S'ad: Ni harufi iliyo anzia Sura hii kama zilivyo anzia baadhi ya Sura nyengine kwa mpango wa Qur'ani katika kuanzia kwa harufi moja moja. Naapa kwa Qur'ani yenye utukufu na shani kubwa kuwa hakika hii ni Kweli isiyo na shaka yoyote.
Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa.
Wakubwa wao wakakimbilia kuusiana wao kwa wao wakiambiana: Endeleeni na njia yenu hiyo hiyo, na shikilieni kuiabudu miungu yenu. Kwani hakika tumepangiwa jambo kubwa hili.
Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
Hatujapata kusikia haya mambo ya Tawhidi, kumfanya Mungu mmoja tu, katika dini ya baba zetu tulio wawahi kuwaona. Haya si chochote ila ni uwongo tu ulio zuliwa.
Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?
Bali sisi tunawauliza hawa wanao kuhusudu: Kwani wao wanazo khazina za rehema ya Mola wako Mlezi Mwenye nguvu, Mwingi wa kutoa, hata wao wawe ndio wa kuteua nani wa kumpa Unabii kwa mujibu wa mapenzi ya nafsi zao?
Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko!
Tena tunawauliza: Kwani wao wanao ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo baina yao? Ikiwa hivyo basi nawazipande ngazi mpaka wafikie pahala ambapo watakuwa wakitoa hukumu kama watakavyo, kama wanaweza!
Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.
Kabla ya hawa, walikadhibisha kaumu ya Nuhu, kina A'adi na Firauni aliye kuwa na majengo makubwa yaliyo simama imara kama milima, na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako.
Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.
Na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako.
Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.
Ewe Muhammad! Yastahamilie hayo wanayo yasema juu yako washirikina. Na mkumbuke mja wetu, Daudi, mwenye nguvu katika Dini na dunia. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika hali zote.
Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.
Hakika Sisi tuliidhalilisha milima pamoja naye, yeye akichuma manufaa kutoka humo, na hiyo milima ikimtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kila upungufu, wakati wa mwisho wa mchana na mwanzo wake.
Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.
Na pia tukamdhalilishia ndege walio kusanywa kutokana na kila namna na kila pahali. Vyote hivyo, milima na ndege, vikimwitikia Daudi kama atakavyo, akivisarifu kama apendavyo kwa maslaha ya umma.
Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani?
Ewe Muhammad! Ati imekujia khabari ya makhasimu wagombanao, walio mjia Daudi kwa kupindukia kuta za mihrabuni palipo kuwa pahala pake pa ibada? Hawakupita mlangoni.
Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.
Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa, akababaika. Wakasema: Usikhofu kitu. Sisi ni wenye kuzozana, tumedhulumiana. Basi tuhukumu kwa uadilifu wala usiupindukie huo uadilifu. Na tuongoze kwenye njia iliyo sawa sawa.
Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.
Mmoja wa hao wagombanao alisema: Hakika huyu ndugu yangu anao kondoo wa kike tisiini na tisa, na mimi ninaye kondoo mmoja tu. Akasema: Nache niwe nakuchungia kama ninavyo wachunga wangu. Na akanishinda katika usemi.
Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.
Daudi akasema kabla hajasikia maneno ya yule mwenye ugomvi mwengine: Hakika huyo amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako amchanganye na wale wake. Na hakika wengi wenye kushirikiana hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa wale ambao Imani yao imetulia katika nyoyo zao, na wakawa wanatenda mema. Na watu kama hao ni wachache, shida kupatikana. Na Daudi akajua kuwa jambo hili si chochote ila ni mtihani tuliyo mfanyia Sisi. Basi akaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na akainama kurukuu kwa Mwenyezi Mungu, na akarejea kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu.
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
Na Mwenyezi Mungu alimfunulia kwa kumwambia: Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa, yaani Naibu, wetu katika ardhi. Basi wahukumu watu kwa sharia niliyo kupa, wala usiendeshe hukumu kufuata matamanio yao, yakakupotosha njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wendao pogo na njia ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata matamanio yao wao watapata adhabu kali kwa kughafilika kwao na Siku ya Malipo.
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata.
Wala Sisi hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa mchezo. Hayo ndiyo wanayo yadhania makafiri. Na kwa hivyo wakapitisha hukumu kwa mujibu wa pumbao zao. Basi hao walio kufuru watapata adhabu kali ya Moto.
Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu?
Inaelekeana vipi na hikima yetu na uadilifu wetu tuwafanye sawa baina ya Waumini wenye kutenda mema, na wale wanao fanya uharibifu katika ardhi? Au yaelekea vipi tuwaweke sawa baina ya wenye kuikhofu adhabu yetu na wakaiogopa ikabu yetu na wale walio waasi wakenda kinyume na hukumu zetu?
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
Ewe Muhammad! Hichi tulicho kuteremshia ni Kitabu chenye manufaa mengi, ili wenye akili nzuri na nyoyo za kufahamu wapate kuzielewa Aya zake, na wawaidhike kwazo.
Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.
Na Daudi tulimtunukia mwana, aitwaye Suleiman, mwenye kustahiki sifa nzuri, ambaye anafaa kuitwa, "Mja mwema kweli". Kwa sababu yeye alikuwa mwingi mno wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika kila hali.
Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.
Suleiman akasema: Hakika mimi nimenyweshwa mapenzi ya farasi, kwa sababu hawa ni katika matayarisho ya mambo ya kheri, nayo ni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Mapenzi haya yametokana na kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Na hakusita kushughulika kuwaangalia mpaka wakapotea machoni mwake.
Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.
Na hakika Sisi tulimfanyia mtihani Suleiman ili asighurike na heba ya ufalme. Tukaweka juu ya kiti chake kiwiliwili kisicho weza kuendesha mambo. Akautambua mtihani, akarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akatubu.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
Suleiman alimwomba Mola wake Mlezi kwa kurejea kwake: Mola wangu Mlezi! Nighufirie yaliyo toka kwangu kwa ghafla, na unitunukie ufalme usio elekea yeyote kuupata baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kutunukia, na ndiye Mwingi wa kutoa.
Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
Na akamfunulia kwa wahyi : Haya tuliyo kuneemesha kwayo ni kipawa kilicho toka kwetu. Yaani ni Sisi tulio kupa. Basi mpe umtakaye, na mnyime umtakaye. Hapana hisabu juu yako kwa kutoa au kunyima.
(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa.
Tukamuitikia na tukamwambia: Ipige ardhi kwa mguu wako, yatatimbuka maji baridi, utakoga na utakunywa hayo, na kwa hivyo yatakuondokea machofu na adhabu.
Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
Tukamkusanyia watu wake walio kuwa wametapanyika mbali naye siku zile za mateso yake. Na tukamzidishia wenginewe kama wale. Na tulifanya hayo kuwa ni rehema kutokana nasi, na ili yawe ni mawaidha kwa wenye akili, wapate kujua kuwa matokeo ya subira ni faraji.
Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
Ayubu alikuwa kaapa kuwa atampiga mmoja wapo katika ahali zake fimbo kadhaa wa kadhaa. Mwenyezi Mungu alimhalalishia aondoe kiapo chake kwa kuchukua kifungu cha fimbo idadi ile ile alio apia kuwa atampigia. Basi kwa kile kifungu cha fimbo ampige aliye apa kuwa atampiga, na hapo yamini yake itakuwa imetimia kwa uchache wa machungu. Mwenyezi Mungu ndiye aliye mneemesha kwa neema hizi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimwona kuwa ni mtu aliye vumilia masaibu yake. Kwa hivyo amestahiki sifa. Mbora wa kusifiwa kwa ibada ni yeye, kwa sababu yeye ni mwingi mno wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika kila jambo.
Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri.
Haya tuliyo kusimulia ni khabari za baadhi ya Mitume ili kukukumbusha wewe na kuwakumbusha watu wako. Na hakika wachamngu walio jikinga na kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu watapata marejeo mazuri na natija njema.
Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
Na huko Peponi watakuwa na wake ambao macho yao hayawatazami ila waume zao tu, hawawaangalii wengineo, nao ni wa miaka sawa na waume zao. Kwa hivyo wameelekeana kuwafikiana.
Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
Na majabari, wale marais wa washirikina, wataambiwa: Hawa chungu ya watu wanao ingia Motoni pamoja nanyi kwa kusukumana na kwa shida, ni wafwasi wenu. Wale marais watasema: Hawana mapokezi mema hao! Hakika hao wanaingia Motoni wapate kuteseka kwa mvukuto wake.
Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa!
Na wafwasi hao watasema: Bali nyinyi ndio mnastahiki zaidi hayo maapizo mnayo tuapizia sisi, kwani nyinyi ndio mlio tuletea adhabu hii kwa vile mlivyo tudanganya na mkatuitia ukafirini, nasi tukakufuru kwa sababu yenu. Basi nyumba ovu kabisa ya kukaa ni Jahannamu!
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?
Na watu wa Motoni watasema: Mbona hatuwaoni wale watu ambao tulikuwa duniani tukiwahisabu kuwa ndio katika waovu, na wa duni, wasio kuwa na jema lolote? Na watu hao ni wale mafakiri wa Kiislamu.
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu,
Ewe Muhammad! Waambie washirikina: Hakika mimi ni mwenye kukuonyeni na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wake, Mtenda nguvu, Mwenye kumshinda kila mwenye madaraka.
Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana.
Mimi sikuwa nikijua khabari za watukufu walio juu walipo kuwa wakizozana juu ya shauri ya Adam, kwa sababu mimi sikupitia njia za kupata ilimu zilizo zowewa na watu za kusoma vitabu au kupokea masomo kwa wataalamu. Njia yangu mimi ya kujua ni kwa kufunuliwa kwa Wahyi.
Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri.
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.
Malaika wote wakafanya kama walivyo amrishwa, wakamuangukia wakisujudu, isipo kuwa Iblisi. Yeye hakusujudu, na akajiona bora na akapanda kiburi, na akawa miongoni mwa makafiri.
Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ewe Iblisi! Nini kilicho kuzuilia kumsujudia niliye muumba Mimi mwenyewe bila ya kuingiliwa na yeyote kati yake! Umejiona mkubwa hali nawe si mkubwa, au hakika wewe nafsi yako ni katika walio shinda ukubwa?
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kumlipa Iblisi kwa kiburi chake cha kukataa amri ya Mola wake Mlezi, alimwambia: Basi toka kwenye kundi la watukufu walio juu, kwani wewe umekwisha fukuzwa kutokana na rehema yangu!
Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,
Iblisi akasema: Basi naapa kwa Ukubwa wako na Utukufu wako, kwa yakini nitawapoteza watu wote, isipo kuwa waja wako ulio wateuwa kwa ajili ya kukut'ii Wewe. Hao sina madaraka nao.
Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Haki ndiyo yamini yangu na kiapo changu; na wala sisemi ila Haki. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa jinsi yako ya kishetani na watakao kufuata katika vizazi vya Adam wote. Hapana khitilafu kwangu baina ya wafuasi na wanao fuatwa.
Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.
Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Haki ndiyo yamini yangu na kiapo changu; na wala sisemi ila Haki. Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa jinsi yako ya kishetani na watakao kufuata katika vizazi vya Adam wote. Hapana khitilafu kwangu baina ya wafuasi na wanao fuatwa.
Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.
Ewe Muhammad! Waambie umma wako: Mimi sikuombeni ujira kwa ajili ya haya niliyo amrishwa nikufikishieni yaliyomo katika Qur'ani na Wahyi. Wala mimi si katika hao wanao jipamba na yasiyo kuwa yao, hata nijidai Unabii.
Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.
Na hapana shaka nyinyi, mnao ikadhibisha Qur'ani, mtakuja jua karibuni hivi ukweli uliomo ndani yake wa ahadi, na maonyo, na khabari za mambo yatakayo kuja, na Ishara za ulimwengu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
સંશોધનના પરિણામો:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".