Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Sura: Houd   Aya:
فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا جَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهَا حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٖ مَّنضُودٖ
Basi ilipokuja amri yetu, tuliigeuza nchi juu chini, na tukaiteremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu uliokamatana wa Motoni.
Tafsiran larabci:
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَۖ وَمَا هِيَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ بِبَعِيدٖ
Zilizotiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na madhalimu wengineo.
Tafsiran larabci:
۞ وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ وَلَا تَنقُصُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَۖ إِنِّيٓ أَرَىٰكُم بِخَيۡرٖ وَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ مُّحِيطٖ
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu yoyote isipokuwa Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi ninawaona mmo katika hali njema, nami ninawahofia adhabu ya Siku kubwa hiyo itakayowazunguka.
Tafsiran larabci:
وَيَٰقَوۡمِ أَوۡفُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Na enyi kaumu yangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msienee katika ardhi mkifanya uharibifu.
Tafsiran larabci:
بَقِيَّتُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ
Alivyowabakishia Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. Wala mimi siye mlinzi wenu.
Tafsiran larabci:
قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأۡمُرُكَ أَن نَّتۡرُكَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوۡ أَن نَّفۡعَلَ فِيٓ أَمۡوَٰلِنَا مَا نَشَٰٓؤُاْۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلۡحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Je, ni sala zako ndizo zinazokuamrisha tuyaache yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu mno!
Tafsiran larabci:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sitaki kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza. Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye ninarudi.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Houd
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Fassara ta wani gungu na cibiyar fassara ta Ruwwad tare da haɗin gwiwar Ƙungiyar Da'awa ta Rabwah da Ƙungiyar Hidimar Abun ciki na Musulunci a harsuna.

Rufewa