للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى * - فهرس التراجم


ترجمة معاني سورة: النساء   آية:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلٗا
Na wale walioamini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitazo mito kwa chini yake. Watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli. Na ni nani mkweli zaidi wa kauli kuliko Mwenyezi Mungu.
التفاسير العربية:
لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Mwenye kufanya ubaya, atalipwa kwa huo, wala hatajipatia kando na Mwenyezi Mungu mlinzi wala wa kumnusuru.
التفاسير العربية:
وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا
Na mwenye kufanya katika mema, akiwa wa kiume au wa kike, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa kiasi cha jicho la kokwa ya tende.
التفاسير العربية:
وَمَنۡ أَحۡسَنُ دِينٗا مِّمَّنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبۡرَٰهِيمَ خَلِيلٗا
Na ni nani aliye bora zaidi kwa dini kuliko yule aliyeusilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni mwema, na akafuata mila ya Ibrahim mnyoofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwandani.
التفاسير العربية:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika dunia. Na Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu.
التفاسير العربية:
وَيَسۡتَفۡتُونَكَ فِي ٱلنِّسَآءِۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِيهِنَّ وَمَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ فِي يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِي لَا تُؤۡتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرۡغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلۡوِلۡدَٰنِ وَأَن تَقُومُواْ لِلۡيَتَٰمَىٰ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمٗا
Na wanakuuliza kuhusiana na wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu anawatolea fatwa juu yao, na yale mnayosomewa katika Kitabu hiki kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi kile walichoandikiwa, na mnapenda kwamba muwaoe, na kuhusu wanyonge katika watoto, na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na chochote mnachofanya katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua vyema.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: النساء
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى - فهرس التراجم

صادرة عن جمعية خدمة المحتوى الإسلامي باللغات.

إغلاق