Check out the new design

ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس * - لیست ترجمه ها


ترجمهٔ معانی سوره: نحل   آیه:
۞ يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na wakumbushe wao, ewe Mtume, Siku ya Kiyama pindi itakapokuja kila nafsi ikijitetea yenyewe na kutoa nyudhuru za kila aina, na hapo Mwenyezi Mungu Ailipe kila nafsi malipo ya ilichokifanya bila ya kuidhulumu. Hatawaongezea mateso wala hawatapunguzia malipo yao.
تفسیرهای عربی:
وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا قَرۡيَةٗ كَانَتۡ ءَامِنَةٗ مُّطۡمَئِنَّةٗ يَأۡتِيهَا رِزۡقُهَا رَغَدٗا مِّن كُلِّ مَكَانٖ فَكَفَرَتۡ بِأَنۡعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلۡجُوعِ وَٱلۡخَوۡفِ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ
Na Mwenyezi Mungu Amepiga mfano wa mji wa Makkh. Ulikuwa uko kwenye salama ya kutofanyiwa uadui, utulivu kutokana na dhiki za maisha na unajiliwa na riziki zake kwa uzuri na usahali kutoka kila upande, wakazi wake wakazikanusha neema za Mwenyezi Mungu kwao, wakamshirikisha na wasimshukuru, hapo Mwenyezi Mungu Akawatesa kwa njaa na kicho kwa kuviogopa vikosi vya Mtume, reheme ya Mwenyezi Mungu na amni zimshukiye, na majeshi yake yaliyokuwa yakiwatisha, na hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na vitendo vyao vya ubatilifu.
تفسیرهای عربی:
وَلَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡهُمۡ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu Alipeleka kwa watu wa Makkah Mtume miongoni mwao, yeye ni Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanaijua nasaba yake, ukweli wake na uaminifu wake, wasiyakubali yale aliyowajia nayo na wasimuamini. Hapo iliwapata adhabu ya shida, njaa, kicho na kuuawa wakuu wao huko Badr na hali wao ni madhalimu wa nafsi zao kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwazuia watu njia Yake.
تفسیرهای عربی:
فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ
Basi kuleni, enyi Waumini, miongoni mwa vile ambavyo Mwenyezi Mungu Amewaruzuku na Akavifanya ni halali nzuri kwenu. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu kwenu, kwa kuzitambua na kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu, iwapo nyinyi, kikweli, ni wenye kuandama amri Yake, ni wenye kusikia na kumtii Yeye, mnamuabudu Yeye Peke Yake, Asiye na mshirika.
تفسیرهای عربی:
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحۡمَ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦۖ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ غَيۡرَ بَاغٖ وَلَا عَادٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Hakika Amewaharamishia mfu wa mnyama, damu yenye kutiririka kutoka kwa mnyama aliechinjwa pale achinjwapo, nyama ya nguruwe na mnyama aliyechinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini yoyote Aliyelazimika kula chochote kati ya vitu hivi vilivyoharamishwa, kwa dharura ya kuogopa kufa, na hali yeye si dhalimu wala si mkiukaji mpaka ya dharura, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye, Hatamtesa kwa kwa kitendo alichokifanya.
تفسیرهای عربی:
وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ
wala msiseme, enyi washirikina, urongo unaotolewa na ndimi zenu: «hii ni halali» juu ya kitu kilichoharamishwa «na hii ni haramu» juu ya kitu kilichohalalishwa, ili kumzulia Mwenyezi Mungu urongo kwa kumnasibishia uhalalishaji na uharamishaji. Hakika wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu urongo hawatafaulu kupata wema wowote ulimwenguni wala Akhera.
تفسیرهای عربی:
مَتَٰعٞ قَلِيلٞ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Starehe walionayo duniani na starehe yenye kuondoka na ni chache. Na huko Akhera watapata adhabu iumizayo.
تفسیرهای عربی:
وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا مَا قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُۖ وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Na Mayahudi tuliwaharamishia vile vitu tulivyokupa habari zake, ewe Mtume, kabla, navyo ni kila mnyama mwenye kucha na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa kile kilichobebwa na migongo yao au matumbo yao au kilichotangamana na mifupa. Na sisi hatukuwadhulumu wao , lakini wao walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kufanya uadui, ndipo wakastahili kuharamishiwa kwa njia ya kutiwa adabu.
تفسیرهای عربی:
 
ترجمهٔ معانی سوره: نحل
فهرست سوره ها شماره صفحه
 
ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس - لیست ترجمه ها

مترجم: دکتر عبد الله محمد ابو بکر و شیخ ناصر خميس.

بستن