ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس * - لیست ترجمه ها


ترجمهٔ معانی سوره: سوره غافر   آیه:

Surat Ghafir

حمٓ
«Ḥā, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.
تفسیرهای عربی:
تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ
Kuteremshiwa Qur’ani Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kunatokana na Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, Mwenye ushindi Ambaye kwa enzi Yake amekilazimisha kila kiumbe, Mwenye ujuzi wa kila kitu.
تفسیرهای عربی:
غَافِرِ ٱلذَّنۢبِ وَقَابِلِ ٱلتَّوۡبِ شَدِيدِ ٱلۡعِقَابِ ذِي ٱلطَّوۡلِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ إِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ
Mwenye kusamehe dhambi za wafanya dhambi, Mwenye kukubali toba ya wenye kutubia, Mkali wa kutesa juu ya aliyejasiri kufanya dhambi na kutotubia kutokana nayo. Na Yeye. Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mwenye kuwaneemesha na kuwafadhili waja Wake watiifu. Hakuna muabudiwa yoyote anayefaa kuabudiwa isipokuwa Yeye. Kwake Yeye ndio mwisho wa viumbe wote Siku hiyo ya Hesabu, ili Amlipe kila mmoja kile anachostahiki.
تفسیرهای عربی:
مَا يُجَٰدِلُ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَا يَغۡرُرۡكَ تَقَلُّبُهُمۡ فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Hakuna anayeteta kuhusu aya za Mwenyezi Mungu na dalili Zake za kutolea ushahidi umoja wa Mwenyezi Mungu, akawa anazikabili kwa ubatilifu isipokuwa wapinzani wenye kukataa kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake. Basi kusikudanganye wewe kule kutanga kwao mijini kwa aina mbalimbali za biashara, shughuli za kuchuma, starehe za ulimwenguni na uzuri wake.
تفسیرهای عربی:
كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَٱلۡأَحۡزَابُ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۖ وَهَمَّتۡ كُلُّ أُمَّةِۭ بِرَسُولِهِمۡ لِيَأۡخُذُوهُۖ وَجَٰدَلُواْ بِٱلۡبَٰطِلِ لِيُدۡحِضُواْ بِهِ ٱلۡحَقَّ فَأَخَذۡتُهُمۡۖ فَكَيۡفَ كَانَ عِقَابِ
Walikanusha, kabla ya makafiri hawa, watu wa Nūḥ na waliowafuata wao miongoni mwa ummah waliotangaza vita vyao dhidi ya Mitume, kama vile 'Ād na Thamūd, kwa kuwa waliazimia kuwaudhi na wakaamua kwa umoja wao wawaadhibu au wawaue. Na kila watu, miongoni mwa ummah hawa wenye kuwakanusha Mitume wao, walitaka kumuua Mtume wao na wakajadiliana na yeye kwa njia ya ubatilifu ili waitangue haki kwa kujadili kwao, na kwa hivyo nikawatesa. Basi ni namna gani kule kuwatesa kwangu kulikuwa ni mazingatio kwa viumbe na mawaidha kwa watakaokuja baada yao?
تفسیرهای عربی:
وَكَذَٰلِكَ حَقَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ
Na kama yalivyothibiti mateso kwa ummah waliopita waliowakanusha Mitume wao, pia yalithibiti kwa wale waliokufuru kuwa wao ni watu wa Motoni.
تفسیرهای عربی:
ٱلَّذِينَ يَحۡمِلُونَ ٱلۡعَرۡشَ وَمَنۡ حَوۡلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْۖ رَبَّنَا وَسِعۡتَ كُلَّ شَيۡءٖ رَّحۡمَةٗ وَعِلۡمٗا فَٱغۡفِرۡ لِلَّذِينَ تَابُواْ وَٱتَّبَعُواْ سَبِيلَكَ وَقِهِمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Wale wanaoibeba ‘Arshi ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa Malaika na wale walioko pambizoni mwake kati ya wale wanaoizunguka miongoni mwao, wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kasoro, wanamshukuru kwa yale Anayostahiki, wanamuamini Yeye haki ya kumuamini na wanamuomba Awasamehe Waumini kwa kusema, «Mola wetu! Umekienea kile kitu kwa rehema na ujuzi. Kwa hivyo wasamehe wale waliotubia kutokana na ushirikina na maasia na wakafuata njia uliyowaamrisha waifuate, nayo ni Uislamu, na uwaepushie adhabu ya Moto na vituko vyake.
تفسیرهای عربی:
رَبَّنَا وَأَدۡخِلۡهُمۡ جَنَّٰتِ عَدۡنٍ ٱلَّتِي وَعَدتَّهُمۡ وَمَن صَلَحَ مِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَأَزۡوَٰجِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
«Mola wetu! Na uwatie Waumini kwenye mabustani ya Pepo ya 'Adn uliyowaahidi wao na baba zao, wake zao na watoto wao waliokuwa wema kwa Imani na matendo mazuri. Hakika wewe Ndiye Mshindi Mwenye kukilazimisha kila kitu, Ndiye Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake na utengenezaji Wake.
تفسیرهای عربی:
وَقِهِمُ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ وَمَن تَقِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ يَوۡمَئِذٖ فَقَدۡ رَحِمۡتَهُۥۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
«Na uwaepushie mwisho mbaya wa dhambi zao, usiwaadhibu kwa dhambi hizo. Na yoyote yule utakayemuepushia maovu Siku ya kuhesabiwa, huyo umeshamrehemu na umempa neema ya kuokolewa na adhabu yako. Na huko ndiko kufaulu kukubwa ambako hakuna kufaulu kupita huko.»
تفسیرهای عربی:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنَادَوۡنَ لَمَقۡتُ ٱللَّهِ أَكۡبَرُ مِن مَّقۡتِكُمۡ أَنفُسَكُمۡ إِذۡ تُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلۡإِيمَٰنِ فَتَكۡفُرُونَ
Hakika ya wale waliokanusha kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki na wakaielekeza ibada kwa asiyekuwa Yeye, watakapovishuhudia wenyewe vituko vya Moto watajichukia machukivu makubwa, na hapo walinzi wa Moto wa Jahanamu watawaita na kuwaambia, «Machukivu ya Mwenyezi Mungu kwenu huko ulimwenguni, Alipowataka nyinyi mumuamini Yeye na muwafuate Mitume Wake na mkakataa, yalikuwa makubwa zaidi kuliko vile mnavyojichukia nyinyi wenyewe hivi sasa, baada ya kujua kwenu kuwa mnastahili hasira za mwenyezi Mungu na adhabu Yake.»
تفسیرهای عربی:
قَالُواْ رَبَّنَآ أَمَتَّنَا ٱثۡنَتَيۡنِ وَأَحۡيَيۡتَنَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَٱعۡتَرَفۡنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلۡ إِلَىٰ خُرُوجٖ مِّن سَبِيلٖ
Makafiri watasema, «Mola wetu! Umetufisha mara mbili: tulipokuwa matone ya manii ndani ya matumbo ya mama zetu kabla ya kupulizwa roho na ulipokoma muda wetu wa kuishi katika uhai wa duniani, na umetuhuisha mara mbili:katika nyumba ya duniani siku tuliyozaliwa na siku tuliyofufuliwa kutoka makaburini mwetu. Kwa hivyo sisi sasa tunakubali makosa yetu yaliyotangulia, basi je kuna njia yoyote ya sisi kutoka Motoni na uturudishe kupitia njia hiyo duniani tukapate kufanya matendo ya utiifu kwako?» Lakini haliwi hilo kabisa la wao kunufaika kwa kukubali kwao huku.
تفسیرهای عربی:
ذَٰلِكُم بِأَنَّهُۥٓ إِذَا دُعِيَ ٱللَّهُ وَحۡدَهُۥ كَفَرۡتُمۡ وَإِن يُشۡرَكۡ بِهِۦ تُؤۡمِنُواْۚ فَٱلۡحُكۡمُ لِلَّهِ ٱلۡعَلِيِّ ٱلۡكَبِيرِ
Adhabu hiyo ambayo itakayowapata, enyi makafiri, ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlikuwa mkiitwa kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia matendo mema Kwake mnalikanusha hilo, na ashirikishwapo Mwenyezi Mungu mnaliamini hilo na mnalifuata. Basi Mwenyezi Mungu Ndiye Muamuzi kwa viumbe wake, Ndiye Muadilifu Asiyedhulumu, Anamuongoza Ananayemtaka na Anampoteza Anayemtaka, Anamrehemu Anayemtaka na Anamuadhibu Anayemtaka. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliye juu kidhati, kicheo na kinguvu (kupitisha Analolitaka).
تفسیرهای عربی:
هُوَ ٱلَّذِي يُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ رِزۡقٗاۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ
Yeye Ndiye Anayewaonyesha, enyi watu, uweza Wake kwa zile alama kubwa zenye kutolea ushahidi ukamilifu wa Mwenye kuziumba na kuzianzisha, na Anawateremshia mvua kutoka mawinguni ambayo kwayo mnaruzukiwa. Na hajikumbushi kwa alama hizi isipokuwa yule anayerudi kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada.
تفسیرهای عربی:
فَٱدۡعُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Basi, enyi waumini, mtakasieni Mwenyezi Mungu Peke Yake ibada na dua, na endeni kinyume na washirikina katika nyendo zao, na hata kama hilo litawakasirisha wao msiwajali.
تفسیرهای عربی:
رَفِيعُ ٱلدَّرَجَٰتِ ذُو ٱلۡعَرۡشِ يُلۡقِي ٱلرُّوحَ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ لِيُنذِرَ يَوۡمَ ٱلتَّلَاقِ
Mwenyezi Mungu Ndiye Mtukufu Aliye juu kabisa Ambaye daraja Zake zimepaa juu sana kwa namna ya kuwa Yeye, kwa daraja hizo, Ameepukana na viumbe Vyake na kimekuwa juu cheo Chake. Yeye Ndiye Mwenye 'Arsh iliyo kubwa. Na miongoni mwa rehema Zake kwa waja Wake ni kuwatumia Wajumbe kuwapelekea wahyi ambao kwa wahyi huo wanapata uhai na kuwa kwenye mwangaza wa kuwapa muelekeo katika mambo yao, ili hao Mitume (walioletewa wahyi) wawaogopeshe waja wa Mwenyezi Mungu na wawaonye Siku ya Kiyama ambayo watakutana Siku hiyo wa mwanzo na wa mwisho.
تفسیرهای عربی:
يَوۡمَ هُم بَٰرِزُونَۖ لَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنۡهُمۡ شَيۡءٞۚ لِّمَنِ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَۖ لِلَّهِ ٱلۡوَٰحِدِ ٱلۡقَهَّارِ
Siku ya Kiyama watajitokeza viumbe mbele ya Mola wao, hakuna chochote kuhusu wao au kuhusu matendo yao waliyoyafanya ulimwenguni kitakachofichamana kwa Mwenyezi Mungu. Hapo Atasema Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Ni wa nani ufalme na mamlaka Siku ya Leo?» Na Ajijibu Mwenyewe, «Ni vya Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake, Mwenye kutendesha nguvu Aliyevilazimisha viumbe vyote kwa uweza Wake na enzi Yake.»
تفسیرهای عربی:
ٱلۡيَوۡمَ تُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۚ لَا ظُلۡمَ ٱلۡيَوۡمَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ
Leo italipwa kila nafsi kwa kile ilichokitenda duniani, chema au kiovu; hakuna maonevu leo kufanyiwa yoyote, ya kuongezewa dhambi zake au kupunguziwa thawabu zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwpesi wa kuhesabu, basi msiione Siku hiyo ni yenye kuchelewa kufika, kwani iko karibu.
تفسیرهای عربی:
وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡأٓزِفَةِ إِذِ ٱلۡقُلُوبُ لَدَى ٱلۡحَنَاجِرِ كَٰظِمِينَۚ مَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنۡ حَمِيمٖ وَلَا شَفِيعٖ يُطَاعُ
Na uwaonye watu, ewe Mtume, na Siku ya Kiyama iliyo karibu, ingawa wao waiona kuwa iko mbali, pindi nyoyo za waja, kwa kuogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, zitakapopanda juu vifuani mwao na kushikana na koo zao, na hali wao wamejawa na hamu na huzuni. Madhalimu hawatakuwa na jamaa wa karibu wala rafiki wala muombezi wa kuwaombea kwa Mola wao akawa ni mwenye kukubaliwa.
تفسیرهای عربی:
يَعۡلَمُ خَآئِنَةَ ٱلۡأَعۡيُنِ وَمَا تُخۡفِي ٱلصُّدُورُ
Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Anakijua kile kinachopitishwa na maangalizi ya macho kwa njia ya siri na kuiba na kile ambacho mtu anakidhamiria katika nafsi yake kizuri au kibaya.
تفسیرهای عربی:
وَٱللَّهُ يَقۡضِي بِٱلۡحَقِّۖ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقۡضُونَ بِشَيۡءٍۗ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
Na Mwenyezi Mungu Anahukumu baina ya watu kwa uadilifu kwa kumpa kila mtu haki yake. Na wale waungu wanaoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, hawahukumu chochote kwa kutoweza kwao kufanya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyaona matendo wanayoyafanya, na Atawalipa kwayo.
تفسیرهای عربی:
۞ أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ كَانُواْ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُواْ هُمۡ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗ وَءَاثَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٖ
Kwani hawakutembea katika ardhi hawa wanaoukanusha utume wako, ewe Mtume, wakaangalia ulikuwa vipi mwisho wa ummah waliopita kabla yao? Walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao na wenye athari zilizosalia muda mrefu zaidi, na hazikuwafaa wao nguvu zao nyingi wala miili yao mikubwa yenye nguvu, kwani Mwenyezi Mungu Aliwapatiliza kwa kuwatesa, kwa sababu ya ukafiri wao na kutenda kwao madhambi, na hawakuwa na mwokoaji wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuizuia isiwafike.
تفسیرهای عربی:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَكَفَرُواْ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ قَوِيّٞ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ
Adhabu hiyo iliyowafikia wakanushaji waliopita ilikuwa ni kwa sababu ya msimamo wao juu ya Mitume ya Mwenyezi Mungu waliokuja na dalili za yakini za kuonesha ukweli wa madai yao, basi wakawakanusha na wakawafanya warongo na Mwenyezi Mungu Akawapatiliza kwa mateso Yake, hakika Yeye ni Mwenye nguvu hashindwi na yoyote, ni Mkali wa kutesa kwa aliyemkanusha na kumuasi.
تفسیرهای عربی:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ
Hakika tulimpelekea Mūsā alama zetu kubwa zenye kutolea ushahidi uhakika wa utume aliopewa na hoja zilizofunuka waziwazi juu ya ukweli wake katika ulinganizi wake, na kutanguka yale ambayo walikuwa nayo wale waliopelekewa hao Mitume.
تفسیرهای عربی:
إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَهَٰمَٰنَ وَقَٰرُونَ فَقَالُواْ سَٰحِرٞ كَذَّابٞ
Apate kuenda kwa Fir'awn, mfalme wa Misri, na Hāmān waziri wake, na Qārūn mwenye mali mengi na mahazina ya vitu vya thamani, wakaukanusha utume wake na wakafanya kiburi na wakamwambia, «Yeye ni mchawi mrongo sana, basi ni vipi anadai kuwa yeye ametumilizwa kwa watu kuwa ni Mtume?»
تفسیرهای عربی:
فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡحَقِّ مِنۡ عِندِنَا قَالُواْ ٱقۡتُلُوٓاْ أَبۡنَآءَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ وَٱسۡتَحۡيُواْ نِسَآءَهُمۡۚ وَمَا كَيۡدُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ
Basi Mūsā alipomjia Fir'awn, Hāmān na Qārūn kwa miujiza iliyo waziwazi kutoka kwetu, hawakutosheka kwa kuipinga na kuikanusha , bali walisema, «waueni wana wa kiume wa wale walioamini pamoja naye na waacheni wanawake wao watumike na wafanywe watumwa. Na haikuwa mipango ya makafiri isipokuwa ni yenye kupita na kuangamia.
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ ذَرُونِيٓ أَقۡتُلۡ مُوسَىٰ وَلۡيَدۡعُ رَبَّهُۥٓۖ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمۡ أَوۡ أَن يُظۡهِرَ فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡفَسَادَ
Na Fir'awn alisema kuwaambia watukufu wa watu wake, «Niacheni nimuue Mūsā, na amuombe Mola wake, anayedai kuwa Yeye Amemtumiliza kwetu, Amhifadhi na sisi. Mimi ninachelea asije akaigeuza dini yenu mliyonayo au asije akaeneza uharibifu kwenye ardhi ya Misri.»
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٖ لَّا يُؤۡمِنُ بِيَوۡمِ ٱلۡحِسَابِ
Na Mūsā akasema kumwambia Fir'awn na viongozi wa mamlaka yake, «Mimi nimeomba hifadhi kwa Mola wangu na Mola wenu, enyi watu, Anihami na kila mwenye kiburi cha kukataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, asiyeiamini Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atawahesabu viumbe Wake.»
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ رَجُلٞ مُّؤۡمِنٞ مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَكۡتُمُ إِيمَٰنَهُۥٓ أَتَقۡتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ ٱللَّهُ وَقَدۡ جَآءَكُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ مِن رَّبِّكُمۡۖ وَإِن يَكُ كَٰذِبٗا فَعَلَيۡهِ كَذِبُهُۥۖ وَإِن يَكُ صَادِقٗا يُصِبۡكُم بَعۡضُ ٱلَّذِي يَعِدُكُمۡۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَنۡ هُوَ مُسۡرِفٞ كَذَّابٞ
Na akasema mtu mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu miongoni mwa jamaa za Fir’awn anayeificha Imani yake akiwakemea watu wake, «Vipi nyinyi mtahalalisha kuuawa kwa mtu asiyekuwa na kosa kwenu isipokuwa anasema, ‘Mola wangu ni Mwenyezi Mungu’ na hali yeye amewajia na hoja za yakini kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa anayoyasema? Na iwapo Mūsā ni mrongo basi urongo wake utamdhuru mwenyewe, na iwapo ni mkweli basi baadhi ya yale anayowaonya kwayo yatawapata. Hakika Mwenyezi Mungu Hamuelekezi kwenye haki yoyote mwenye kupitisha mpaka kwa kuiacha haki na kuielekea batili, aliye mwingi wa urongo kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu ukiukaji wake.
تفسیرهای عربی:
يَٰقَوۡمِ لَكُمُ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَ ظَٰهِرِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِنۢ بَأۡسِ ٱللَّهِ إِن جَآءَنَاۚ قَالَ فِرۡعَوۡنُ مَآ أُرِيكُمۡ إِلَّا مَآ أَرَىٰ وَمَآ أَهۡدِيكُمۡ إِلَّا سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ
«Enyi watu wangu! Utawala ni wenu leo hali ya kuwa mna ushindi katika ardhi ya Misri juu raia wenu miongoni mwa Wana wa Isrāīl na wengineo. Ni nani atakayeizuia adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa itatushukia?» Fir’awn akasema kuwajibu watu wake, «Siwapatii ushauri, enyi watu, wala mawazo isipokuwa ule ninaouona kuwa ni mzuri na wa sawa kwangu na kwenu. Na siwaiti isipokuwa kwenye njia ya haki na usawa.»
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ ٱلَّذِيٓ ءَامَنَ يَٰقَوۡمِ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُم مِّثۡلَ يَوۡمِ ٱلۡأَحۡزَابِ
Na akasema yule Aliyeamini katika jamaa za Fir’awn kumwambia Fir’awn na viongozi wa mamlaka yake kwa kuwapa ushauri na kuwaonya, «Mimi ninawaogopea mkimuua Mūsā mfano wa siku ya makundi yaliyojikusanya dhidi ya manabii wao.
تفسیرهای عربی:
مِثۡلَ دَأۡبِ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۚ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعِبَادِ
«Mfano wa mwenendo wa watu wa Nūḥ, 'Ād, Thamūd na waliokuja baada yao katika ukafiri na ukanushaji, ambao Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa sababu ya hilo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Hataki kuwafanyia maonevu waja, Akawa Atawaadhibu bila dhambi walilolitenda. Mwenyezi Mungu Yuko juu sana mno kwa kujiepusha na maonevu na upungufu.
تفسیرهای عربی:
وَيَٰقَوۡمِ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ يَوۡمَ ٱلتَّنَادِ
«Na enyi watu wangu! Mimi ninawachelea nyinyi adhabu ya Siku ya Kiyama. Siku ambyo wataitana watu wao kwa wao kwa kituko cha Kisimamo Siku hiyo.
تفسیرهای عربی:
يَوۡمَ تُوَلُّونَ مُدۡبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنۡ عَاصِمٖۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ
«Siku ambayo mtazunguka muende hali ya kukimbia, hamtakuwa na mwenye kuwahami wala kuwanusuru. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Atamuachilia Asimuafikie kuufikia uongofu Wake, basi yeye hatakuwa na mtu mwenye kumuongoza kwenye haki na usawa.
تفسیرهای عربی:
وَلَقَدۡ جَآءَكُمۡ يُوسُفُ مِن قَبۡلُ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا زِلۡتُمۡ فِي شَكّٖ مِّمَّا جَآءَكُم بِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا هَلَكَ قُلۡتُمۡ لَن يَبۡعَثَ ٱللَّهُ مِنۢ بَعۡدِهِۦ رَسُولٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَنۡ هُوَ مُسۡرِفٞ مُّرۡتَابٌ
«Na Mwenyezi Mungu Aliwatumilizia kwenu Nabii mtukufu, Yūsuf mwana wa Ya’qūb, amani ziwashukie, kabla ya Mtume Mūsā, Akampatia dalili zilizo wazi juu ya ukweli wake, na Akawaamuru nyinyi kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika, mkaendelea kuwa na shaka juu ya yale aliyokuja nayo katika kipindi cha uhai wake mpaka alipokufa. Na alipokufa shaka yenu iliongezeka na pia ushirikina wenu na mkasema, ‘Mwenyezi Mungu Hatatuma mjumbe baada yake.’ Mfano wa upotevu huu ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyompoteza kila anayeikiuka haki, mwenye shaka juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Asimuafikie kwenye uongofu na unyofu.
تفسیرهای عربی:
ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡۖ كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلۡبِ مُتَكَبِّرٖ جَبَّارٖ
«Wale wanaobishana na aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake kwa kuzipinga bila kuwa na hoja zenye kukubalika, upinzani wao huo unawaletea machukivu makubwa kwa Mwenyezi Mungu na kwa wale walioamini, kama Alivyopiga muhuri kwenye nyoyo za hawa wapinzani na Akazifinika zisiongoke, ndivyo Anavyoupiga muhuri moyo wa kila mwenye kiburi cha kumfanya akatae kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, aliye mjeuri sana kwa wingi wa udhalimu wake na uadui wake.»
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَٰهَٰمَٰنُ ٱبۡنِ لِي صَرۡحٗا لَّعَلِّيٓ أَبۡلُغُ ٱلۡأَسۡبَٰبَ
Na Fir’awn akasema akimkanusha Mūsā katika ule mwito wake wa kumkubali Mola wa viumbe wote na kujisalimisha Kwake, «Ewe Hāmān! Nijengee jengo kubwa. Huenda mimi nikafikia milango ya mbingu au nikakifikia kile chenye kunifikisha hapo,
تفسیرهای عربی:
أَسۡبَٰبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُۥ كَٰذِبٗاۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرۡعَوۡنَ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَصُدَّ عَنِ ٱلسَّبِيلِۚ وَمَا كَيۡدُ فِرۡعَوۡنَ إِلَّا فِي تَبَابٖ
nipate kumtazama Mungu wa Mūsā mimi mwenyewe. Na mimi ninadhani kuwa Mūsā ni mrongo katika madai yake kwamba sisi tuna Mola na kwamba Yeye Yuko juu ya mbingu.» Hivyo ndivyo alivyopambiwa Fir'awn matendo yake mabaya akayadhania ni mazuri, na ndivyo alivyozuiliwa njia ya haki kwa sababu ya ubatilifu aliopambiwa nao. Na hazikuwa hila za Fir’awn na mipango yake ya kuwalaghai watu kuwa yeye yuko katika usawa na Mūsā yuko kwenye ubatilifu isipokuwa kwenye hasara na maangamivu, hakukuwa na kitu chenye kumfidisha isipokuwa ni kupata usumbufu wa duniani na Akhera.
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ ٱلَّذِيٓ ءَامَنَ يَٰقَوۡمِ ٱتَّبِعُونِ أَهۡدِكُمۡ سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ
Na akasema yule aliyeamini, akirudia ushauri wake, «Enyi watu wangu! Nifuateni niwaongoze njia ya uongofu na usawa.
تفسیرهای عربی:
يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا مَتَٰعٞ وَإِنَّ ٱلۡأٓخِرَةَ هِيَ دَارُ ٱلۡقَرَارِ
«Enyi watu wangu! Hakika ya uhai huu wa kilimwengu ni uhai wa watu kustarehe kidogo, kisha unakatika na kuondoka, basi inatakikana msiutegemee na kwamba Nyumba ya Akhera na starehe za daima zilizomo ndani ndiyo mahali pa makazi ya nyinyi kutulia humo, basi inatakikana muipe kipaumbele na mtende kwa ajili yake matendo mema ambayo yatawapatia furaha huko.
تفسیرهای عربی:
مَنۡ عَمِلَ سَيِّئَةٗ فَلَا يُجۡزَىٰٓ إِلَّا مِثۡلَهَاۖ وَمَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ يُرۡزَقُونَ فِيهَا بِغَيۡرِ حِسَابٖ
«Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu katika uhai wake na akapotoka kwenye njia ya uongofu, hatalipwa huko Akhera isipokuwa mateso yanayolingana na maasia yake. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na akafanya matendo mema, kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, awe mwanamume au mwanamke, na hali yeye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha, basi hao wataingia Peponi na humo Mwenyezi Mungu Atawaruzuku kutokana na matunda yake na starehe zake pasi na hesabu.
تفسیرهای عربی:
۞ وَيَٰقَوۡمِ مَا لِيٓ أَدۡعُوكُمۡ إِلَى ٱلنَّجَوٰةِ وَتَدۡعُونَنِيٓ إِلَى ٱلنَّارِ
«Na enyi watu wangu! Vipi mimi ninawalingania kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake Mūsā, nao ni ulinganizi utakaowafanya nyinyi muishie Peponi na muwe mbali na vituko vya Moto, na nyinyi mnanilingania kufany matendo yenye kupelekea kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake Motoni.?
تفسیرهای عربی:
تَدۡعُونَنِي لِأَكۡفُرَ بِٱللَّهِ وَأُشۡرِكَ بِهِۦ مَا لَيۡسَ لِي بِهِۦ عِلۡمٞ وَأَنَا۠ أَدۡعُوكُمۡ إِلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡغَفَّٰرِ
«Mnanilingania mimi nimkanushe Mwenyezi Mungu na nimshirikishe Yeye na kitu amabacho sina ujuzi nacho kuwa kinastahiki kuabudiwa badala Yake- na hili ni miongoni madhambi makubwa zaidi na maovu zaidi- Na mimi ninawalingania kwenye njia yenye kupelekea kwa Mwenyezi Mungu Aliye Mshindi katika kutesa Kwake, Mwingi wa msamaha kwa aliyerudia Kwake kwa kutubia baada ya kumuasi.
تفسیرهای عربی:
لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِ لَيۡسَ لَهُۥ دَعۡوَةٞ فِي ٱلدُّنۡيَا وَلَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَآ إِلَى ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ
«Ukweli ni kwamba kile mnachoniitia kukiamini hakistahiki kuitiwa wala kutegemewa kwa kupata himaya duniani wala Akhera kwa kuwa chenyewe kina udhaifu na upungufu. Na mjuwe kwamba mwisho wa viumbe vyote ni kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika, na Yeye Atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake, na wale waliokiuka mipaka Yake kwa kufanya vitendo vya uasi, kumwaga damu na kukanusha, wao ndio watu wa Motoni.»
تفسیرهای عربی:
فَسَتَذۡكُرُونَ مَآ أَقُولُ لَكُمۡۚ وَأُفَوِّضُ أَمۡرِيٓ إِلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ
Alipowasihi na wasimkubalie aliwaambia, «Basi mtakumbuka kuwa mimi niliwasihi na nikawakumbusha, na mtajuta wakati ambao majuto hayatanufaisha. Na mimi ninahamia kwa Mola wangu nataka hifadhi Yake na ninamtegemea Yeye, hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, ni Mtambuzi wa hali za waja na malipo wanayostahiki malipo, hakuna kinachofichamana Kwake chochote katika hayo.»
تفسیرهای عربی:
فَوَقَىٰهُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِ مَا مَكَرُواْۖ وَحَاقَ بِـَٔالِ فِرۡعَوۡنَ سُوٓءُ ٱلۡعَذَابِ
Basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Akamuokoa mtu huyo aliyeamini na mateso ya vitimbi vya Fir’awn na jamaa zake, na ikawashukia wao adhabu mbaya, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliwazamisha wote mpaka wa mwisho wao.
تفسیرهای عربی:
ٱلنَّارُ يُعۡرَضُونَ عَلَيۡهَا غُدُوّٗا وَعَشِيّٗاۚ وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ أَدۡخِلُوٓاْ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ أَشَدَّ ٱلۡعَذَابِ
Kwanza walipatikana na gharika wakaangamia, kisha wakawa wanaadhibiwa ndani ya makaburi yao ambapo Moto unaorodheshwa kwao, asubuhi na jioni, mpaka wakati wa kuhesabiwa. Na Siku ambayo Kiyama kitasimama kutasemwa, «Watieni Motoni jamaa wa Fir’awn ukiwa ni malipo ya matendo mabaya waliyoyatenda.» Aya hii ndio msingi wa kuthibitisha adhabu ya kaburini.
تفسیرهای عربی:
وَإِذۡ يَتَحَآجُّونَ فِي ٱلنَّارِ فَيَقُولُ ٱلضُّعَفَٰٓؤُاْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُنَّا لَكُمۡ تَبَعٗا فَهَلۡ أَنتُم مُّغۡنُونَ عَنَّا نَصِيبٗا مِّنَ ٱلنَّارِ
Na pindi watakapogombana watu wa Motoni na kulaumiana wao kwa wao, hapo wajenge hoja wafuasi wenye kuandama dhidi ya viongozi wao wenye kiburi ambao waliwapoteza na wakawapambia njia ya uovu, kwa kuwaambia, «Je, nyinyi mtatuondolea sehemu ya Moto kwa kujibebesha fungu la adhabu yetu?»
تفسیرهای عربی:
قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُلّٞ فِيهَآ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ حَكَمَ بَيۡنَ ٱلۡعِبَادِ
Viongozi waliokuwa na kiburi watasema, wakieleza ulemevu wao, «Hatutawabebea kitu chochote cha adhabu ya Moto, na hali sisi sote tumo ndani yake, hatuna namna ya kuokoka nao, Mwenyezi Mungu Amegawanya adhabu baina yetu kwa uamuzi Wake wa haki, kila mmoja wetu kwa kadiri anayostahiki.»
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ فِي ٱلنَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ٱدۡعُواْ رَبَّكُمۡ يُخَفِّفۡ عَنَّا يَوۡمٗا مِّنَ ٱلۡعَذَابِ
Na watasema wale waliyomo Motoni miongoni mwa watu wakubwa wenye kiburi na wanyonge wakiwaambia walinzi wa Jahanamu, «Muombeni Mola wenu atusahilishie adhabu kwa siku moja ili tupate kiasi fulani cha mapumziko.»
تفسیرهای عربی:
قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ تَكُ تَأۡتِيكُمۡ رُسُلُكُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ قَالُواْ بَلَىٰۚ قَالُواْ فَٱدۡعُواْۗ وَمَا دُعَٰٓؤُاْ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٍ
Washika hazina wa Jahanamu waseme kuwaambia kwa njia ya kuwakaripia na kuwalaumu, «Maombi haya hayatafalia kitu. Kwani hawakuwajia nyinyi Mitume wenu na hoja waziwazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mkawakanusha?» Hapo wale wakanushaji walikubali hilo na wasema, «Ndio, wametujia.» Na washika hazina wa Jahanamu wajiepushe na wao na waseme, «Sisi hatutawaombea wala kuingilia kati kuhusu nyinyi. Ombeni nyinyi wenyewe, lakini dua hiyo haitafalia kitu, kwa kuwa nyinyi ni makafiri, na hayawi maombi ya makafiri isipokuwa ni yenye kupotea, hayakubaliwi wala hayaitikiwi.»
تفسیرهای عربی:
إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ
Sisi tutawapa ushindi mitume wetu na wale waliowafuata, na tutawapa nguvu juu ya wale waliowaudhi katika uhai wa kilimwengu na Siku ya Kiyama, Siku ambayo watatoa ushahdi Malaika, Manabii na Waumini juu ya watu waliopita waliowakanusha Mitume wao; watatoa ushahidi kwamba Mitume walifikisha jumbe za Mola wao na kwamba watu hao waliwakanusha.
تفسیرهای عربی:
يَوۡمَ لَا يَنفَعُ ٱلظَّٰلِمِينَ مَعۡذِرَتُهُمۡۖ وَلَهُمُ ٱللَّعۡنَةُ وَلَهُمۡ سُوٓءُ ٱلدَّارِ
Siku ya kuhesabiwa, hawatanufaika makafiri waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa zile nyudhuru wanazozitoa za kuwakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu. Watakalolipata ni kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na watakuwa na Nyumba mbaya huko Akhera, nayo ni Moto.
تفسیرهای عربی:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡهُدَىٰ وَأَوۡرَثۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡكِتَٰبَ
Kwa hakika tulimpa Mūsā Taurati na miujiza miongoni mwa vitu vinavyoongoza kwenye haki, na tukawafanya Wana wa Isrāīl warithiane Taurati: wanyuma kutoka kwa waliopita,
تفسیرهای عربی:
هُدٗى وَذِكۡرَىٰ لِأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ
hali ya kuwa ni yenye kuongoza kwenye njia ya usawa na ni waadhi kwa wenye akili kamilifu.
تفسیرهای عربی:
فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ بِٱلۡعَشِيِّ وَٱلۡإِبۡكَٰرِ
Basi subiri, ewe Mtume, juu ya udhia wa washirikina, kwani tumekuahidi kulitukuza neno lako, na ahadi yetu ni kweli haiendi kinyume, na utake msamaha wa dhambi zako, na uendelee daima kumtakasa Mola wako na kila sifa isiyonasibiana na Yeye katika kipindi cha mwisho wa mchana na mwanzo wake.
تفسیرهای عربی:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡ إِن فِي صُدُورِهِمۡ إِلَّا كِبۡرٞ مَّا هُم بِبَٰلِغِيهِۚ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
Hakika ya wale wanaoipinga haki kwa ubatilifu, na wanaozirudisha hoja sahihi kwa udanganyifu wa uharibifu bila ya kuwa na dalili wala ushahidi wala hoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hamna ndani ya nyoyo za hao isipokuwa kuifanyia kiburi haki, kwa uhasidi wao juu ya fadhila ambazo Mwenyezi Mungu Amempa mtume Wake na utukufu wa utume ambao Amemkirimu nao, nayo ni mambo wao si wenye kuyafikia wala kuyapata. Basi shikamana na Mwenyezi Mungu akuhifadhi na shari lao, kwani Yeye ni Mwenye kuyasikia maneno yao , ni Mwenye kuyaona matendo yao, na Atawalipa kwayo.
تفسیرهای عربی:
لَخَلۡقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَكۡبَرُ مِنۡ خَلۡقِ ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Hakika ni kwamba uumbaji wa Mwenyezi Mungu wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko kuwaumba watu na kuwarudisha uhai baada ya kufa, lakini wengi wa watu hawajui kwamba uumbaji wa vyote hivyo ni jambo sahali kwa Mwenyezi Mungu.
تفسیرهای عربی:
وَمَا يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَلَا ٱلۡمُسِيٓءُۚ قَلِيلٗا مَّا تَتَذَكَّرُونَ
Na halingani kipofu na anayeona, pia hawalingani Waumini wanaokubali kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu wa haki Asiye na mshirika, wanaowaitikia Mitume Wake na wanaozifuata kivitendo Sheria Zake (hawalingani) na wenye kukataa ambao wanapinga kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki, na wakawakanusha Mitume Wake na wasizifuate Sheria Zake kivitendo. Ni uchache sana kwa nyinyi, enyi watu, kuzikumbuka hoja za Mwenyezi Mungu, mkazingatia na mkawaidhika nazo.
تفسیرهای عربی:
إِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞ لَّا رَيۡبَ فِيهَا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ
Hakika Kiyama ni chenye kuja, hakina shaka. Basi kuweni na yakini ya kuja kwake, kama walivyolitolea habari hilo Mitume. Lakini wengi wa watu hawaamini kuwa kitakuja wala hawafanyi vitendo vya kuwafaa hapo.
تفسیرهای عربی:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ٱدۡعُونِيٓ أَسۡتَجِبۡ لَكُمۡۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِي سَيَدۡخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ
Na Anasema Mola wenu, «Enyi waja! Niombeni Peke Yangu na niabuduni mimi tu, nitawakubalia maombi yenu. Hakika ya wale wenye kufanya kiburi kwa kukataa kunipwekesha katika ibada na ustahiki wa kuabudiwa wataingia Moto wa Jahanamu wakiwa watwevu na wanyonge.
تفسیرهای عربی:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبۡصِرًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ
Mwenyezi Mungu peke Yake Ndiye Aliyewawekea usiku ili mtulie ndani yake na mpate mapumziko yenu, na Ameufanya mchana kuwa na mwangaza ili muendeshe mambo ya maisha yenu. Hakika Mwenyezi Mungu Ana wema mwingi kwa watu. lakini wengi wao hawamshukuru kwa kumtii na kumtakasia ibada.
تفسیرهای عربی:
ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ
Yule Aliyewaneemesha neema hizi si mwingine bali ni Mwenyezi Mungu Mola wenu, Muumba vitu vyote. Hapana Mola Anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Basi ni vipi nyinyi mnajiepusha na kumuamini Yeye na mnamuabudu asiyekuwa Yeye miongoni mwa masanamu, baada ya kuwafunukia dalili Zake.
تفسیرهای عربی:
كَذَٰلِكَ يُؤۡفَكُ ٱلَّذِينَ كَانُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ
Kama mlivyoikanusha haki, enyi makafiri wa Kikureshi, na mkaipa mgongo na mkaenda kwenye ubatilifu, hivyo ndivyo wanavyopotoshwa na haki na kuiamini wale waliokuwa wakizikanusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake.
تفسیرهای عربی:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ قَرَارٗا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءٗ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡۖ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewafanyia hii ardhi ili mtulie hapo, Akawasahilishia kukaa juu yake, Akawafanyia mbingu kuwa ni sakafu ya ardhi, Akaeneza huko alama zenye kuongoza, Akawaumba kwa namna kamilifu zaidi na maumbile mazuri zaidi, Akawaneemesha kwa riziki ya halali na vilaji na vinywaji vyenye ladha. Huyo Aliyewaneemesha nyinyi neema hizi ndiye Mola wenu, Mwingi wa kheri, fadhila na baraka, na Ameepukana na kila kisichonasibiana na Yeye. Na Yeye Ndiye Mola wa viumbe wote.
تفسیرهای عربی:
هُوَ ٱلۡحَيُّ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۗ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Aliye hai Ambaye Ana uhai mkamilifu uliotimia, Hapana Mola isipokuwa Yeye. Basi muombeni na ielekezeni ibada Kwake Yeye, Peke Yake, hali ya kumtakasia Yeye Dini yenu na utiifu wenu. Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu na sifa kamilifu ni Zake, Mola wa viumbe wote.
تفسیرهای عربی:
۞ قُلۡ إِنِّي نُهِيتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَمَّا جَآءَنِيَ ٱلۡبَيِّنَٰتُ مِن رَّبِّي وَأُمِرۡتُ أَنۡ أُسۡلِمَ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina wa watu wako, «Hakika mimi nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu baada ya kunijia mimi alama zilizo wazi kutoka kwa Mola wangu na kuniamrisha mimi nimnyenyekee Yeye na nimfuate kwa utiifu mkamilifu Kwake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Mola wa viumbe wote,»
تفسیرهای عربی:
هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ مِنۡ عَلَقَةٖ ثُمَّ يُخۡرِجُكُمۡ طِفۡلٗا ثُمَّ لِتَبۡلُغُوٓاْ أَشُدَّكُمۡ ثُمَّ لِتَكُونُواْ شُيُوخٗاۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبۡلُۖ وَلِتَبۡلُغُوٓاْ أَجَلٗا مُّسَمّٗى وَلَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Yeye Ndiye Aliyemuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, kisha Akawafanya mpatikane kutokana na manii kwa uweza Wake, na baada yake mnahamia kwenye mwongo wa damu nzito iliyo nyekundu, kisha mnapitiwa na miongo kadha ndani ya vizazi, mpaka mnapozaliwa mkiwa watoto wadogo, kisha umbile lenu linapata nguvu (na mnaendelea hivyo) mpaka mnapokuwa wazee, na miongoni mwenu kuna wanaokufa kabla ya hapo. Na ili mfikie kwa miongo hii kipindi kiliotajwa ambacho hapo umri wenu ukome. Huenda nyinyi mkazitia akilini hoja za Mwenyezi Mungu katika hilo na mkazizingatia aya zake mkajua kuwa hakuna Mola isipokuwa Yeye Anayefanya hilo, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye haitakiwi kuabudiwa isipokuwa Yeye.
تفسیرهای عربی:
هُوَ ٱلَّذِي يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَإِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyepwekeka kwa kuhuisha na kufisha. Na Akiamua jambo Analiambia, «Kuwa!» na likawa, hakuna mwenye kurudisha uamuzi Wake.
تفسیرهای عربی:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ أَنَّىٰ يُصۡرَفُونَ
Je, huwaonei ajabu, ewe Mtume, hawa wakanushaji wa aya za Mwenyezi Mungu vile wanavyoshindana nazo, na hali hizo ziko wazi katika kutolea ushahidi upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza Wake, ni vipi wao wanaziepuka pamoja na usahihi wake? Na wataenda kwenye kitu gani baada ya huu ufafanuzi kamili?
تفسیرهای عربی:
ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِٱلۡكِتَٰبِ وَبِمَآ أَرۡسَلۡنَا بِهِۦ رُسُلَنَاۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Washirikina hawa waliokanusha Qur’ani na Vitabu vya mbinguni Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume Wake ili kuongoza watu, watajua wakanushaji hawa mwisho wa ukanushaji wao.
تفسیرهای عربی:
إِذِ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَٰقِهِمۡ وَٱلسَّلَٰسِلُ يُسۡحَبُونَ
Pindi watakapotiwa pingu kwenye shingo zao na minyonyoro kwenye miguu yao, na huku Malaika wa adhabu wakiwaburuta.
تفسیرهای عربی:
فِي ٱلۡحَمِيمِ ثُمَّ فِي ٱلنَّارِ يُسۡجَرُونَ
Wakiwatia kwenye maji moto yaliyochemka sana na yenye uharara mwingi, kisha wachomwe ndani ya Moto wa Jahanamu.
تفسیرهای عربی:
ثُمَّ قِيلَ لَهُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تُشۡرِكُونَ
Kisha waambiwe kwa kuwasimanga, na wao wako kwenye hali hii ya unguliko , «Wako wapi waungu mliokuwa mkiwaabudu.
تفسیرهای عربی:
مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا بَل لَّمۡ نَكُن نَّدۡعُواْ مِن قَبۡلُ شَيۡـٔٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلۡكَٰفِرِينَ
badala ya Mwenyezi Mungu? Je watawatetea nyinyi leo? Basi waiteni ili wawaokoe na balaa hii iliyowashukia iwapo wataweza.» Hapo wakanushaji waseme, «Wametupotea machoni hatuwaoni, na hawakutunufaisha kitu chochote.» Hapo wakubali kuwa wao walikuwa ujingani katika mambo yao, na kuwa kule kuabudu kwao wale waungu kulikuwa ni ubatilifu usio na faida yoyote. Na kama vile Mwenyezi Mungu Alivyowapoteza hawa waliowapotea katika moto wa Jahanamu waliokuwa wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyowapoteza wale wenye kumkanusha.
تفسیرهای عربی:
ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمۡ تَفۡرَحُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَبِمَا كُنتُمۡ تَمۡرَحُونَ
Adhabu hiyo itakayowapata ni kwa sababu ya kughafilika mliokuwa nako katika uhai wenu wa kilimwengu, kwa kuwa mlikuwa mkifurahika na yale mnayoyatenda ya maasia na madhambi na tabia mliokuwa nazo za gogi, kiburi na kuwafanyia udhalimu waja wa Mwenyezi Mungu.
تفسیرهای عربی:
ٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ فَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ
Ingieni kwenye milango ya Jahanamu ikiwa ni mateso yenu kwa kumkanusha kwenu Mwenyezi Mungu na kumuasi, hali ya kukaa milele humo. Ni mbaya sana Jahanamu kuwa ni mashukio ya wenye kumfanyia kuburi Mwenyezi Mungu duniani.
تفسیرهای عربی:
فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ
Basi vumilia, ewe Mtume, na uendelee katika njia ya ulinganizi, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Atakutekelezea kile Alichokuahidi. Basi, ima tukuoneshe katika uhai wako sehemu ya adhabu tunayowaahidi hawa washirikina au tukufishe kabla ya hiyo adhabu kuwashukia, kwani ni kwetu sisi mwisho wao Siku ya Kiyama, na tutawaonjesha adhabu kali kwa yale waliokuwa wakiyakanusha.
تفسیرهای عربی:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ مِنۡهُم مَّن قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ وَمِنۡهُم مَّن لَّمۡ نَقۡصُصۡ عَلَيۡكَۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأۡتِيَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ فَإِذَا جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ قُضِيَ بِٱلۡحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Hakika tuliwatumiliza kabla yako, ewe Mtume, Mitume wengi kwa watu wao wawalinganie na wavumilie udhia wao. Miongoni mwao kuna wale tuliokuhadithia habari zao, na miongoni mwao kuna wale ambao hatukukuhadithia. Na wote hao wameaminiwa kufikisha wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa watu wao. Na haikuwa ni yenye kuwezekana kwa yoyote miongoni mwao kuleta alama yoyote miongoni mwa alama zinazoonekana au zinazofahamika isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Basi itakapokuja amri ya Mwenyezi Mungu ya kuadhibiwa wakanushaji, itatolewa hukumu ya uadilifu baina ya Mitume na wale waliowakanusha, na hapo watapata hasara waliokuwa wabatilifu kwa kule kumzulia kwao Mwenyezi Mungu urongo na kuabudu kwao asiyekuwa Yeye.
تفسیرهای عربی:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَنۡعَٰمَ لِتَرۡكَبُواْ مِنۡهَا وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ
Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Ndiye Aliyewapa nyinyi wanyama , ili mnufaike nao kwa kupanda na kula
تفسیرهای عربی:
وَلَكُمۡ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَلِتَبۡلُغُواْ عَلَيۡهَا حَاجَةٗ فِي صُدُورِكُمۡ وَعَلَيۡهَا وَعَلَى ٱلۡفُلۡكِ تُحۡمَلُونَ
na manufaa mengineyo, na ili mfikie, kwa kuwabebesha wengineo, haja ya nafsi zenu ya kufika miji ya mbali. Na juu ya wanyama hao mnabebwa barani, na juu ya majahazi mkiwa baharini mnabebwa pia.
تفسیرهای عربی:
وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ فَأَيَّ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ تُنكِرُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anawaonyesha dalili zake nyinygi zilizo wazi zenye kutolea ushahidi uweza Wake na uendeshaji mambo Wake. Basi ni dalili gani miongoni mwa dalili za Mwenyezi Mungu mnazikanusha na hamzikubali?
تفسیرهای عربی:
أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِنۡهُمۡ وَأَشَدَّ قُوَّةٗ وَءَاثَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Kwani hawakutembea kwenye ardhi wakanushaji hawa wakafikiria juu ya maangamivu ya ummah waliokanusha waliokuwa kabla yao ulikuwa vipi mwisho wao? Ummah hao waliopita walikuwa ni wengi kuliko wao kwa idadi, zana na athari ya majengo, viwanda, ukulima na yasiyokuwa hayo. Na yote hayo waliyoyatenda hayakuwafalia kitu ilipowateremkia wao adhabu ya Mwenyezi Mungu.
تفسیرهای عربی:
فَلَمَّا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرِحُواْ بِمَا عِندَهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Walipowajia, hao ummah waliowakanusha, Mitume wao kwa dalili zilizo wazi, walifurahia, kwa ujinga wao, ujuzi walionao unaogongana na yale waliyokuja nayo Mitume, na ikawashukia wao ile adhabu waliokuwa wakiiharakisha kwa njia ya shere na dhihaka. Katika aya hii kuna dalili kuwa kila ujuzi unaogongana na Uislamu au kuutia kombo au kutilia shaka usahihi wake, basi ujuzi huo ni mwenye kutukanika na kuchukiza, na mwenye kuuamini si miongoni mwa wafuasi wa Muhammad, reheme ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
تفسیرهای عربی:
فَلَمَّا رَأَوۡاْ بَأۡسَنَا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥ وَكَفَرۡنَا بِمَا كُنَّا بِهِۦ مُشۡرِكِينَ
Walipoiona adhabu yetu, walikubali wakati ambapo kukubali hakunufaishi, na wakasema, «Tumemuamini Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na tumekikanusha kile ambacho tulikuwa tukikishirikisha katika ibada ya Mwenyezi Mungu.»
تفسیرهای عربی:
فَلَمۡ يَكُ يَنفَعُهُمۡ إِيمَٰنُهُمۡ لَمَّا رَأَوۡاْ بَأۡسَنَاۖ سُنَّتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِي قَدۡ خَلَتۡ فِي عِبَادِهِۦۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Imani yao hiyo haikuwa ni yenye kuwanufaisha walipoiona adhabu yetu, kwa kuwa ni imani ambayo hawakuwa na budi nayo, na si Imani ya hiyari na kutaka. Huo ndio mpango na njia Aliyoiweka kwa ummah wote, kwamba Imani isiwanufaishe wanapoiona adhabu. Na itakapokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu, wataangamia wenye kumkanusha Mola wao, wenye kukataa kumpwekesha na kumtii.
تفسیرهای عربی:
 
ترجمهٔ معانی سوره: سوره غافر
فهرست سوره ها شماره صفحه
 
ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس - لیست ترجمه ها

ترجمهٔ معانی قرآن کریم به زبان سواحلی. ترجمهٔ دکتر عبدالله محمد ابوبکر و شیخ ناصر خمیس.

بستن