Check out the new design

Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah * - Índice de traducciones


Traducción de significados Capítulo: Al-Nisaa   Versículo:
وَٱسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na muombe Mwenyezi Mungu kufutiwa dhambi. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Las Exégesis Árabes:
وَلَا تُجَٰدِلۡ عَنِ ٱلَّذِينَ يَخۡتَانُونَ أَنفُسَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمٗا
Wala usimbishanie wale wanaozihini nafsi zao. Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi yule ambaye ni haini mkubwa, mwenye dhambi nyingi.
Las Exégesis Árabes:
يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا
Wanawaficha watu, wala hawamfichi Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapopanga njama usiku kwa maneno asiyoyapenda. Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka vyema wanayoyatenda.
Las Exégesis Árabes:
هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ جَٰدَلۡتُمۡ عَنۡهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَمَن يُجَٰدِلُ ٱللَّهَ عَنۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا
Hivi ni nyinyi hawa mmewabishania katika uhai huu wa duniani. Basi ni nani atakayewabishania dhidi ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea?
Las Exégesis Árabes:
وَمَن يَعۡمَلۡ سُوٓءًا أَوۡ يَظۡلِمۡ نَفۡسَهُۥ ثُمَّ يَسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na anayetenda uovu au akaidhulumu nafsi yake, kisha akaomba kufutiwa dhambi kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Las Exégesis Árabes:
وَمَن يَكۡسِبۡ إِثۡمٗا فَإِنَّمَا يَكۡسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Na mwenye kuchuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Las Exégesis Árabes:
وَمَن يَكۡسِبۡ خَطِيٓـَٔةً أَوۡ إِثۡمٗا ثُمَّ يَرۡمِ بِهِۦ بَرِيٓـٔٗا فَقَدِ ٱحۡتَمَلَ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا
Na mwenye kuchuma kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika kashfa na dhambi iliyo wazi.
Las Exégesis Árabes:
وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao lingedhamiria kukupoteza. Na hawapotezi isipokuwa nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima, na akakufundisha yale uliyokuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa.
Las Exégesis Árabes:
 
Traducción de significados Capítulo: Al-Nisaa
Índice de Capítulos Número de página
 
Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah - Índice de traducciones

Traducida por el equipo del Centro Rowad Al-Taryamah en cooperación con la Asociación de Dawah en Rabwa y la Asociación para el Servicio del Contenido Islámico en Idiomas.

Cerrar