Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Sura: Al'roum   Aya:
قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلُۚ كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّشۡرِكِينَ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wenye kuyakanusha uliyokuja nayo, «Tembeeni kwenye sehemu za ardhi matembezi ya kuzingatia na kutia mambo akilini, na mtazame vile ulivyokuwa mwisho wa ummah waliopita wenye kukanusha, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd, mtakuta kwamba mwisho wao walioishia ulikuwa mbaya zaidi na kikomo hiko walichokomea kilikuwa kibaya zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
Tafsiran larabci:
فَأَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ ٱلۡقَيِّمِ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۖ يَوۡمَئِذٖ يَصَّدَّعُونَ
Basi elekeza uso wako, ewe Mtume, upande wa Dini iliyonyoka, nayo ni Uislamu, hali ya kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha makatazo yake. Na ushikamane nayo kabla Siku ya Kiyama haijaja, kwani ijapo Siku hiyo, ambayo hakuna anayeweza kuirudisha, viumbe watapambanuka wakiwa makundi- makundi yalio tafauti ili waoneshwe matendo yao.
Tafsiran larabci:
مَن كَفَرَ فَعَلَيۡهِ كُفۡرُهُۥۖ وَمَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا فَلِأَنفُسِهِمۡ يَمۡهَدُونَ
Mwenye kukanusha basi mateso ya ukanushaji wake yatamshukia yeye, nayo ni kukaa milele Motoni. Na mwenye kuamini na akafanya matendo mema basi hao wanajitayarishia wenyewe makao ya Peponi, kwa sababu ya kushikamana kwao na utiifu wa Mola wao.
Tafsiran larabci:
لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن فَضۡلِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Hivyo basi Mwenyezi Mungu Awalipe wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema kwa fadhila Zake na wema Wake, hakika Yeye Hawapendi wakanushaji kwa kuwa Ana hasira na ghadhabu juu yao.
Tafsiran larabci:
وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن يُرۡسِلَ ٱلرِّيَاحَ مُبَشِّرَٰتٖ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحۡمَتِهِۦ وَلِتَجۡرِيَ ٱلۡفُلۡكُ بِأَمۡرِهِۦ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu zenye kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu wa kweli Peke Yake, Asiye na Mshirika, na kuwa Ana uweza mkubwa, ni kule kutuma upepo mbele ya mvua ukiwa ni wenye kuleta habari njema, kwa kuyasukuma mawingu, hapo nafsi zikaingiwa na furaha kwa hilo, ili awaonjeshe rehema Yake kwa kuwateremshia mvua ambayo kwayo miji inahuika na pia waja, na ili jahazi zitembee baharini kwa amri Yake na matakwa Yake, na ili mtafute fadhila Zake kwa kufanya biashara na megineyo. Mwenyezi Mungu Amefanya hayo yote ili mzishukuru neema Zake na mmuabudu Yeye Peke Yake.
Tafsiran larabci:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَٱنتَقَمۡنَا مِنَ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيۡنَا نَصۡرُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Kwa hakika tuliwatuma kabla yako wewe, ewe Mtume, Mitume waende kwa watu wao kwa kubashiria na kuonya, wawaite kwenye upwekeshaji (wa Mwenyezi Mungu) na wawatahadharishe na ushirikina. Wakawajia na miujiza na hoja zenye mwangaza, na wengi wao wakamkanusha Mola wao, na kwa hivyo tukawatesa wale waliotenda mabaya miongoni mwao, tukawaangamiza na tukawapa ushindi wafuasi wa Mitume. Na hivyo ndivyo tunavyowafanya wenye kukukanusha wanapoendelea kukukanusha na wasiamini.
Tafsiran larabci:
ٱللَّهُ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ فَتُثِيرُ سَحَابٗا فَيَبۡسُطُهُۥ فِي ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ يَشَآءُ وَيَجۡعَلُهُۥ كِسَفٗا فَتَرَى ٱلۡوَدۡقَ يَخۡرُجُ مِنۡ خِلَٰلِهِۦۖ فَإِذَآ أَصَابَ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ إِذَا هُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayetuma upepo ukayasukuma mawingu yaliyojaa maji, na Mwenyezi Mungu Akayasambaza mbinguni vile Anavyotaka, Akayafanya ni vipande vilivyotenganika mbalimbali, hapo ukaiona mvua inatoka mawinguni. Na Aipelekapo Mwenyezi Mungu kwa waja wake, ghafla utawakuta wameingiwa na bashasha na wanafurahi kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amewaletea hiyo.
Tafsiran larabci:
وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيۡهِم مِّن قَبۡلِهِۦ لَمُبۡلِسِينَ
Na ingawa wao kabla ya kuteremka mvua walikuwa katika hali ya kukata tamaa na kutokuwa na matumaini kwa sababu ya kutonyeshewa na mvua.
Tafsiran larabci:
فَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ ءَاثَٰرِ رَحۡمَتِ ٱللَّهِ كَيۡفَ يُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Basi Tazama, ewe mwenye kuangalia, mtazamo wa kutia akilini na kuzingatia, athari za mvua kwenye mimea, nafaka na miti, ujionee vipi Mwenyezi Mungu Anaipa uhai ardhi baada ya kuwa imekufa, Akaiotesha mimea na nyasi? Hakika Yule aliyeweza kuihuisha ardhi hii Ndiye Atakayehuisha wafu, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Al'roum
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Dr. Abdullahi Muhammad Abubakar da Sheikh Nasir Khamis suka fassarata.

Rufewa