Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Ayah: (101) Surah: Surah Al-A'rāf
تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Miji hiyo iliyotangulia kutajwa, nayo ni miji ya watu wa Nūḥ„ Hūd, Ṣāliḥ, Lūṭ, na Shu'ayb, tunakupatia, ewe Mtume, habari zake na zile zinazohusu mambo ya Mitume wa Mwenyezi Mungu waliotumwa kwa watu wa miji hiyo, zinazofanya mazingatio yapatikane kwa wenye kuzingatia na pia makemeo kwa madhalimu. Hakika watu wa miji hiyo walijiwa na Mitume wetu na hoja zilizo wazi juu ya ukweli wao, lakini hawakuwa ni wenye kuyaamini yale waliyokuja nayo hao Mitume kwao kwa sababu ya kupita mipaka kwao na kuikanusha haki. Na mfano Alivyopiga chapa Mwenyezi Mungu kwenye nyoyo za makafiri hawa waliotajwa, Atapiga mhuri kwenye nyoyo za wenye kumkanusha Muhammad (S.A.W.).
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Ayah: (101) Surah: Surah Al-A'rāf
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis - Daftar isi terjemahan

Terjemahan makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke bahasa Sawahili oleh Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakar dan Syekh Nasir Khamis

Tutup