Check out the new design

Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori


Fassarar Ma'anoni Sura: Houd   Aya:
أُوْلَٰٓئِكَ لَمۡ يَكُونُواْ مُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَۘ يُضَٰعَفُ لَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ مَا كَانُواْ يَسۡتَطِيعُونَ ٱلسَّمۡعَ وَمَا كَانُواْ يُبۡصِرُونَ
Hao hawakuwa ni wa kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu. Watazidishiwa adhabu. Kwa kuwa, hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona.
Tafsiran larabci:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Hao ndio waliozihasiri nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
Tafsiran larabci:
لَا جَرَمَ أَنَّهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡأَخۡسَرُونَ
Hakuna shaka kwamba wao katika Akhera ndio waliohasiri zaidi.
Tafsiran larabci:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَأَخۡبَتُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Hakika, wale walioamini, na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi, hao ndio wenza wa Pepo, humo watadumu.
Tafsiran larabci:
۞ مَثَلُ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ كَٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡأَصَمِّ وَٱلۡبَصِيرِ وَٱلسَّمِيعِۚ هَلۡ يَسۡتَوِيَانِ مَثَلًاۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Mfano wa makundi mawili haya ni kama kipofu na kiziwi, na mwenye kuona na anayesikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamkumbuki?
Tafsiran larabci:
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Na hakika, tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akawaambia, "Hakika mimi ni mwonyaji aliye wazi kwenu."
Tafsiran larabci:
أَن لَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ أَلِيمٖ
Ya kwamba msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Hakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku Chungu.
Tafsiran larabci:
فَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرٗا مِّثۡلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمۡ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ ٱلرَّأۡيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلِۭ بَلۡ نَظُنُّكُمۡ كَٰذِبِينَ
Basi wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Hatukuoni wewe isipokuwa ni mtu tu mfano wetu, wala hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale wetu walio duni, watu wasiokuwa na maoni. Wala hatuwaoni nyinyi kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tunawadhania nyinyi kuwa ni waongo."
Tafsiran larabci:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِهِۦ فَعُمِّيَتۡ عَلَيۡكُمۡ أَنُلۡزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمۡ لَهَا كَٰرِهُونَ
Akasema, "Enyi kaumu yangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyotoka kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikafichwa kwenu. Je, tuwalazimishe kuikubali ilhali nyinyi mnaichukia?"
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Houd
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Cibiyar fassara ta Ruwwad - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

Fassara ta wani gungu na cibiyar fassara ta Ruwwad tare da haɗin gwiwar Ƙungiyar Da'awa ta Rabwah da Ƙungiyar Hidimar Abun ciki na Musulunci a harsuna.

Rufewa