Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Ayah: (150) Surah: Al-A‘rāf
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Aliporejea Mūsā kwa watu wake akiwa na hasira na huzuni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimpa habari kwamba watu wake wamepatikana na mtihani na kwamba Sāmirīy amewapoteza. Mūsā alisema, «Ni ubaya ulioje mlioufanya nyuma yangu baada ya mimi kuondoka! Je mumeitangulia amri ya Mola wenu?» Yaani, mulikufanyia haraka kuja kwangu kwenu, na hali ni jambo lililopangwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?. Mūsā alizitupa mbao za Taurati kwa kuwakasirikia watu wake walioabudu kigombe na kwa kumkasirikia ndugu yake Hārūn. Akakishika kichwa cha Hārūn na akakivuta upande wake. Hārūn alisema kwa kubembeleza, «Ewe mwana wa mamangu, ‘Hakika hawa watu walinidharau, waliniona ni mnyonge na walikaribia kuniua, kwa hivyo usiwafurahishe maadui kwa unayonifanya na usiniingize katika hasira zako ukanifanya ni pamoja na wale walioenda kinyume na amri yako na wakaabudu kigombe.’»
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Ayah: (150) Surah: Al-A‘rāf
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close