Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Adh-Dhāriyāt   Ayah:
۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema: 'Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mliotumwa?'
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema: 'Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu.'
Arabic explanations of the Qur’an:
لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ
Tuwatupie mawe ya udongo.
Arabic explanations of the Qur’an:
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ
Yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na katika habari za Musa, tulipomtuma kwa Firauni na hoja wazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: 'Huyu ni mchawi au mwendawazimu!'
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ
Na katika habari za 'Adi tulipowatumia upepo wa kukata uzazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ
Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichonyambuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ
Na katika habari za Thamudi walipoambiwa: 'Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.'
Arabic explanations of the Qur’an:
فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi ukawanyakua moto wa radi nao wanaona.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio wenye uwezo wa kuzitanua.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Adh-Dhāriyāt
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close