Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da yaren Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Aya: (145) Sura: Suratu Al'a'raf
وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Na tulimuandikia Mūsā katika Taurati mawaidha ya kila anachokihitajia katika hukumu za Dini yake, ili yapatikane makemeo na mazingatio, na maelezo yanayofafanua mambo ambayo walikalifishwa nayo ya halali na ya haramu, maamrisho na makatazo, visa, mambo ya itikadi, habari na mambo yasiyoonekana. Mwenyezi Mungu Alimwambia, «Basi yashike kwa nguvu.» Yaani, ishike Taurati kwa kwa bidii na hima. «Na uwaamrishe watu wako wazitumie sheria za Mwenyezi Mungu zilizomo humo. Hakika mwenye kushirikisha miongoni mwao na wengineo, mimi nitamuonesha huko Akhera nyumba ya waasi, nayo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ambao Ameutayarisha kwa maadui Wake waliyotoka nje ya utiifu Wake.»
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Aya: (145) Sura: Suratu Al'a'raf
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da yaren Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

Rufewa