Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Hūd   Ayah:

Hud

الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Alif, Lām, Rā’. Maneno yashatangulia, kuhusu herufi zinazokatwa, katika mwanzo wa Sura ya Al-Baqarah. Hiki ni Kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Amemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na ambacho aya zake zimepangwa vizuri zisizo na kasoro wala ubatilifu, kisha zimefafanuliwa kwa maamrisho na makatazo na maelezo ya halali na haramu yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Aliye na hekima katika uendeshaji mambo Aliye Mtambuzi wa vile yanavyoishia.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ
Na kuteremsha Qur’ani na kuzifafanua hukumu zake na kuzipambanua na kuipanga vizuri, ili mpate kumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Mimi kwenu nyinyi, enyi watu, ni muonyaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenye kuwaonya mateso Yake na ni mwenye kuwabashiria habari njema ya malipo Yake mema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَنِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُمَتِّعۡكُم مَّتَٰعًا حَسَنًا إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى وَيُؤۡتِ كُلَّ ذِي فَضۡلٖ فَضۡلَهُۥۖ وَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ كَبِيرٍ
Na muombeni Awasamehe dhambi zenu kisha mrudi Kwake hali ya kujuta, Atawapumbaza katika ulimwengu wenu kwa kuwastarehesha vizuri kwa maisha mazuri humo mpaka ufikie kikomo muda wenu wa kuishi na Ampe kila mwenye wema wa elimu na matendo malipo makamilifu ya wema wake yasiyo na upungufu. Na mkiyapa mgongo yale ninayowaitia kwayo, basi nawachelea nyinyi kufikiwa na adhabu ya Siku ngumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Hili ni onyo kali kwa aliyezipa mgongo amri za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na akawakanusha Mitume Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Ni kwa Mwenyezi Mungu marejeo yenu baada ya kufa kwenu nyote, basi jitahadharini na mateso Yake. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Muweza wa kuwafufua nyinyi, kuwakusanya na kuwalipa.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَآ إِنَّهُمۡ يَثۡنُونَ صُدُورَهُمۡ لِيَسۡتَخۡفُواْ مِنۡهُۚ أَلَا حِينَ يَسۡتَغۡشُونَ ثِيَابَهُمۡ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Hakika washirikina hawa wanaficha ukafiri katika nyoyo zao wakidhani kwamba yale ambayo nafsi zao zinayadhamiria yanafichika kwa Mwenyezi Mungu. Kwani hawajui wanapoifinika miili yao kwa nguo zao kwamba hayafichiki kwa Mwenyezi Mungu mambo yao ya siri na ya wazi? Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila ambacho vifua vyao vinakifinika miongoni mwa nia, madhamirio na siri.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Hūd
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis - Translations’ Index

Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Sh. Naser Khamis

close