Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-An‘ām   Ayah:
ذَٰلِكَ أَن لَّمۡ يَكُن رَّبُّكَ مُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا غَٰفِلُونَ
Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma, hali ya kuwa wenyewe wameghafilika.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِكُلّٖ دَرَجَٰتٞ مِّمَّا عَمِلُواْۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعۡمَلُونَ
Na kila mmoja ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَرَبُّكَ ٱلۡغَنِيُّ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفۡ مِنۢ بَعۡدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوۡمٍ ءَاخَرِينَ
Na Mola wako Mlezi ndiye Asiyemhitaji yeyote, Mwenye rehema. Akitaka, atawaondoa na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyowatoa kutokana na dhuria ya kaumu wengine.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَأٓتٖۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ
Hakika, yale mnayoahidiwa yatafika, wala nyinyi hamtaweza kushinda.
Arabic explanations of the Qur’an:
قُلۡ يَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَامِلٞۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Sema: Enyi kaumu yangu! Fanyeni pahali penu mlipo, na hakika mimi ninafanya. Mtakuja jua ni ya nani yatakuwa makaazi mema mwishoni. Hakika, madhalimu hawafaulu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَجَعَلُواْ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلۡحَرۡثِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ نَصِيبٗا فَقَالُواْ هَٰذَا لِلَّهِ بِزَعۡمِهِمۡ وَهَٰذَا لِشُرَكَآئِنَاۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمۡ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمۡۗ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ
Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu. Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu, vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu, huwafikia washirikishwa wao. Ni uovu mno hayo wanayoyahukumu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٖ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ قَتۡلَ أَوۡلَٰدِهِمۡ شُرَكَآؤُهُمۡ لِيُرۡدُوهُمۡ وَلِيَلۡبِسُواْ عَلَيۡهِمۡ دِينَهُمۡۖ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ
Na kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwachanganyia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayozua ya uongo.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-An‘ām
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close