Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Surah: An-Naḥl   Ayah:
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ
Kisha hakika Mola wako, kwa wale waliofanya maasia, kwa kutojua mwisho wake na kwamba yanapasisha hasira za Mwenyezi Mungu - kwani kila anayemuasi Mwenyezi Mungu, kwa kukosea au kwa kusudia, huwa ni mjinga kwa mtazamo huu, hata kama anajua kuwa ni haramu-, kisha wakarudi kwa Mwenyezi Mungu na kuyaepuka yale madhambi waliokuwa wakiyafanya na wakazitengeneza nafsi zao na matendo yao, hakika Mola wako, baada ya kutubia kwao na kutengenea kwao, ni Mwenye kuwasamehe, ni Mwenye huruma kwao.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةٗ قَانِتٗا لِّلَّهِ حَنِيفٗا وَلَمۡ يَكُ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Hakika Ibrāhīm alikuwa kiongozi katika mema, na alikuwa mtiifu mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, haendi kombo na Uislamu, ni mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, si mwenye kumshirikisha.
Tafsir berbahasa Arab:
شَاكِرٗا لِّأَنۡعُمِهِۚ ٱجۡتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na alikuwa ni mwenye kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu kwake. Mwenyezi Mungu Alimchagua kwa ujumbe Wake na Akamuongoza kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَءَاتَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na tulimpa ulimwenguni neema nzuri ya kusifiwa na watu waliokuja nyuma yake, kufuatwa na kuwa na watoto wema. Na yeye, mbele ya Mwenyezi Mungu, huko Akhera, ni miongoni mwa watu wema wenye daraja za juu.
Tafsir berbahasa Arab:
ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Kisha tukakuletea wahyi, ewe Mtume, kwamba uifuate dini ya Uislamu kama alivyoifuata Ibrāhīm na kwamba ulingane juu yake na usiiyepuke, kwani Ibrāhīm hakuwa ni miongoni mwa wale wanaowashrikisha wengine pamoja na Mwenyezi Mungu.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ
Mwenyezi Mungu Ameufanya utukuzaji wa siku ya Jumamosi, kwa kuitenga kwa kufanya ibada ndani yake, kwa Myahudi ambao walitafautiana na Nabii wao juu yake, na wakaiteua badala ya siku ya Ijumaa ambayo waliamrishwa waitukuze. Hakika Mola wako , ewe Mtume, ni Mwenye kuhukumu baina ya wale waliotafautiana na Nabii wao Siku ya Kiyama na kumlipa kila mmoja kwa yale anayofaa kuyapata.
Tafsir berbahasa Arab:
ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ
Lingania, ewe Mtume, wewe na aliyekufuata, kwenye Dini ya Mola wako na njia Yake iliyolingana sawa kwa kutumia hekima ambayo Mwenyezi Mungu alikuletea wahyi nayo ndani ya ya Qur’ani na Sunnah. Na uwazungumzie watu kwa njia inayolingana na wao, uwape nasaha kwa njia nzuri yenye kuwavutia kwenye kheri na kuwakimbiza wajiepushe na shari, na ujadiliane na wao kwa njia nzuri za kujadiliana za utaratibu na upole, kwani si juu yako isipokuwa ni kufikisha ujumbe, na ushafikisha. Ama kuwafanya waongoke, hilo ni juu ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Yeye Ndiye Anayemjua zaidi yule aliyepotea na akaiyepuka njia Yake, na Yeye Anawajua zaidi walioongoka.
Tafsir berbahasa Arab:
وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ
Na mkitaka kuwalipiza kisasi, enyi Waumini, wale waliowafanyia uadui, msiongeze zaidi ya vile walivyowafanya. Na mkisubiri, basi hilo ni bora kwenu nyinyi ulimwenguni, kwa kupewa ushindi, na kesho Akhera, kwa kupewa malipo makubwa.
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ
Na vumilia, ewe Mtume, kwa maudhi yanayokupata katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka ikujie faraji, na hakukuwa huku kuvumilia kwako isipokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye Ndiye mwenye kukusaidia na kukupa uthabiti, na usisikitike juu ya wale wanaoenda kinyume na wewe na wasiitikie ulinganizi wako, wala usiwe na usijitie dhiki za moyo kutokana na hila zao na vitimbi vyao, kwani hilo litawarudia wao wenyewe kwa shari na mateso.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ
Kwa hakika Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwa taufiki Yake, msaada Wake, upaji nguvu Wake na nusura Yake Yuko pamoja na waliomcha kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kuyaepuka Aliyoyakataza; na yuko pamoja na wale wanatenda wema, kwa kutekeleza faradhi Zake na kusimama kutimiza haki Zaka na kujilazimisha kumtii, kwa kuwapa msaada Wake, uongozi Wake na nusura Yake.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: An-Naḥl
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis - Daftar isi terjemahan

Diterjemahkan oleh Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakar dan Syekh Nasir Khamis.

Tutup