Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa wa kuiangamiza miji kwa dhulma, hali wenyewe wameghafilika.
Na huku kutuma Mitume, wenye kuonya na kubainisha ni kwa kuwa Mola wako Mlezi, ewe Nabii, haiangamizi miji kwa dhulma yao na watu wake wameghafilika na Haki tu. Bali hapana budi ila awabainishie kwa uwazi na awaonye.
Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.
Na kila mtenda kheri au mtenda shari ana daraja yake ya malipo kwa anayo yatenda. Ikiwa kheri atapata kheri, na ikiwa shari basi atapata shari. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika ndiye Muumba, si Mwenye kughafilika na wanayo yatenda. Bali hakika vitendo vyao vimo katika Kitabu kisicho acha dogo wala kubwa ila hulitia hisabuni.
Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu, kama vile alivyo kutoeni kutokana na uzazi wa watu wengine.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wako Mlezi, ni Mkwasi, hahitajii waja wala ibada zao. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye rehema iliyo kusanya kila kitu. Na kwa mujibu wa hayo ndio akakuamrisheni mtende mema, na akakukatazeni maovu. Naye ndiye Muweza. Akitaka atakuondoeni na alete duniani wenginewe wa kufuatia baada yenu kwa mujibu wa atakavyo. Wala hilo si gumu kwake Subhanahu, Aliye takasika. Kwani Yeye alikuumbeni kutokana na uzao wa wengine walio kutangulieni. Nanyi mkawa ndio warithi wa ardhi baada yao.
Bila ya shaka hayo mnayo ahidiwa yatafika tu, wala nyinyi hamtaweza kuyaepuka.
Na hayo anayo kuonyeni kwayo, nayo ni adhabu, na anayo kubashirieni kwayo, nayo ni thawabu baada ya kufufuliwa, na kukusanywa, na kuhisabiwa, yatakuja tu hapana hivi wala hivi. Wala nyinyi hamwezi kumshinda huyo anaye kutakeni Siku hiyo. Basi hamna uwezo wa kukataa kukusanyika wala kuhisabiwa.
Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na hakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa.
Ewe Nabii! Waambie kwa kuwatisha: Fanyeni kama mpendavyo kwa ukomo wa uwezo wenu. Na mimi nitafanya kwa mujibu wa Haki. Na mwishoe bila ya shaka mtajua nani atakuwa na khatima njema katika makaazi ya Akhera. Na hayo watayapata watu wa Haki, hapana hivi wala hivi. Kwa sababu nyinyi ni madhaalimu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaandikia kufuzu walio dhulumu.
Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimea na wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vya Mwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu.
Na washirikina, ambao wanayaabudu masanamu, wamo katika udanganyifu wa daima. Wao hufanya katika aliyo yaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika mazao ya mimea, na ngamia, na ng'ombe, na kondoo, fungu la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakiwatumilia wageni na wenye haja, na fungu jingine hulitumia katika kuwakhudumia masanamu ambayo wameyafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa mujibu wa madai yao! Ama walicho wawekea masanamu huwafikia masanamu yao, na hukitumia kwa ajili yao. Na walicho muwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu hakifiki chochote kwa hao wageni na mafakiri! Uovu ulioje huu wa hukumu yao ya dhulma! Kwani wao wameyafanya masanamu ndio wenziwe Mwenye kuumba hiyo mimea na wanyama, na hawatumii inavyo stahiki hicho walicho mwekea Mwenyezi Mungu.
Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwauwa watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua.
Kama ilivyo kuwa hayo mawazo yao yalivyo wapambia huo mgawanyo wa dhulma katika mazao ya mimea, na ngamia, na ng'ombe, na kondoo, alio umba Mwenyezi Mungu, basi kadhaalika mawazo yao yamewapambia, kutokana na hayo masanamu ambayo wanadai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, kuwauwa watoto wao pale wanapo zaliwa, na kuwa ati waliweka nadhiri kwa miungu yao kuwachinja watoto wao! Na hakika hayo mawazo yao yanawaangamiza na yanawavurugia mambo ya dini, kwa hivyo hawaielewi vilivyo! Na ilivyo kuwa mawazo yao yamezisaliti akili zao hadi hiyo, basi wewe waachilie mbali wao na hayo wanayo mzulia Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kukuzulia wewe. Nao watakuja pata malipo ya huo uzushi wao. Na hayo ndio matakwa ya Mwenyezi Mungu, kwani angeli taka wasingeli fanya hayo.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Resultados de la búsqueda:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".