Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Ayah: (129) Surah: Al-A‘rāf
قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ
Walisema watu wa Mūsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kumwambia Nabii wao Mūsā, «Tulisumbuliwa na tukaudhiwa na nguvu za Fir'awn na watu wake, kwa kuuawa watoto wetu wa kiume na kuachiliwa wanawake wetu, kabla hujatujia na baada ya kutujia.» Mūsā akawaambia, «Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu, Fir'awn na watu wake, na Awaweke nyinyi katika ardhi yao badala yao, baada ya kuangamia kwao, Aangalie namna mtakavyofanya: mtashukuru au mtakufuru?»
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Ayah: (129) Surah: Al-A‘rāf
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close