Check out the new design

Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah * - Índice de traducciones


Traducción de significados Capítulo: Al-An'aam   Versículo:
۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰۖ يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَمُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتِ مِنَ ٱلۡحَيِّۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na mwenye kumtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa?
Las Exégesis Árabes:
فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ
Ndiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote.
Las Exégesis Árabes:
وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهۡتَدُواْ بِهَا فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ
Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali ya bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua.
Las Exégesis Árabes:
وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ فَمُسۡتَقَرّٞ وَمُسۡتَوۡدَعٞۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَفۡقَهُونَ
Na Yeye ndiye aliyewazalishia kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu.
Las Exégesis Árabes:
وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَيۡءٖ فَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهُ خَضِرٗا نُّخۡرِجُ مِنۡهُ حَبّٗا مُّتَرَاكِبٗا وَمِنَ ٱلنَّخۡلِ مِن طَلۡعِهَا قِنۡوَانٞ دَانِيَةٞ وَجَنَّٰتٖ مِّنۡ أَعۡنَابٖ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشۡتَبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٍۗ ٱنظُرُوٓاْ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَيَنۡعِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمۡ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Na Yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tukatoa mimea ya kila kitu. Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani, tukatoa ndani yake punje zilizopandana; na kutokana na mitende katika makole yake yakatoka mashada yaliyo karibu; na mabustani ya mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yakaiva. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini.
Las Exégesis Árabes:
وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلۡجِنَّ وَخَلَقَهُمۡۖ وَخَرَقُواْ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَٰتِۭ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ
Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu ya hayo wanayomsifu kwayo!
Las Exégesis Árabes:
بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَمۡ تَكُن لَّهُۥ صَٰحِبَةٞۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu.
Las Exégesis Árabes:
 
Traducción de significados Capítulo: Al-An'aam
Índice de Capítulos Número de página
 
Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al suajili - El Centro de Rowad Al- Taryamah - Índice de traducciones

Traducida por el equipo del Centro Rowad Al-Taryamah en cooperación con la Asociación de Dawah en Rabwa y la Asociación para el Servicio del Contenido Islámico en Idiomas.

Cerrar