Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Ayah: (44) Surah: Al-A‘rāf
وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ أَن قَدۡ وَجَدۡنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقّٗا فَهَلۡ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمۡ حَقّٗاۖ قَالُواْ نَعَمۡۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنُۢ بَيۡنَهُمۡ أَن لَّعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ
Watu wa Peponi, baada ya kuingia humo, watawaita watu wa Motoni wawaambie, «Sisi tumeshapata kuwa ni kweli tuliyoahidiwa na Mola wetu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuhusu kuwalipa wanaomtii. Je, nyinyi mumeyapata mliyoahidiwa na Mola wenu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuwa ni kweli kuhusu kuwaadhibu wanaomuasi?» Hapo watu wa Motoni watawajibu watu wa Peponi wakiwaambia, «Ndio, kwa kweli tumeyapata yale Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli.» Hapo Atatangaza mwenye kutangaza, akiwa kati baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni akisema, «Laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie watu madhalimu» ambao walikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wakamkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Ayah: (44) Surah: Al-A‘rāf
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close