Check out the new design

Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Al-Hāqqah   Ayah:
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ
Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ
Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ
Basi ninaapa kwa mnavyoviona.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ
Na msivyoviona.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ
Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye heshima.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ
Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ
Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ
Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ
Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ
Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!
Arabic explanations of the Qur’an:
فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ
Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ
Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wacha Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ
Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanaokataa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Al-Hāqqah
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center - Translations’ Index

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

close