Check out the new design

ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس * - لیست ترجمه ها


ترجمهٔ معانی آیه: (37) سوره: توبه
إِنَّمَا ٱلنَّسِيٓءُ زِيَادَةٞ فِي ٱلۡكُفۡرِۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُحِلُّونَهُۥ عَامٗا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامٗا لِّيُوَاطِـُٔواْ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّواْ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُۚ زُيِّنَ لَهُمۡ سُوٓءُ أَعۡمَٰلِهِمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hakika yale Waarabu walikuwa wakiyafanya katika kipindi cha ujinga kwa kuiharamisha miezi minne kila mwaka, kwa idadi na sio kwa kuyataja majina ya miezi iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, wakawa waichelewesha baadhi yake au waitanguliza, na wakaiweka badala yake miezi ya uhalali kama wanavyotaka, kulingana na mahitaji yao ya kupigana. Hakika hayo ni katika kuzidisha ukafiri. Shetani anawapoteza kwa hayo wale waliokufuru : wanauhalalisha ule waliouchelewesha kuuharamisha kati ya miezi minne mwaka huu, na wanauhalalisha mwaka mwingine, ili walinganishe kiwango cha miezi minne, wapate kuihalalisha Aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu kati ya hiyo. Shetani amewapambia vitendo viovu. Na Mwenyezi Mungu Hawaafikii watu Makafiri kufuata haki na usawa.
تفسیرهای عربی:
 
ترجمهٔ معانی آیه: (37) سوره: توبه
فهرست سوره ها شماره صفحه
 
ترجمهٔ معانی قرآن کریم - ترجمه‌ى سواحلى - عبد الله محمد و ناصر خميس - لیست ترجمه ها

مترجم: دکتر عبد الله محمد ابو بکر و شیخ ناصر خميس.

بستن