Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Ayah: (38) Surah: Al-A‘rāf
قَالَ ٱدۡخُلُواْ فِيٓ أُمَمٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِكُم مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ فِي ٱلنَّارِۖ كُلَّمَا دَخَلَتۡ أُمَّةٞ لَّعَنَتۡ أُخۡتَهَاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا ٱدَّارَكُواْ فِيهَا جَمِيعٗا قَالَتۡ أُخۡرَىٰهُمۡ لِأُولَىٰهُمۡ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ أَضَلُّونَا فَـَٔاتِهِمۡ عَذَابٗا ضِعۡفٗا مِّنَ ٱلنَّارِۖ قَالَ لِكُلّٖ ضِعۡفٞ وَلَٰكِن لَّا تَعۡلَمُونَ
Hapo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema kuwaambia washirikina hawa wazushi, «Ingieni Motoni mkiwa pamoja na makundi ya walio mfano wenu katika ukafiri, waliotangulia kabla yenu, kati ya majini na wanadamu. Kila kundi la mila mimoja likiingia Motoni litalaani watu wa kundi lingine linalofanana nalo, waliokuwa ni sababu ya kupotea kwake kwa kuwafuata. Mpaka watakapokutana ndani ya Moto wote pamoja: wa mwanzo, miongoni mwa wafuasi wa mila za kikafiri, na wa mwisho miongoni mwao; hapo watasema wa mwisho, waliokuwa ni watu wa kuandama ulimwenguni, kuwaambia viongozi wao, «Mola wetu, hawa ndio waliotupoteza wakatupotosha na haki, basi wape adhabu nyongeza ya Moto.» Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema, «Kila mmoja atapata nyongeza.» Yaani, kila mmoja kati yenu na wao atapata adhabu nyongeza ya Moto, «lakini nyinyi wafuasi hamuijui ile sehemu ya adhabu na machungu ambayo kila kundi miongoni mwenu ataipata.»
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Ayah: (38) Surah: Al-A‘rāf
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close