Check out the new design

કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની * - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: સબા   આયત:
وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ يَقُولُ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ أَهَٰٓؤُلَآءِ إِيَّاكُمۡ كَانُواْ يَعۡبُدُونَ
Na siku atakayo wakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je! Hawa walikuwa wakikuabuduni?
Na taja, ewe Nabii, siku Mwenyezi Mungu atapo wakusanya wote, na kisha Subhanahu awaambie Malaika mbele ya wale walio kuwa wakiwaabudu: Je! Hawa walikuabuduni nyinyi khasa badala yangu mimi?
અરબી તફસીરો:
قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِمۖ بَلۡ كَانُواْ يَعۡبُدُونَ ٱلۡجِنَّۖ أَكۡثَرُهُم بِهِم مُّؤۡمِنُونَ
Waseme: Subhanak, Umetakasika. Wewe ndiye kipenzi chetu si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao.
Malaika watasema: Sisi tunakutakasa kabisa na kuwa Wewe una mshirika wowote. Wewe ndiye tulio shikamana nawe kwa mapenzi na ut'iifu, sio wao. Hao wameghurika katika madai yao kuwa wanatuabudu sisi. Bali walikuwa wanafuata nyayo za mashetani walio wapambia ushirikina. Wengi wao wakiwasadiki hao.
અરબી તફસીરો:
فَٱلۡيَوۡمَ لَا يَمۡلِكُ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٖ نَّفۡعٗا وَلَا ضَرّٗا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلنَّارِ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
Hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenzie. Na tutawaambia walio dhulumu: Onjeni adhabu ya Moto mlio kuwa mkiukanusha.
Basi Siku ya Mkusanyo hapana atakaye weza kumletea mwenzie manufaa wala kumkinga na madhara. Na tutawaambia walio jidhulumu nafsi zao: Ionjeni adhabu ya Moto ambayo mlio kuwa duniani mkiikanusha.
અરબી તફસીરો:
وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالُواْ مَا هَٰذَآ إِلَّا رَجُلٞ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمۡ عَمَّا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُكُمۡ وَقَالُواْ مَا هَٰذَآ إِلَّآ إِفۡكٞ مُّفۡتَرٗىۚ وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi wanasema: Huyu si chochote ila ni mtu anaye taka kukuzuieni na waliyo kuwa wakiabudu baba zenu. Na wakasema: Haya si chochote ila ni uwongo ulio zuliwa. Na walio kufuru waliiambia Haki ilipo wajia: Haya si chochote ila ni uchawi ulio dhaahiri.
Na makafiri walipo somewa Aya zetu zilio wazi dalili zake kuonyesha Haki, makafiri walisema: Huyu si chochote ila ni mtu anaye taka kukuzuilieni msiwaabudu walio kuwa wakiwaabudu baba zenu. Na pia walisema: Hii Qur'ani si chochote ila ni uwongo ulio tungwa tu. Na walio ikataa Qur'ani ilipo wajia walisema: Hii si chochote ila ni uchawi ulio wazi.
અરબી તફસીરો:
وَمَآ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّن كُتُبٖ يَدۡرُسُونَهَاۖ وَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ قَبۡلَكَ مِن نَّذِيرٖ
Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia Mwonyaji kabla yako wewe.
Na Mwenyezi Mungu hakuwateremshia Waarabu Vitabu vya mbinguni wavisome; wala hutukupata kuwapelekea Mwonyaji kabla yako wa kuwahadharisha na matokeo ya ukafiri wao.
અરબી તફસીરો:
وَكَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَمَا بَلَغُواْ مِعۡشَارَ مَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ فَكَذَّبُواْ رُسُلِيۖ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ
Na walikadhibisha walio kuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyo wapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!
Na kaumu zilizo tangulia ziliwakadhibisha Manabii wao. Na hawa washirikina wa kaumu yako hawajafikia hata sehemu moja katika kumi za nguvu na umadhubuti tulio wapa hao walio tangulia. Wakawakanusha Mitume wangu. Basi ilikuwaje ghadhabu yangu juu yao jinsi nilivyo wakasirikia!
અરબી તફસીરો:
۞ قُلۡ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍۖ أَن تَقُومُواْ لِلَّهِ مَثۡنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُواْۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ لَّكُم بَيۡنَ يَدَيۡ عَذَابٖ شَدِيدٖ
Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote ila ni Mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali.
Waambie: Mimi nakuamrisheni jambo moja tu - Msimame kwa ikhlasi ya kumtakasia Mwenyezi Mungu muache kufuata mitindo yenu ya zamani - katika kuchungua kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, mkigawika wawili-wawili, au mmoja-mmoja, muangalie kwa uadilifu na insafu. Kisha mfikiri khabari ya huyu mwenzenu, Muhammad, ambaye mmeishi naye na mnajua kuwa akili yake ni timamu. Huyu hana wazimu kwa kuliingia jambo hili. Yeye huyu si chochote ila ni Mwonyaji kwenu, anakuhadharisheni msije mkapata adhabu kali inayo kukabilini mbele yenu.
અરબી તફસીરો:
قُلۡ مَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٖ فَهُوَ لَكُمۡۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٞ
Sema: Ujira nilio kuombeni ni wenu nyinyi. Sina ujira ila kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu.
Waambie makafiri: Ujira wowote nilio kutakeni juu ya kufikisha Ujumbe ni kwa maslaha yenu. (Yaani nyinyi mwongoke na mpate malipo kwa Mwenyezi Mungu.) Sina ujira ninao utaraji mimi ila kwa Mwenyezi Mungu. Naye ni Mwenye kuangalia na kuchungua kila kitu.
અરબી તફસીરો:
قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَقۡذِفُ بِٱلۡحَقِّ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Sema: Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa Haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema yaliyo ghaibu.
Waambie: Hakika Mola wangu Mlezi huitupa Haki juu ya baat'ili (uwongo) ikauondoa. Na Yeye ndiye Mwenye kuijua vyema ghaibu; hapana siri inayo fichikana kwake.
અરબી તફસીરો:
 
શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: સબા
સૂરહ માટે અનુક્રમણિકા પેજ નંબર
 
કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા

તેનું અનુવાદ અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની દ્વારા કરવામાં આવ્યું.

બંધ કરો