ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس * - لیست ترجمه ها


ترجمهٔ معانی آیه: (179) سوره: سوره اعراف
وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٞ لَّا يَفۡقَهُونَ بِهَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٞ لَّا يُبۡصِرُونَ بِهَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٞ لَّا يَسۡمَعُونَ بِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ
Na kwa hakika tuliuumbia Moto - ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Atawaadhibu wanaostahili kuadhibiwa huko Akhera- majini na binadamu wengi, wana nyoyo lakini hawaelewi kwazo, hawatazamii malipo mazuri wala hawaogopi mateso; na wana macho hawaangalii kwayo aya za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, na wana masikio hawasikii kwayo aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuzitia akilini. Hawa ni kama wanyama wasioelewa waambiwacho, wasiofahamu wakionacho na wasiotia akilini kwa nyoyo zao kizuri na kibaya wakaweza kuzitenganisha. Bali wao wamepotea zaidi kuliko hao wanyama, kwani wanyama wanaona yanayowafaa na yanayowadhuru na wanamfuata mchungaji wao. Ama wao ni kinyume cha hilo, wao ndio wenye kughafilika na jambo la kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtii.
تفسیرهای عربی:
 
ترجمهٔ معانی آیه: (179) سوره: سوره اعراف
فهرست سوره ها شماره صفحه
 
ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس - لیست ترجمه ها

ترجمهٔ معانی قرآن کریم به زبان سواحلی. ترجمهٔ دکتر عبدالله محمد ابوبکر و شیخ ناصر خمیس.

بستن