Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Isrā’   Ayah:

Al-Isra

سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِيٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلٗا مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِي بَٰرَكۡنَا حَوۡلَهُۥ لِنُرِيَهُۥ مِنۡ ءَايَٰتِنَآۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
Ametakasika yule aliyempeleka mja wake usiku mmoja kutoka katika Msikiti Mtakatifu mpaka Msikiti wa Al-Aqswa, ambao tumebariki kandoni mwake, ili tumuonyeshe katika Ishara zetu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia zaidi, Mwenye kuona zaidi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَٰهُ هُدٗى لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُواْ مِن دُونِي وَكِيلٗا
Na tulimpa Musa Kitabu na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia) kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mtegemewa wenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ذُرِّيَّةَ مَنۡ حَمَلۡنَا مَعَ نُوحٍۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَبۡدٗا شَكُورٗا
Kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nuhu. Hakika yeye alikuwa mja wa kushukuru sana.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَضَيۡنَآ إِلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَتُفۡسِدُنَّ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَرَّتَيۡنِ وَلَتَعۡلُنَّ عُلُوّٗا كَبِيرٗا
Na tukawahukumia Wana wa Israili katika kitabu kwamba hakika mtafanya uharibifu katika ardhi mara mbili, na hakika mtapanda kiburi, kiburi kikubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ أُولَىٰهُمَا بَعَثۡنَا عَلَيۡكُمۡ عِبَادٗا لَّنَآ أُوْلِي بَأۡسٖ شَدِيدٖ فَجَاسُواْ خِلَٰلَ ٱلدِّيَارِۚ وَكَانَ وَعۡدٗا مَّفۡعُولٗا
Na itakapokuja ahadi ya kwanza yake, tutawatumia waja wetu wenye nguvu kubwa. Watawaingilia ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ رَدَدۡنَا لَكُمُ ٱلۡكَرَّةَ عَلَيۡهِمۡ وَأَمۡدَدۡنَٰكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَجَعَلۡنَٰكُمۡ أَكۡثَرَ نَفِيرًا
Kisha tukawarudishia nguvu zenu dhidi yao, na tukawasaidia kwa mali na wana, na tukawajalia mkawa wengi zaidi.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنۡ أَحۡسَنتُمۡ أَحۡسَنتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡۖ وَإِنۡ أَسَأۡتُمۡ فَلَهَاۚ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ لِيَسُـُٔواْ وُجُوهَكُمۡ وَلِيَدۡخُلُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوۡاْ تَتۡبِيرًا
Mkifanya wema, mnafanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, basi mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu na waingie msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Isrā’
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close