للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى * - فهرس التراجم


ترجمة معاني سورة: طه   آية:
إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ
Pale tulipomfunulia mama yako yaliyofunuliwa,
التفاسير العربية:
أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوّٞ لِّي وَعَدُوّٞ لَّهُۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةٗ مِّنِّي وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِيٓ
Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayotokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
التفاسير العربية:
إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ
Dada yako alipokwenda na akasema: Je! Niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuua mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa, ewe Musa!
التفاسير العربية:
وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِي
Na nimekuteua kwa ajili ya nafsi yangu.
التفاسير العربية:
ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَٰتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكۡرِي
Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.
التفاسير العربية:
ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
التفاسير العربية:
فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
التفاسير العربية:
قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ
Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.
التفاسير العربية:
قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِي مَعَكُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ
Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.
التفاسير العربية:
فَأۡتِيَاهُ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَا تُعَذِّبۡهُمۡۖ قَدۡ جِئۡنَٰكَ بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكَۖ وَٱلسَّلَٰمُ عَلَىٰ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلۡهُدَىٰٓ
Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani iwe juu ya atakayefuata uwongofu.
التفاسير العربية:
إِنَّا قَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡنَآ أَنَّ ٱلۡعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anayekadhibisha na akapuuza
التفاسير العربية:
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَٰمُوسَىٰ
(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
التفاسير العربية:
قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِيٓ أَعۡطَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ خَلۡقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ
Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.
التفاسير العربية:
قَالَ فَمَا بَالُ ٱلۡقُرُونِ ٱلۡأُولَىٰ
Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: طه
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى - فهرس التراجم

صادرة عن جمعية خدمة المحتوى الإسلامي باللغات.

إغلاق