45 : 43

وَسۡـَٔلۡ مَنۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ مِن رُّسُلِنَآ أَجَعَلۡنَا مِن دُونِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ءَالِهَةٗ يُعۡبَدُونَ

Na uwaulize, ewe Mtume, wafuasi wa wale tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Mitume wetu na wabebaji sheria zao, «Je walikuja Mitume wao na ujumbe wa kuabudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu? Wao watakupasha habari kuwa hilo halikutokea, kwani Mitume wote walilingania kile ulichowaitia watu cha kumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake Asiye na mshirika, na wakakataza kuabudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu». info
التفاسير: |
prev

Az-Zukhruf

next
:
0:00 0:00