Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da yaren Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Aya: (163) Sura: Suratu Al'a'raf
وَسۡـَٔلۡهُمۡ عَنِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَتۡ حَاضِرَةَ ٱلۡبَحۡرِ إِذۡ يَعۡدُونَ فِي ٱلسَّبۡتِ إِذۡ تَأۡتِيهِمۡ حِيتَانُهُمۡ يَوۡمَ سَبۡتِهِمۡ شُرَّعٗا وَيَوۡمَ لَا يَسۡبِتُونَ لَا تَأۡتِيهِمۡۚ كَذَٰلِكَ نَبۡلُوهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Na waulize, ewe Mtume, hawa Mayahudi kuhusu habari ya watu wa kijiji kilichokuwa karibu ya bahari, ambacho watu wake walikuwa wakipita mipaka siku ya Jumamosi kwa kufanya mambo yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, kwani Alikuwa Amewaamrisha waitukuze siku ya Jumamosi na wasivue samaki siku hiyo. Mwanyezi Mungu Akawajaribu na kuwapa mtihani, wakawa samaki wao wawajia siku ya Jumamosi kwa wingi wakiwa juu ya uso wa bahari, na Jumamosi ikipita wakawa samaki wanapotea na hawawaoni kabisa. Basi wakawa wafanya hila ya kuwatega siku ya Jumamosi kwenye mashimo na kuwavua baada yake. Na kama tulivyowaelezea vile Mwenyezi Mungu Alivyowajaribu na kuwapa mtihani kwa kuwatoa samake juu ya bahari katika siku ambayo waliharamishiwa kuwavua na kuwaficha wasiwaone katika siku ambazo ni halali kwao kuwavua, ndivyo tunavyowafanyia mtihani wao kwa sababu ya uasi wao na kutoka kwao kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Aya: (163) Sura: Suratu Al'a'raf
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da yaren Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

Rufewa