للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: التحريم   آية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ تُوبُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ تَوۡبَةٗ نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيُدۡخِلَكُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ يَوۡمَ لَا يُخۡزِي ٱللَّهُ ٱلنَّبِيَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥۖ نُورُهُمۡ يَسۡعَىٰ بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَبِأَيۡمَٰنِهِمۡ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتۡمِمۡ لَنَا نُورَنَا وَٱغۡفِرۡ لَنَآۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
Enyi mlio amini! Rejeeni kwa Mwenyezi Mungu, muache madhambi yenu, mrejee kweli kweli kwa ikhlasi. Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu, na akakutieni Peponi kwenye kupita mito chini ya majumba yake na miti yake, Siku atakayo inyanyua Mwenyezi Mungu hadhi ya Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao hao itakuwa inakwenda mbele yao, nayo itakuwa kuliani mwao, nao watakuwa wakisema kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu: Ewe Bwana wetu, Mwenye kumiliki mambo yetu! Tutimizie nuru yetu, mpaka tuongoke kufikia Peponi. Na tusamehe dhambi zetu. Hakika Wewe ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ
Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makaazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.
Ewe Nabii! Pambana kwa Jihadi na hao walio tangaza ukafiri wao, na wanaafiki walio uficha ukafiri wao, kwa kila unacho kimiliki, nguvu na hoja. Na kuwa mkali juu ya makundi yote mawili hayo katika Jihadi yako. Na makaazi ya hao ni Jahannamu. Na marejeo maovu ni hayo marejeo yao!
التفاسير العربية:
ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱمۡرَأَتَ نُوحٖ وَٱمۡرَأَتَ لُوطٖۖ كَانَتَا تَحۡتَ عَبۡدَيۡنِ مِنۡ عِبَادِنَا صَٰلِحَيۡنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمۡ يُغۡنِيَا عَنۡهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَقِيلَ ٱدۡخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّٰخِلِينَ
Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!
Mwenyezi Mungu ametaja hali ya ajabu inayo juulikana kuwa ni hali zinazo fanana kwa wanao kufuru. Nayo ni hali ya mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Hao walikuwa chini ya ulinzi wa waja wawili katika waja wema. Nao wakawakhuni kwa kupanga njama dhidi yao, na kufichua siri zao kwenda wambia kaumu zao. Na waja wema wawili hawakuweza kuwakinga wake zao kwa lolote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wakaambiwa hao wake wawili walipo angamizwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!
التفاسير العربية:
وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱمۡرَأَتَ فِرۡعَوۡنَ إِذۡ قَالَتۡ رَبِّ ٱبۡنِ لِي عِندَكَ بَيۡتٗا فِي ٱلۡجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرۡعَوۡنَ وَعَمَلِهِۦ وَنَجِّنِي مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.
Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa Waumini kisa cha mke wa Firauni alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba karibu na rehema yako Peponi, na uniokoe na utawala wa Firauni na vitendo vyake vilivyo pita mipaka katika dhulma, na uniokoe na kaumu ya wanao fanya uadui!
التفاسير العربية:
وَمَرۡيَمَ ٱبۡنَتَ عِمۡرَٰنَ ٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتۡ بِكَلِمَٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتۡ مِنَ ٱلۡقَٰنِتِينَ
Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu.
Na Mwenyezi Mungu amewapigia Waumini mfano wa Mariamu binti wa Imrani, ambaye amehifadhi utupu wake, tukampulizia humo katika roho yetu, akashika mimba ya Isa. Naye akayasadiki maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni amri zake, na makatazo yake, na Vitabu vilivyo teremshwa juu ya Mitume wake. Na yeye alikuwa miongoni mwa idadi walio dumu juu ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. (Huku kupuliziwa Mariamu roho ya Mwenyezi Mungu si kiroja, kwani wanaadamu wote wamepuliziwa kadhaalika. Soma Surat Al-H'ijr Aya 28-29 inapo simuliwa alipo umbwa mtu na akapuliziwa kutokana na roho ya Mwenyezi Mungu.)
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: التحريم
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق