Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makaazi yao.
Hakika Mwenyezi Mungu atawatia wenye kuamini na wakatenda mema katika Pepo tukufu zenye kupitiwa ndani yake mito. Na makafiri wanastarehe duniani kidogo, na wanakula kama walavyo wanyama, wamepigwa na mghafala wala hawajifikirii mwisho wao. Hawanalo lao ila matamanio yao. Na kesho Akhera nyumba yao ni Motoni.
Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu ulio kutoa; nao tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru.
Na wengi katika watu wa miji walio tangulia walio kuwa na nguvu zaidi kushinda watu wa mji wako wa Makka ambao watu wake wamekufukuza, ewe Muhammad, tuliwaangamiza kwa namna mbali mbali za adhabu. Na hakutokea yeyote wa kuwanusuru nasi.
Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao?
Je! Wanaweza kuwa sawa makundi mawili haya katika malipo? Mwenye kuwa na ujuzi wazi kumjua Muumba wake na Mlezi wake, naye akawa anamt'ii, atakuwa sawa na mwenye kuwa na vitendo vyake viovu naye akaviona ni vizuri, na akafuata hayo ayatendayo na akaeneza pumbao lake la upotovu.
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?
Sifa ya Pepo walio ahidiwa wachamngu ni kama hivi: ndani yake imo mito ya maji yasiyo chafuka, na mito ya maziwa yasiyo haribika utamu wake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa na takataka zote. Na humo watakuwa na kila namna ya matunda, na msamaha mkubwa kutokana na Mola wao Mlezi. Je! Sifa za Pepo ya hawa ni kama sifa itayo kuwa ni malipo ya mwenye kudumu milele Motoni, na akanyweshwa maji yaliyo tokota ya kukata matumbo? Aya hii tukufu inataka tuzingatie kuwa maji yaliyo vunda, yaliyo tuama, yenye kutaghayari, ni maji yenye madhara. Na Aya hii tukufu imesema hayo kabla ya kuvumbuliwa darubini za kutazamia vijidudu (Microscope) kwa makarne ya miaka, ndipo ilipo juulikana kuwa maji yaliyo tuama yaliyo taghayari yanakuwamo ndani yake mamilioni ya vijidudu vyenye madhara ya kuwasibu watu na wanyama kwa namna mbali mbali ya magonjwa.
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.
Na miongoni mwa makafiri kipo kikundi cha watu wanao kusikiliza wewe, Muhammad. Hawakuamini wewe, wala hawanafiiki na maneno yako. Mpaka wakisha ondoka kwenye baraza yako husema kwa kejeli kuwaambia walio pewa ujuzi: Kasema nini huyu Muhammad sasa hivi? Watu hao ndio Mwenyezi Mungu amepiga muhuri wa ukafiri juu ya nyoyo zao. Ndio wameiacha kheri wakifuata matamanio yao.
Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi kukumbuka hapo?
Wanao kanusha hawawaidhiki na hali za walio tangulia. Basi je! Wanangojea Saa (ya Kiyama) iwajie kwa ghafla? Kwa hakika alama zake zimekwisha dhihiri, na wao hawajazingatia kuwa inakuja. Basi watakumbuka wapi itapo wajia mara moja kwa ghafla?
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
Basi thibiti juu ya ujuzi ya kwamba hakika hapana wa kuabudiwa kwa Haki ila Mwenyezi Mungu tu. Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu kwa dhambi yako na madhambi ya Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua kila lenu, la kupita na la kukaa.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
অনুসন্ধানৰ ফলাফল:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".