Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani * - Translations’ Index

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Translation of the meanings Surah: Adh-Dhāriyāt   Ayah:
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ
Naapa kwa mbingu zenye njia!
Ninaapa kwa mbingu zenye njia zilizo wekwa baraabara.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.
Kwamba nyinyi msemapo mnayo yasema ni maneno ya kugongana.
Arabic explanations of the Qur’an:
يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
Huacha kuamini hiyo ahadi ya kweli na malipo yatakayo kuwa huyo anaye acha, kwa sababu amekhiari kufuata pumbao la nafsi yake kuliko akili yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ
Wazushi wameangamizwa.
Wameteketea waongo wanao sema katika khabari za Kiyama kuwa ni mambo ya dhana na kukisia tu, ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ
Ambao wameghafilika katika ujinga.
Ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo?
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
Siku watapo simamishwa Motoni wakichomwa!
Arabic explanations of the Qur’an:
ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
Wataambiwa: Onjeni adhabu yenu hii ambayo duniani mlikuwa mkiihimiza iwe.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
Walikuwa kulala kwao usiku ni kuchache, na wakikesha sana kwa ibada.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
Na mwishoni mwa usiku walikuwa wakiomba maghfira.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.
Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
Na katika mbingu ipo amri ya riziki zenu na kukadiriwa mnayo ahidiwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.
Arabic explanations of the Qur’an:
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
Akenda kwa mkewe naye ana khofu, akaja na ndama aliye nona.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
Akawakaribisha, nao hawakula. Akasema kwa kuto wajua hakika yao: Mbona hamli?
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Adh-Dhāriyāt
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani - Translations’ Index

Translated by Ali Muhsen Al-Berwani

close