mwenye uweza ulio timia juu ya kila kitu.
التفاسير العربية:
هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ فَمِنكُمۡ كَافِرٞ وَمِنكُم مُّؤۡمِنٞۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ
Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
Yeye peke yake ndiye aliye kuumbeni mlipo kuwa si chochote. Basi kati yenu yupo anaye kanya Ungu wake, na miongoni mwenu yupo anaye sadiki. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda, na atakulipeni kwa mujibu wa vitendo vyenu.
التفاسير العربية:
خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ
Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake.
Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa hikima isiyo na ukomo, na akakuumbeni kwa sura, na akazifanya nzuri sura zenu, kwa kuwa amewafanya wanaadamu ndio viumbe walio nyooka vizuri. Na kwake Yeye ndiyo marejeo Siku ya Kiyama.
التفاسير العربية:
يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Anajua viliomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliomo vifuani.
Yeye Mwenyezi Mungu anajua yote yaliomo katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha, na mnayo yaeneza, ikiwa maneno au vitendo. Na Mwenyezi Mungu ametimia ujuzi wake kwa mnayo dhamiria katika nyoyo zenu.
التفاسير العربية:
أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُ فَذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Kwani haikukujieni khabari ya walio kufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.
Zimekwisha wafikieni khabari za walio kufuru kabla yenu, na wao wakameza ubaya wa matokeo wa mambo yao katika dunia. Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.
التفاسير العربية:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُۥ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٞ يَهۡدُونَنَا فَكَفَرُواْ وَتَوَلَّواْۖ وَّٱسۡتَغۡنَى ٱللَّهُۚ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَمِيدٞ
Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo binaadamu ndio atuongoe? Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, naye ni Msifiwa.
Masaibu hayo yaliyo wapata ni kwa sababu Mitume wao waliwajia na miujiza iliyo dhaahiri, nao wakasema kwa kukanya: Ati atujie mtu kama sisi kutuongoza? Wakakanya kuwa watafufuliwa. Wakaiacha Haki. Mwenyezi Mungu akadhihirisha kuwa hana haja na imani yao kwa kuwaangamiza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ukwasi wake (kujitosha kwake), si Mwenye kuwa na haja na viumbe vyake. Ni Mwenye kustahiki kusifiwa na kuhimidiwa kwa uzuri wa neema zake.
التفاسير العربية:
زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن لَّن يُبۡعَثُواْۚ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبۡعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلۡتُمۡۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ
Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
Makafiri wamedai kwa uwongo kwamba hawatafufuliwa baada ya kufa kwao. Ewe Muhammad! Waambie: Mambo sio kama mnavyo dai nyinyi. Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka yoyote nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa kwenu, na hapana shaka yoyote kuwa mtaambiwa mliyo yatenda duniani. Kisha mtalipwa kwayo. Na huko kufufuliwa, na kuhisabiwa, na kulipwa, ni jambo sahali na jepesi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.
التفاسير العربية:
فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyo iteremsha. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Basi msadikini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ongokeni kwa kuifuata Nuru tuliyo mteremshia hata akakufahamisheni kwa uwazi kuwa kufufuliwa kunakuja bila ya shaka yoyote. Na Mwenyezi Mungu ana ujuzi wa kutumia kwa yote yanayo tokana nanyi.
التفاسير العربية:
يَوۡمَ يَجۡمَعُكُمۡ لِيَوۡمِ ٱلۡجَمۡعِۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلتَّغَابُنِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Siku atakayo kukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko; hiyo ni siku ya kupunjana. Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Mabustani yenye kupitiwa kati yake na mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Siku atapo kukusanyeni katika Siku ya Mkusanyo wa walio tangulia mwanzo na walio kuja mwisho, akulipeni kwa vitendo vyenu! Siku hiyo ndiyo Siku ya Taghaabun, Kupunjana, kutapo dhihiri kupunjika kwa makafiri kwa kuacha Imani, na kupunjika Waumini kwa kupuuza kuongeza ut'iifu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema atamwondolea maovu yake, na atamtia katika Bustani zenye kupita kati yake mito, wakae humo milele. Malipo hayo ndio kufuzu kukubwa.
التفاسير العربية:
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Na walio kufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marudio mabaya.
Na walio ikataa Imani, na wakaikanusha miujiza yetu tuliyo wapa Mitume wetu kuwaunga mkono, hao ndio watu wa Motoni. Watadumu humo. Na marudio maovu ni hayo walio yarudia hao.
التفاسير العربية:
مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Mja hasibiwi na balaa ila kwa kudra ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumsadiki Mwenyezi Mungu basi humwongoa moyo wake kwendea katika yanayo mpendeza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.
التفاسير العربية:
وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu.
Na mt'iini Mwenyezi Mungu kwa aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa Ujumbe aliyo kufikishieni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Mkiupuuza ut'iifu huu, basi Yeye hadhuriki kitu kwa mapuuza yenu. Na hakika Mtume wetu hana jukumu juu yake ila kufikisha Utume wake tu kwa uwazi.
التفاسير العربية:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu nawategemee Waumini.
Mwenyezi Mungu, hapana wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye tu peke yake. Basi Waumini nawamtegemee Yeye tu katika mambo yao yote.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ وَأَوۡلَٰدِكُمۡ عَدُوّٗا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُواْ وَتَصۡفَحُواْ وَتَغۡفِرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ
Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu, ambao wanakuzuilieni msimt'ii Mwenyezi Mungu kwa kutaka kuwatimizia hao matakwa yao. Basi kuweni na hadhari nao. Na mkiweza kuyavuka makosa yao yanayo kubalika kusameheka, na mkayapuuza, na mkawafichia, basi Mwenyezi Mungu naye atakughufirieni nyinyi. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira na rehema.
التفاسير العربية:
إِنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞۚ وَٱللَّهُ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ
Hakika mali yenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.
Hakika mali yenu na watoto wenu ni majaribio na mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa kwa anaye pendelea kumt'ii Mwenyezi Mungu.
التفاسير العربية:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ وَٱسۡمَعُواْ وَأَطِيعُواْ وَأَنفِقُواْ خَيۡرٗا لِّأَنفُسِكُمۡۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio walio fanikiwa.
Basi tumieni juhudi zenu na nguvu zenu katika kumcha Mwenyezi Mungu. Na sikieni mawaidha yake, na t'iini amri zake, na toeni katika alicho kuruzukuni kwa ajili ya hicho alicho amrisha kitolewe kwa ajili yake. Na tendeni kheri kwa sababu ya nafsi zenu. Na mwenye kuzuiliwa na Mwenyezi Mungu ubakhili na uchoyo wa roho yake, basi watu kama hao ndio walio jaaliwa kupata kila kheri.
التفاسير العربية:
إِن تُقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعِفۡهُ لَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ
Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni mardufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukra, Mpole.
Mkitoa katika mambo ya kheri kutoa kwa moyo safi, basi Mwenyezi Mungu atazidisha mardufu thawabu za mlicho toa, na atakusameheni madhambi yenu yaliyo kuponyokeni. Na Mwenyezi Mungu ni Mkuu wa shukrani, na kuwalipa watendao mema, na ni Mpole, hafanyi haraka kuwaadhibu wanao muasi.
التفاسير العربية:
عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Mwenye kujua siri na dhaahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Yeye ni Mjuzi wa vilivyo fichikana na vinavyo onekana, Mwenye nguvu, Mtenda nguvu, Mwenye hikima katika mipango ya viumbe vyake, Mwenye kuweka kila kitu kwa pahala pake.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: التغابن
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق